Bureau de change haziwezi kufanya hivyo.
Labda tupate uelewa kidogo wa jinsi currency zinavyofanya kazi.
Ili kitu chochote kitumike kwa ajili ya kubadilishana thamani (yaani kama currency), nilazima kitu hicho kiwe na guarantee of value. Yaani ili mimi nikupe ndizi wewe unipe yale makaratasi, ni lazima kuwe na guarantee some where kwamba nikipeleka hayo makaratasi nitapata thamani inayokaribiana na thamani ya ndizi zangu. Without this guarantee no one would use the currency. Ndio maana gold inaweza kutumika kama currency. Haina explicit guarantee ya value, lakini mtu atakuwa tayari kubadilisha bidhaa yake na gold kama anaamini kwamba baadaye atarudisha thamani yake kwa kuibadilisha hiyo gold na kitu kingine chenye thamani sawa na hiyo. Na kuna maeneo kuna wakati hata chumvi imetumiaka kama currency, kwa sababu kwa wakati husika watu walikuwa wanaamini kwamba akibadilisha kitu na chumvi atarudhisha thamani yake baadaye.
Sasa currency za nchi hazina tofauti. Bila kuwa na guarantee of value, hakuna mtu angekubali kuzitumia. Sasa the question is: how is this value guaranteed? Ukielewa hilo itasaidia kuepuka asking the wrong questions.
Mimi ninaweza kuissue currency yangu nikaiita Manitoba Shilling (MNS). Ili wewe ukubali kuitumia kwenye biashara zako ni lazima nikuhakikishie kwamba ukipokea MNS na kuiweka nyumbani unaweza ukarudi kwangu siku yoyote na ntakurudishia thamani yako. Thamani ya 1 MNS ni kiasi gani? Mimi naweza kusema kila 1 MNS ntakupa kilo moja ya mahindi. Kwanini isiwe gram 1 ya gold? Well, ningeweza kuchagua hicho, ila lazima nichague kitu ambacho kila mtu atakuwa anaamini thamani yake haibadiliki over time (au haibadiliki-badiliki sana over time). Sasa watu watakubali kutumia MNS zangu ikiwa tu wanaamini thamani yake ni relatively stable, na kwamba ni convenient kuitumia kwa ajili ya kuhifadhia thamani.
Kwa kuwa nimeguarantee kwamba kwa kila MNS 1 nitatoa kilo moja ya mahindi, itanibidi kwa kila MSN 1 ninayo issue nihakikishe kuna kilo moja ya mahindi store kwangu ili jamaa akirudi nayo niwe na mahindi ya kumpa. Bila kufanya hivyo watu hawataamini kwamba nitaweza kuwarudishia 1kg ya mahindi kwa kila MSN 1 watakayorudisha, therefore thamani yake itaporomoka to 0 na hakuna atakayekuwa tayari kuitumia.
Kwa hiyo kama 1,000MSN zipo kwenye circulation, lazima niwe na 1,000Kg za mahindi store kwangu. Hizo 1,000Kg za mahindi ndiyo "guarantee of value" kwa hizo noti za MSN zilizoko kwenye mzunguko. Ghala langu la mahindi likiungua na watu wakajua, basi thamani ya MSN itashuka, na hakuna takayetaka kuitumia. Walionazo watakuwa wamefulia, kwa sababu siwezi tena ku-guarantee value ya MSN 1. (Ndicho kilichotokea Zimbabwe)
Hivyo ndivyo jinsi currency za nchi zilivyokuwa zinaendeshwa wakati flani, na gold imetumika sana ku-guarantee value ya currency. Kwa mfano nchi flani inaweza ikawa inatumia currency inayoitwa Manitoba. Ikisema Manitoba 1 ni sawa na gram 10 za gold, then watahakikisha kwa kila Manitoba moja wanayoingiza kwenye mzunguko, kuna gram 1 ya gold inayoingia kwenye reserve ya central bank yako. Na central bank itakuwa ina warehouses kwa ajili ya kuhifadhi gold hizo.
Kwa mfano huo, ili kuingiza noti zaidi kwenye mzunguko, inabidi wawe na uwezo wa kupata na khifadhi kiasi cha gold sawa sawa na thamani ya hiyo hizo pesa wanazoingiza kwenye mzunguko. Kwa jinsi hiyo thamani ya Manitoba haiwezi kushuka kwa sababu yoyote isipokuwa thamani ya gold kushuka.
Sasa imagine wewe ndio mkuu wa nchi hiyo ya kizamani. Na uongozi wako unataka kutengeneza pyramid flani lakini pesa iko tight. Unajua unahitaji Manitoba 10,000 kwa ajili ya hilo. Maana yake unahitaji gram 1,000 za gold ili iweze kuwapelekea central bank wakupe pesa hizi ukamilishe project. Lakini kama huna uwezo wa kupata hizo gold, unafanyaje? Unaweza ukaamua kuwalazimisha central bank watengeneze na wakupe hizo pesa. Kitakacotokea ni kwamba zitaingia Manitoba 10,000 kwenye mzunguko ambazo hazina backup, na hivyo in reality thamani ya Manitoba moja itakuwa imepungu na sio 10 gram za gold tena. Watu wasipojua poa, lakini wakija kujua, thamani ya Manitoba moja itapungua accordingly. Sikuhizi wanaita hii inflation.
Hicho ndicho moja ya vitu vilivyoangusha Roman Empire.
Sasa kabla ya miaka ya 1970s, nchi nyingi zilikuwa zime-guarantee currency zao kwa kutumia gold. Na maana yake ni kwamba kulikuwa na gold reserves mainteined kwa kila noti na sarafu iliyokuwa inatolewa.
Baadaye na mpaka sasa hiyo ikawa tofauti. Sasa swali ni je, nini kina-guarantee value ya USD au Tanzanian Shilling (TZS) siku hizi? Wengine wanasema exports na imports, wengine demand na supply, etc na wote wako sawa. Ila kwa maneno ya jumla zaidi ni kwamba uchumi wa nchi ndio una-act kama guarantee ya value ya currency ya nchi husika.
Chochote kingine utakachojaribu kufanya (kudhibiti nani anaweza kununuafedha za kigeni, etc) kunaweza kukaonekana kama kusaidia ku-stabilizie currency ya nchi. Lakini in the long run, haitasaidia kama uchumi wa nchi si mzuri.
Na kingine ni kwamba wakuu wanaweza kushawishika ku-print fedha ili kugharimia miradi ambayo fedha zake inakuwa ngumu kuzipata kutokana na mikopo au mapato. Sasa effect ya ku print fedha huku ni sawa na effec ya ku-issue Manitoba bila kuongeza size ya gold reserve. Zote zitasababisha thamai ya fedha husika kushuka. Mwingine atasema bei za vitu zimepanda, ambayo ni sawa. Lakini ukweli ni kwamba thamani ya fedha husika ndio imeshuka. Mtu akisema mahindi yamepanda bei, mimi ntamwambia shilingi imeshuka bei. Na wote tutakuwa sawa.
Kwa hayo pengine unaweza kuona kwamba, hata tuki-export vitu vichache, bado kuna uwezekano wa kuwa na currency ambayo inathamani. La sivyo ingebidi tuhitimishe kwamba nchi ambayo hai-export chochote basi fedha yake itakuwa haina thamani kabisa, kitu ambacho si kweli pengine.
Uchumi weto ukikomaa, uzalishaji ukaongezeka hata kama ni kwa ajili ya mahitaji ya ndani tu, ajira zikaongezeka, etc, hata kama exports hazitapanda kihivyo kuna uwezekano wa thamani ya shilingi kupanda.
Kwa maoni yangu, sababu kwa nini export na import zina-corelate na thamani ya shilingi ni kwa sababu mara nyingi uchumi ukikomaa hivyo, maana yake bidhaa zenu ni nyingi pengine zina ubora sana na kuna uwezekano zaidi wa watu wa nje kuzihitaji, na hivyo demand yake ya nje itaongezeka. Lakini hii demand ya nje sio lazima kiwe ndio kitu kilichosababisha thamani ya fedha hiyo kukua moja kwa moja. Of couse hiyo itakuwa tofauti kama nchi husika imekuza uchumiwake kwa kutumia exports (exports led growth).
Tukirudi kwa swala la Bureau De Change, wale jama ni wafanyabiashara, na wanafanya biashara ya fedha jinsi mtu mwingine anavyofanya biashara ya mahindi na maharage. Kwake yeye demand na supply ndio vinavyopanga bei. Akiuza ghali sana na asipopata mteja, atashusha bei. Akitaka kunua rahisi sana asipopata anayemuuzia, atapanda dau. Na kumbuka bei zao huwa zinakuwa guided na mi-market rate (bei ya kati ya mauzo na manunuzi ya fedha baina ya mabenk nadhani) ya bei za fedha ambazo wao Beureau De Change hawana influence nazo kabisa.
Mimi sio mchumi, kwa hiyo inawezekana nimefikiria upande kuhusu hili. Jisikie huru kukosoa.