TANZIA Buriani Dunstan Charles Rally Navigator mkongwe

TANZIA Buriani Dunstan Charles Rally Navigator mkongwe

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Buriani brother.
Jana tumekutana Msasani Flats tukipanga mipango mingi na mipangilio kuhusu safari ya leo kwenda kwenye mashindano ya mbio za magari Sao Hill Iringa zinazo dhaminiwa na CMC Automobiles.

Ulitamani sana uingie kwenye michuano hii ukiwa na gari yako, lakini ilikuwa na changamoto ya suspensions. Suspensions za rally moja inagharimu million 5 na zaidi, sijui kwa nini nilikuwa nachelewa kukutengenezea gari yako.

Leo Jemima Mrembo ananipigia simu asubuhi hii kwamba umepatwa na umauti jana usiku ukiwa maeneo jirani na nyumbani kwako Tegeta.

Naambiwa chanzo cha umauti wako ni High Blood Pressure. Imekuchukua ndani ya dakika chache ukiwa na mdogo wako King.

Bro, umeniachia msiba mkubwa sana, nina deni kwako. Sijui hata gari yako iko garage gani, niitengeneze tu, niipaki nyumbani kwako.

Mungu akufanyie wepesi, akulaze na kukupumzisha kwa amani.

Tulipanga twende wote Iringa kwenye mbio, mmoja atwaliwa mwingine aachwa, sijafanya lolote la kumfurahisha Mungu, pumzi ninayoivuta ni kwa neema yake tu.

Mungu aitunze roho yako nzuri mahali pema sana.
 
Back
Top Bottom