Halafu kuna kitu kingine ambacho nadhani kinachangia kwenye inflation nchi hiii.
Sijui kama wengine msha-notice kwamba hii nchi kila mtu sasa anakuwa dalali, na anataka cha juu. Yaani hata ndugu yako ukimwambia tu unatafuta kitu, unaweza ukadhani anakusaidia kutafuta, kumbe na yeye anatafuta cha juu.
Na unakuta dalali mmoja anamwambia mwengine "ukileta mteja unakula pasenti yako". Na huyo anayeambiwa hivyo naye anamwambia mwingine hivyo hivyo. Sasa kitu cha sh 200 kikipita kwa madalali kadhaa unaweza ukajikuta unalipa zaidi ya mara mbili ya thamani yake.
Na pia madalali hawa wanasaidia sana kupandisha thamani ya kitu. Kumbuka wao wanalipwa kamisheni, kwa hiyo anavyouza kwa bei kubwa ndivyo kamisheni yake inakuwa kubwa, kwa hiyo ana kila insentive ya kuhakikisha bei iko juu.
Nadhani hii imechangia kwa kiasi flani ku-inflate bei za nyumba, viwanja, etc.
Hii hali kwa kweli mimi binafsi inanitisha. Labda wataalamu wa uchumi watatusaidia. Lakini ninaloliona wazi ni kwamba kunakuwa na kundi hili la watu ambao hawazalishi kitu lakini wanaishi, wakigharimiwa na wachache wanaozalisha. Sasa nguvu kazi ambayo ndiyo ingebidi iende kwenye "Kilimo Kwanza" ndiyo ambayo tayari ina shughuli nyingine inayolipa.
lol