Buriani rafiki yangu wa udogoni, Ibrahim Mussa Panzi

Buriani rafiki yangu wa udogoni, Ibrahim Mussa Panzi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
BURIANI RAFIKI YANGU WA UDOGONI IBRAHIM MUSSA PAZI

Nimesoma taarifa ya kifo cha Ibrahim Mussa Pazi nikiwa katikati ya Bahari ya Hindi nikitokea Zanzibar kurejea Dar es Salaam.

Ibrahim tumekuwa sote udogoni tukicheza mpira Saigon.

Huu ni mwaka wa 1966 umri wetu haujapita Miaka 15.

Leo nimesimama nje ya nyumba yao Mtaa wa Mafia na Nyamwezi mbele inapita Barabara ya Msimbazi.

Nyumba ya bibi yangu Asha bint Farijallah ilikuwa hapa lakini ilivunjwa ili kupisha upanuzi wa Barabara ya Msimbazi.

Kipande hicho kati ya Nyamwezi na Msimbazi kina historia inayoieleza Dar es Salaam na Kariakoo.

Hapo kuna nyumba tatu maarufu.

Kwanza nyumba ya Mzee Mussa Pazi, nyumba ya Sheikh Hussein Juma na nyumba nyingine ambayo akiishi Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir.

Hii nyumba ya akina Ibrahim yaani nyumba ya baba yake Mzee Mussa bin Pazi ndipo ilipopigwa picha maarufu ya Baraza la Wazee wa TANU mwaka wa 1957.

Mtaa huo kulikuwa na darsa kubwa sana.

Baada ya Sala ya Alfajir Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa akisomesha barabarani yametandikwa majamvi.

Mtaa mzima ulikuwa unafungwa kipande hicho.

Hapo katika Mtaa huu wa Mafia kulikuwa na nyumba ya bibi yangu Asha bint Farjallah.

Mwanamke wa Kiswahili aliyekuwa na gari yake Peugeot 304 na ameajiri dereva wa kumwendesha.

Jambo geni miaka ile kwa mwanamke wa Kiafrika.

Nimesimama mazikoni nje ya nyumba ya rafiki yangu Ibrahim nimerudi udogo tuko sote Mnazi Mmoja napokea pasi kutoka kwake na mimi nampelekea pasi.

Jirani na nyumba ya rafiki yangu huyu alikuwa rafiki yetu na yeye akija kucheza mpira Saigon Mnazi Mmoja jina lake Moshi, mtoto wa Moshi Msosi.

Moshi Msosi alikuwa mtu maarufu sana Dar es Salaam ya miaka ile.

Naiangalia nyumba ya akina Moshi.
Nyumba ile kona ya Mafia na Nyamwezi haipo.

Kuna gorofa ndefu badala yake.
Kote pale ni magorofa matupu.

Moshi alifariki Ulaya akiwa mdogo sana alipokwenda kutafuta maisha kama baharia.

Sidhani kama Moshi alifikisha hata miaka 20.
Umma uliofika mazikoni ni mkubwa sana wake kwa waume.

Watu wanasema umevunja rekodi ya baba yake Mzee Mussa Pazi.
Huu ni ukoo maarufu Dar es Salaam enzi na enzi.

Ukoo wa akina Tambaza.

Walikuwa wakiishi Upanga miaka hata Wajerumani hawajaingia pande hizi na kuzipa jina German Ostafrika.

Upanga yote ni mali yao na Ikulu imejengwa katika ardhi yao na yapo humo ndani makaburi yao hadi leo na makaburi haya mengine yamo ndani ya Wizara ya Ardhi.

Wao ndiyo waliotoa kiwanja chao kilichokuwa na makaburi yao ujengwe Masjid Maamur, Upanga.

Hawa waliishi Kisutu kisha Kariakoo hii tunayoijua hivi sasa.

Hawa ndiyo walijenga Msikiti wa Kisutu unaofahamiaka kama Msikiti wa Mwinyikheri Akida ambao uko hadi leo.

Hawa ndiyo waliompokea Julius Nyerere na ndiyo waliyoimarisha chama cha TANU Dar es Salaam hadi uhuru ukapatikana mwaka wa 1961.

Sheikh Haydar Mwinyimvua anatokana na hawa.

Nyumba ya Haydar Mwinyimvua ilikuwa imepeana mgongo na ofisi ya TANU.

Ilikuwa TANU wakiwa na mikutano ya siri mama yake Haydar Mwinyimvua Bi Mwamtoro bint Chuma alivunja ua wa nyumba yake kuunganisha na ua wa TANU.

Hawa ndiyo waliofungua moja ya matawi ya TANU yenye nguvu Tanganyika nzima tawi la Mtaa wa Mvita.

Watu hawa ni maarufu sana Dar es Salaam.
Nimesimama pembeni mtu tu lakini sipo pale.

Nimeelemewa na mawazo.

Nimesimama katikati ya nyumba mbili za marafiki zangu wa udogoni Ibrahim na Moshi na sasa akili yangu inaniungaisha na wengi wenzangu waliotangulia mbele ya haki wengine nyumba zao zilikuwa hapo jirani na nyumba ya akina Ibrahim.

Nyumba zile hazipo tena.
Magorofa kila pembe kila kona.

Kila nilikotupa jicho ni magorofa matupu.

Nyumba ya akina Ishaka Marande na dada yake Mgeni siioni ni kuvuka Msimbazi tu nyumba yao ilikuwa pembeni ya Barabara ya Msimbazi.

Nashusha pumzi.

Haukupita muda jamaa zangu wamenizunguka na wamekuja na kijana mmoja sheikh anaendesha kipindi cha On Line TV.

''Unataka historia ya Saigon huyu atakueleza kila kitu.''

Nimezinduka.

Muharam Mkamba mjukuu wa Sheikh Idrissa bin Saad huyo anamweleza yule sheikh kijana.

Muaharam ni mtu wa mshakara sana anaendelea, ''Huyu alikuwa akivaa bukta yake mpirani lazima aibenjue huku na huku.''

Muharam kanirejsha kwenye ile hadhira niko tena mazikoni.

Nimeshatoka mwaka wa 1966 Mnazi Mmoja na Saigon niko mazikoni.

Jeneza linatoka linabebwa kuelekea Msikiti wa Makonde kusaliwa Sala ya Jeneza.

Jirani sana ya msikiti ndiko alipokulia Mwana Saigon mwenzetu Ahmada Digila tukimwita, ''Danny Blanchflower.''

Hili ndilo lilikuwa jina lake la mpira.
Danny Blanchflower alikuwa mchezaji wa Uingereza.

Ahmada na yeye aliiaga dunia katika umri mdogo sana.

Naam rafiki yangu Ibrahim ametangulia.

Allah amfanyie safari yake iwe nyepesi na amsamehe dhambi zake na amtie peponi.

Amin.

Screenshot_20220622-050108_WhatsApp.jpg
 
Poleni mno kwa msiba huu, hii ni history ya nchi yetu ambayo wengi hatukuifahamu,kudos kwa mtoa mada na historia ya nchi yetu kuna umuhimu wa kuiandika upya ili ukweli wa yaliyotokea yajulikane
 
Kweli umekumbuka mbali sana Mzee M.Said, unatamani miaka irudi nyuma ujikute unaishi yale maisha ya zamani ukiwa na marafiki zako.

Poleni sana.
 
Kweli umekumbuka mbali sana Mzee M.Said, unatamani miaka irudi nyuma ujikute unaishi yale maisha ya zamani ukiwa na marafiki zako.

Poleni sana.
7seven,
Unajua wenzangu wengi wametangulia.
Nawakumbuka sana na nazisikia hadi sauti zao.

Dar es Salaam ile ilikuwa sote tukijuana na tulikuwa na mapenzi ya ajabu baina yetu.

1660078897243.jpeg
 
7seven,
Unajua wenzangu wengi wametangulia.
Nawakumbuka sana na nazisikia hadi sauti zao.

Dar es Salaam ile ilikuwa sote tukijuana na tulikuwa na mapenzi ya ajabu baina yetu.

View attachment 2319587
Ni kweli mlikuwa na mapenzi yasiyo na unafiki ndio maana mpaka leo hii unawakumbuka marafiki zako kwasababu mlitendeana wema.

Nabarikiwa na makala zako za historia mambo mengi nilikuwa siyajui huwa napata maarifa kutoka kwako.

Ahsante sana Mzee wangu.
 
Ni kweli mlikuwa na mapenzi yasiyo na unafiki ndio maana mpaka leo hii unawakumbuka marafiki zako kwasababu mlitendeana wema.

Nabarikiwa na makala zako za historia mambo mengi nilikuwa siyajui huwa napata maarifa kutoka kwako.

Ahsante sana Mzee wangu.
7seven,
Ahsante sana.
 
Back
Top Bottom