Bungoma: Wanafunzi 36 wa Shule ya Wasichana ya Bakisa wapata Ujauzito

Bungoma: Wanafunzi 36 wa Shule ya Wasichana ya Bakisa wapata Ujauzito

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312

​
Wanafunzi takriban 36 katika Shule ya Wasichana ya Bakisa, iliyopo Webuye Mashariki, Kaunti ya Bungoma, wameripotiwa kuwa wajauzito au tayari ni kina mama.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ruth Mulik, ameeleza kushtushwa na kusikitishwa na ongezeko la mimba za utotoni miongoni mwa wanafunzi wa shule hiyo. Akizungumza kwenye mkutano, alisema alipoomba orodha ya wanafunzi wenye mimba na wale ambao tayari wamejifungua, idadi hiyo ilifikia 36.

Mulik ameonyesha wasiwasi kuhusu jinsi swala la mimba za utotoni linavyoonekana kuchukuliwa kwa urahisi miongoni mwa wanafunzi bila hofu. Hali hii imeanza kuathiri vibaya maendeleo ya masomo katika shule hiyo na jamii kwa ujumla.


Source : CitizenTv
 
Huko sheria zao zinasemaje mwanafunzi akipata mimba?
 
Hayo Ndo matokeo ya kuluhusu wanafunzi wakizaa waendelee na masomo
 
Back
Top Bottom