Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BURIANI RASHID "INZI" TIMAMY MWANASOKA WA SIFA
Imekuwa kawaida yetu kuwa hatuna historia yetu yoyote iliyohifadhiwa rasmi.
Kama si kwa hii video ya marehemu Abdulkarim Shah maarufu kwa jina la Bulji ambae alipata kuwa mbunge wa Mafia leo tusingekuwa na kitu cha kuweka hapa kueleza historia ya Rashid Inzi mchezaji mpira maarufu wa Southern Province enzi za Sunlight Cup kisha Dar-es-Salaam Young Africans na Hydra Club timu ya muajiri wake East African Cargo Handling Services.
Rashid Inzi baada ya kucheza Sunlight Cup ambayo yalikuwa mashindano makubwa yaliyokutanisha majimbo yote ya Tanganyika akiwakilisha Southern Privince, Rashis Inzi alikuja Dar es Salaam kuchezea Young Africans mwaka wa 1959.
Rashid Inzi alicheza Yanga hadi mwaka wa 1964.
Hili jina la "Inzi" alipewa kwa ajili ya ujanja wake wa kuwatoka walinzi na kufunga magoli pale walinzi walipokuwa wanadhani wameshamtia mkononi.
Rashid Inzi alikuwa na umbo dogo lililomvutia mlinzi kuwa mshambuliaji anaemkabili hatafua.dafu.
Kumbe hilo umbo dogo ndiyo ilikuwa silaha yake kubwa ya kuiangamiza safu ya walinzi.
Rashid Inzi alikuwa mwepesi wa kuruka na mpira kutoka mbio mbele na kupokea pasi kugeuka na kupiga mashuti.
Rashid Inzi nimemfahamu kwa karibu sana nilipoingia bandarini lakini wakati huo alikuwa ameshastaafu kucheza mpira lakini hukuacha kuhudhuria mazoezi ya Hydra Jangwani akicheza pamoja na wachezaji waliokuwapo katika timu zilizokuwa kwenye ligi.
Ilikuwa wakati mwingine tabu kumtofautisha kaka Rashid Inzi na wachezaji vijana waliokuwa wananyanyukia kama Adam Juma, Boi Wickens, Silvernus Aoko, Jamil Hizam, (Denis Law), Makanda Tambaza (Norman Hines), Harubu "Nge" kwa kuwataja wachache na kulikuwa na wachezaji wakongwe kama Said Walala, Abdulrahman Lukongo, Emmanuel Albert Mbele, Arthur Mambeta na wengineo.
Wengi wao hawa wametangulia mbele ya haki.
Timu ya Hydra ilikuwa na mchanganyiko maalum wa mastaa kutoka Cosmopolitan, Yanga na Sunderland (Simba).
Katika mkusanyiko huu kaka Inzi alitokeza dhahir kwa ile staili yake ya uchezaji.
Mwaka wa 2013 nilikwenda Kilwa nikiwa katika timu ya watafiti wanne wa Hijja (Haj Research Project) iliyokuwa ikiongozwa na Dr. Issa Ziddy wa State University of Zanzibar akiwakilisha King Abdulaziz University ya Saudia.
Rashid Inzi alikuwa kastaafu miaka mingi yuko Kilwa.
Nilimpigia simu kumtaarifu kuwa nakuja Kilwa na wenzangu katika utafiti na tutahitaji msaada wake.
Ilikuwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kaka Inzi alifurahi sana kwani ilikuwa kipindi kirefu hatujaonana.
Mimi na wenzangu alitutafutia nyumba ya kulala wageni jirani na nyumbani kwake na akatuelekeza wapi tutapata chombo cha kutufikisha Kilwa Kisiwani ambako ndiko utafiti wetu ulipoanzia.
Jina lake lilitosha kutufungulia milango mingi na tuliporudi Masoko yeye mwenyewe akatupitisha kwa watu wote muhimu.
Jioni alituaandalia futari nyumbani kwake ambako tulikutana na mkewe mama yetu ambae alikuwa na madrasa kubwa yeye mwenyewe mama yetu akisomesha watoto wadogo.
Kiasi cha kama majuma matatu hivi alipokuwa Dar-es-Salaam nilipata taarifa kuwa yupo mjini kwa matibabu.
Nilimpigia simu na tukazungumza kiasi wala haikunipitikia kuwa alikuwa mgonjwa sana kwani uchangamfu na vichekesho vyake vilikuwa pale pale.
Juma lililopita nilipanga na Ramadhani Madabida ambae yeye ni mjomba wake twende Jumamosi tukamuone.
Siku hiyo ya Jumamosi ndipo nilipoletewa taarifa kuwa kaka yangu Inzi amefariki dunia na maziko yatakuwa siku hiyo hiyo Kilwa.
Buriani kaka yangu Rashid Inzi.
Allah amsamehe makosa yake na amweke mahali pema peponi.