Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KOKNI MUSLIM JAMAAT of DAR ES SALAAM, TANZANIA
DEATH ANNOUNCEMENT
إِنَّا للهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعون
"Surely we belong to Allah and to Him shall we return".
It is with sadness that we share the news of the demise of MR MOHAMEDRAFIQ ZAHIR FAKI who passed away in Dar Es Salaam on 9th SEPTEMBER 2024, MONDAY
Marhum was the Husband of Mumtaz Mula.
Marhum was the Father of Zarin,Tariq,Shahbaaz and Simeen Faki.
Marhum will be burried on :
Date : 9th SEPTEMBER 2024
Time : After Zohr Prayers (1pm)
JANAZA NAMAZ : KITUMBINI MOSQUE
BURIAL : KMJ GRAVEYARD,KIJITONYAMA.
May Allah (SWT) bless the departed soul with a place amongst His chosen ones and grant the family patience to bear this loss - Ameen.
Kabrastan Committee
BURIANI MWANA- SAIGON ASILI RAFIQ
=====
Tangazo hapo juu ni la kifo cha Rafiq kijana wa Kihindi tuliyekuwa tukichezanae mpira Everton hadi Saigon udogoni katika miaka ya 1966 na tukawanae Saigon 1967.
Wazee wake ndiyo waliokuwa wakiendesha Khalid Restaurant kwa miaka mingi sana sisi tunazaliwa tumeikuta hapo Uhindini pembeni mwa mshonaji bingwa wa nguo wa enzi zetu Louis.
Wazee wake walihusika na Msikiti wa Kitumbini na Rafiq alikuwa akisali hapo sala zake zote.
Everton/Saigon nathubutu kusema ndiyo club pekee Kariakoo katika kumbukumbu yangu ambayo kulikuwa na vijana wachezaji mpira wa Kihindi - Rafiq na Bulji.
Bulji aliondoka Dar-es-Salaam na kuhamia Mtwara na akacheza Taifa Cup timu ya Mtwara akiwa mshambuliaji.
Wengi tunamkubuka Bulji kwa kile kipaji chake cha mpira.
Wale waliokuwa Saigon miaka ya mwanzoni watamkumbuka Rafiq kwa mkono wake wa kutoa.
Siku zote Rafiq tukiwa na michango ya club ya kununua mipira au jezi mchango wake ulikuwa mkubwa.
Rafiq alikuwa mtu wangu ukubwani tukionana na kusalimiana tukikutana hapo hotelini kwao au msikitini Kitumbini.
Lakini wengi waliokuwa wakimfahamu Rafiq walisikitishwa na hali iliyomtokea ghafla akawa mtu mkimya na hazungumzi na yeyote na hata ukimsalimia kwa bashasha atakuitikia na kukupita kama vile hamkupata kujuana na kucheza pamoja utotoni.
Hii ilikuwa awe pale hotelini au msikitini.
Wengi tukatambua ndugu yetu kapata maradhi.
Muda wote alijitenga akiwa amekaa pembeni peke yake kimya na muda wote ana tasbihi mkononi.
Mimi iliponidhihirikia hali ile yake ikawa tukikutana nampungia na yeye atanipungia na tunapishana kimya.
Wengi waliokuwa wanamfahamu Rafiq walikuwa wakifanya hivyo.
Hii ilitutosha.
Allah amfanyie wepesi ndugu yetu.