Bureau 121 : North Korea na Ajira Rasmi ya Wadukuzi wa Mitandaoni

Teknocrat

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2018
Posts
8,472
Reaction score
17,249
APT - Advance Persistence Threat - Maana yake hawachoki wala hawapoi

Fikiria serikali ya nchi inaamua kuunda kitengo cha udukuzi mahususi kuiba hela mitandaoni

Mnamo 1998 chini ya amri ya kiongozi wa zamani Kim Jong-il, Serikali ya Korea Kaskazini iligundua mapema kuwa vita vya mtandaoni ni njia ya gharama nafuu lakini yenye athari kubwa (asymmetrical warfare) dhidi ya maadui zao wenye nguvu kubwa ya kijeshi kama Marekani na Korea Kusini.

Hapo ndipo kitengo 121 au Bureau 121 kilipoanzishwa
Hii ni idara ya siri ya mashambulizi ya mtandaoni (cyberwarfare agency) ya Korea Kaskazini inayofanya kazi chini ya Idara Kuu ya Upelelezi ya nchi hiyo (Reconnaissance General Bureau - RGB).
Kundi hili ambalo mara nyingi linahusishwa na majina kama vile APT38, Lazarus Group, au Bluenoroff, linafahamika duniani kote kwa kufanya ujasusi wa kidijitali, mashambulizi dhidi ya miundombinu, na wizi wa kifedha mtandaoni ili kuipatia serikali ya Korea Kaskazini fedha za kigeni.

Ajira na Waajiiriwa
Wafanyakazi wa kitengo hiki wanachaguliwa kutoka miongoni mwa wanafunzi wenye vipaji vikubwa vya hisabati na sayansi ya kompyuta nchini humo. Wengi wao hufundishwa katika Chuo Kikuu cha Kijeshi cha Mirim na baadaye kupelekwa nchi za nje kama China, Urusi, na nchi za Kusini-Mashariki mwa Asia ili kufanya oparesheni zao kwa siri ili kuzuia kufuatiliwa kwa anuani za mtandao (IP addresses) za Korea Kaskazini.


Muundo na Vikundi vya Ndani
Kitengo 121 kinakadiriwa kuwa na wadukuzi zaidi ya 10, 000 (hackers) wasomi wanaofanya kazi katika vitengo vidogo maalum:

Unit 180 (Kikundi cha Kifedha): Hawa wamebobea mahususi katika kudukua mabenki, taasisi za kifedha, na masoko ya sarafu za kidijitali (Cryptocurrency) ili kupata fedha zinazosaidia kufadhili miradi ya silaha za nyuklia ya Korea Kaskazini.
Lab 110 na Kikundi cha Lazarus: Hufanya kazi ya ujasusi wa kijeshi na kisiasa pamoja na kuharibu miundombinu ya kimkakati ya nchi maadui kama vile mifumo ya umeme na mawasiliano ya Korea Kusini.

Kundi hili limehusishwa na baadhi ya mashambulizi makubwa na hatari zaidi ya mtandaoni katika historia ya dunia, yakiwemo:

Shambulio dhidi ya Sony Pictures (2014): Ofisi 121 ilidukua mifumo ya kampuni ya filamu ya Sony Pictures ili kuzuia kutoka kwa filamu ya ucheshi ya "The Interview", ambayo ilikuwa inamkejeli kiongozi Kim Jong-un. Walivujisha data za siri za kampuni hiyo na kuharibu kompyuta nyingi.

Wizi wa Benki ya Bangladesh (2016): Walifanikiwa kudukua mfumo wa kifedha wa kimataifa wa SWIFT na kujaribu kuiba dola bilioni 1 kutoka Benki Kuu ya Bangladesh. Walifanikiwa kuondoka na dola milioni 81 kupitia akaunti za siri nchini Ufilipino kabla ya kusitishwa.

Virusi vya WannaCry (2017): Kitengo 121 kinalaumiwa kwa kusambaza virusi vya ransomware vya WannaCry vilivyofunga mifumo ya kompyuta zaidi ya 300,000 katika nchi 150, zikiwemo hospitali za shirika la afya la NHS nchini Uingereza, huku wakidai malipo ya fedha za kidijitali (Bitcoin) ili kuzifungua.
Wizi wa Crypto dhidi ya BItBy (2025): Kitengo 121 chini ya kikundi cha Lazarus Group walifanikiwa kushambulia na kuiba fedha zaidi ya billioni $1.5.

Leo hii kitengo cha 1212 cha wadukuzi wamefanya shambulio kubwa kuwa kutokea dunia la wizi wa fedha za kiditali yaani Crypto kwenye mtandao wa Binance lakini hii si mara ya kwanza kwa Binance kudukuliwa na kitengo 121

Haya ni mashambulio na wizi wa fedha za kimtandao yaliyowahi kuyakumba Binance kutoka kwa kikundi 121 cha wadukuzi wa serikali ya Korea Kaskazini:

Mei 2019 — Uvunjaji Mkuu wa Soko la Hisa ($41 milioni): Wadukuzi walitumia ulaghai, virusi vya kompyuta , na kuweza kuiba Bitcoin 7,000 ($41 milioni kwa wakati huo) moja kwa moja kutoka kwa pochi ya Binance katika muamala mmoja.

Oktoba 2022 — ($570 milioni): Wadukuzi walitumia udhaifu katika ulinzi wa Tokeni (Binance Smart Chain), huku wakighushi miamala na kuweza kutoa takriban tokeni milioni 2 senye thamani ya $570 milioni

Oktoba 2026 — ($6.3 bilioni):
Binance imekumbwa wizi mkubwa wa sarafu za kidikitali na kitengo cha 121 chini ya wadukuzi wanaotumia jina la mchezo wa Pokemone na kujiita TraderTraitor , wizi huu ni mkubwa zaidi kuwahi kutokea wa crypto katika historia baada ya washambuliaji kuweza kukwapua zaidi ya $6.3 bilioni

Lazarus Group - Kikundi kikubwa zaidi ndani ya Kitengo 121

Kwanini kimeitwa Lazarus?

Kikundi hiki kilipachickwa jina la Lazarus na wataalamu wa usalama wa kompyuta na mitandao kulingana na maandiko ya bibilia yanaelezea kisa cha kijana anaiwa Lazarus alieelezewa kama alikufa kwa siku kadhaa na kufufuka.
Hivyo wafuatiliaji hao wa usalama wa kompyuta na mitandao wanasema kikundi hiki kina tabia ya kupotea kabisa mpaka kudhani kumeshajifia ila kuja kuibuka na kufanya tukio kubwa la wizi wa mitandaoni mpaka kuiacha dunia nzima mdomo wazi.
Hiki ndio kikundi leo hii mnamo tarehe 30 oktoba 2026 kimeibuka kama TraderTraitor na kufanya shambulio kubwa la wizi wa sarafu za kidigitali kwenye mtandao wa Binance unakisiwa kuwa zaidi ya dola billioni 6.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…