Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 677
mie nnauliza ni sawa kujitokeza hadharani kwa sasa kama alivyofanya?, na huu mfuko wa amina mnauonaje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Baba mjinga sana huyu!!!
Hivi, si hawa hawa wanafamilia waliotuma barua Bungeni ati habari za kifo cha mtoto wao zisiandikwe magazetini, halafu wakati huo huo wanaenda maelezo kuelezea mambo ya ushirikina? Something is very wrong.... Angalia habari hizi ambazo zote ziko kwenye gazeti moja:
1. 2007-07-12 22:02:07 (Nipashe)
Na Mwanaidi Swedi, Dodoma
Familia ya aliyekuwa Mbunge wa Viti- Maalum kupitia Umoja wa Vijana wa CCM, Marehemu Amina Chifupa, imekuja juu ikitaka mpendwa wao asiendelee kuandikwa kwenye vyombo vya habari.
Katika kuhakikisha hilo linatekelezwa, familia hiyo imetuma ujumbe maalum Bungeni, uliosomwa na mmoja wa waheshimiwa wabunge.
Salam hizo za wana familia ziliwasilishwa Bungeni na Mbunge wa Mbinga Magharibi, CCM, Kapten (Mstaafu) John Komba.
Wakati anatoa salam hizo ilikuwa jana yapata saa moja hivi usiku.
Kapteni Komba alifikisha ujumbe huo wakati alipopewa nafasi ya kutoa mchango wake kwenye bajeti ya Wizara ya Miundombinu.
Akasema kuendelea kuamuandika Marehemu Amina Chifupa wakati akiwa tayari ameshatangulia mbele ya haki, ni sawa na kuwakumbusha machungu ndugu na jamaa zake.
Mheshimiwa Amina Chifupa alifariki Juni 26 mwaka huu katika hospitali ya Jeshi Lugalo ambako alilazwa tangu Juni 8 mwaka huu.
Halafu siku moja baadaye,
2007-07-13 10:44:20
Na Lucy Lyatuu
Mzazi wa aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana (CCM), Marehemu Amina Chifupa, ameishauri serikali kuwataja viongozi wanaoshiriki katika sakata la dawa za kulevya ikiwa ni njia mojawapo ya kumuenzi mtoto wao.
Baba wa Amina, Bw. Khamis Chifupa alitoa rai hiyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam jana.
Alikuwa akitoa shukrani zake kwa watu walioshiriki kwa njia moja au nyingine kufanikisha msiba wa mtoto wake.
Mapema kabla ya kuanza mkutano huo, waandishi wa habari walisimama kwa dakika moja na kusali na kutoa heshima kwa marehemu ambaye kitaaluma alikuwa mwandishi wa habari na mtangazaji wa radio.
Alisema familia yake iko tayari kusikia taarifa zozote zinazohusiana na viongozi wanaojihusisha kwa njia moja au nyingine katika sakata la dawa za kulevya na akaiomba serikali kutokuwa na kigugumizi kuwataja wahusika bila kujali nyadhifa zao kisiasa au kijamii.
Hata hivyo, aliishukuru serikali kwa mchango wake ilioutoa katika kipindi chote cha majonzi.
``Tunamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete kwa mchango wake alioutoa ikiwa ni pamoja na kutoa ndege yake kwa ajili ya kusafirisha mwili wa marehemu hadi kijijini Ihanjo wilayani Njombe. Hatuna cha kuwalipa ila tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu,`` alisema Bw. Chifupa.
Alisema familia yake haiwezi kusema serikali ichunguze kifo hicho ila kama kuna mtu mwenye taarifa au anayejua mazingira ya kifo hicho anaweza kutoa taarifa kwa serikali ili wanaohusika wachukuliwe hatua.
``Ninatoa kauli hii kwa kuwa wapo wanaosema kifo cha Amina kinahusishwa na kupewa sumu, wengine uchawi kutokana na kupiga vita dawa za kulevya, jambo ambalo hatuna uhakika nalo,`` alisema.
Hata hivyo, alisema katika kumuenzi mtoto wake, familia itaendeleza mfuko wa Amina Foundation na kuwataka watu wote waliokuwa na mapenzi mema na Amina kuuchangia ili uweze kutekeleza ahadi zote alizokuwa amewaahidi.
``Amina Foundation itaongozwa na mjomba wake, Bw. Solomon Mmbanga, akishirikiana na wajumbe wengine kutoka Bungeni na kamati iliyokuwa ikiandaa msiba wake.
Bw. Chifupa alisema yeyote anayetaka kuuchangia mfuko huo atumie akaunti iliyoko katika tawi la CRDB Kijitonyama yenye namba 01J1014153400.
Alisema marehemu Amina alianza kuumwa Mei 8 mwaka huu mara baada ya kwenda nyumbani kwake akitokea kwa aliyekuwa mume wake, Bw. Mohamed Mpakanjia.
Aliongeza kuwa mwanae aliugua maradhi ya ajabu ambapo alikuwa akitaja baadhi ya viongozi kuwa ndio waliomsababishia tatizo la kuugua.
Hata hivyo, kwa kipindi chote Amina alikuwa hali chakula chochote ndipo tulipojua kuwa yalikuwa mambo ya Kiswahili hivyo ikabidi kumhudumia Kiswahili.
Bw. Chifupa alisema baada ya kumpeleka hospitali kuu ya Jeshi ya Lugalo aligundulika kuwa na ugonjwa wa kisukari kilichofikia 400 kikichanganyikana na homa, ambavyo vyote kwa pamoja vilikuwa havishuki.
``Akiwa hospitalini Amina alizungumza maneno mengi (hakuyataja) ya ajabu na mazito mengine yakiashiria kifo chake,`` alisema.
Katika hatua nyingine, Bw. Chifupa alimetoa ruksa kwa wote wanaoendelea kumuandika mtoto wake lakini waandike yaliyo ya kweli peke yake.
Marehemu Amina alikufa Juni 26, mwaka huu saa 8:45 usiku akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na kuzikwa kijijini Ihanjo wilaya ya Njombe mkoa wa Iringa.
Baba mjinga sana huyu!!!
.... (Mzee Chifupa)...Akasema mwanae aliugua maradhi ya ajabu ambapo alikuwa akitaja majina ya baadhi ya viongozi kuwa ndio waliomsababishia tatizo la kuugua. [*]SOURCE: Alasiri[/LIST]
Ugonjwa huu mpya ambao aliugua Bi. Chifupa na uliosababisha mauti yake kwa jina la kitaalamu hujulikana kama Uumbuajiasis Viongozitanzanialitis Hadharanum. Ugonjwa huu unatokana na kufuatilia mambo ya serikali na viongozi kwa karibu kiasi cha kutaka kuweka ubovu wao hadharani. Dalili kubwa za ugonjwa huu ni hizi:
a. Kupenda nchi zaidi kuliko chama
b. Kuwa tayari kutetea mali ya Taifa na kuilinda mali hiyo
c. Kutoogopa yatakayokukuta
d. Kuanza kuweka hadharani ubovu na siri za viongozi hasa kwa jamaa yako karibu
e. Kutosikiliza ushauri wa kutakiwa kukaa kimya na wakubwa wako
f. Kuwa kimbelembele kuzungumza na kukemea maovu kila upatapo nafasi
g. Kuwa mtetezi wa Katiba na mkosoaji wa jamii
h. Kutolegeza msimamo hadi kifo.
Maambukizi
Ugonjwa huu unaambukiza watu wachache kwani watu wengi wameshapatiwa kinga yake. Kwa wale wanaombukizwa wanafanya hivyo zaidi kwa kusoma habari za ufisadi, rushwa, na ubadhirifu katika serikali yao. Kwa kupitia mitandao, vitabu, na vyombo vya habari virusi vya ugonjwa huu vinajipenyeza katika akili za watu na kusababisha kusisimka kwa ubongo. Wale waliombukizwa ugonjwa huu hujikuta wakitafuta habari za kila namna na kushiriki mijadala yenye kutafakari mustakabali wa Taifa lao.
Kinga:
Ugonjwa huu kinga yake kubwa hujulikana kwa kitaalamu kama Mrungura. Kinga hii hutolewa kwa wale wote wenye kuanza kuonesha dalili za kukumbwa na ugonjwa huu. Kinga hii huwekwa kwenye mabenki na maofisi mbalimbali ili kuzuia viongozi wakubwa wasipatwe na virusi vya ugonjwa huu. Kinga hii pia hufanya kazi kwa wale walioanza kuonesha dalili kama kina Phillip Marmo, Chrisant Mzindakaya n.k Pindi mtu akishapatiwa kinga hii HAWEZI kuipinga serikali!
Tiba:
Hadi hivi sasa ugonjwa huu hauna tiba ya uhakika kwani wale ambao wameshaugua kwa muda mrefu hawako tayari kutibiwa kwani wanaona wanaishi vizuri tu na ugonjwa huu.
Karantini
Pindi baadhi ya wakubwa wakiona kuna mtu ambaye amefikia hatua ya juu kabisa ya ugonjwa huu basi kwa mbinu wanazozijua wenyewe wanamkarantini, na wakati mwingine anakuwa katika hali hiyo ya kutengwa hadi kifo ili asiendelee kuwaambukiza watu wengine.
Jihadhari
Kwa vile ugonjwa huu ni wa hatari, watu wabadhirifu, wezi wa mali ya umma, walaghai, na mafisadi hawawezi kuustahimili. Ugonjwa huu ni kinyume kabisa na watu hawa hivyo kama hutaki kuambuzizwa hakikisha unaendelea kujikita katika katika vitendo viovu vya kuharibu mali za umma na kuivunja vunja nchi huku ukishiriki katika kumegeana hadhina ya Taifa. Kwa vile ugonjwa huu unaendelea kuambukiza taratibu, kuna kila dalili hapo ulipo UNAISHI NA MWATHIRIKA!
Wakati magazeti ya Shigongo yamemwandama kumchafulia jina, jamii ilikaa kimya. Amina akawa analia wakati akiwa chumba cha habari cha Clouds, watu wanasema shangingi huyo. Leo ni wale wale wanaomsifu na kumwagia sifa. Napenda kumaliza kwa kusema Amina hajafa. Waliokufa ni sisi tunaodhani tuko hai. Sisi wanafiki wa kupeleka maua kwenye majeneza wakati tungeweza kutoa maua hayo kukamilisha azma yake ya masha.
muhingo