Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
BURIANI SALUM ZAHORO
Makala hiyo hapo chini niliandika miezi miwili iliyopita.
Naiweka tena tuisome kama kumbukumbu ya Salum Zahoro aliyefariki jana na kuzikwa jana hiyo hiyo:
SALUM ZAHORO MWIMBAJI WA "TANGANYIKA NA UHURU" 1961 NI MGONJWA SANA ANAHITAJI MSAADA
Tarehe 9 Desemba TBC walirusha kipindi cha kumbukumubu ya uhuru kipindi kikijikita zaidi katika mchango wa watu walioishi Magomeni ya miaka ya 1950.
Niliwashauri TBC kutumia nyimbo ya Salum Zahoro na Kiko Kids, ''Tanganyika na Uhuru,'' katika kipindi chao na kwa hakika hili walilipenda sana na wakaipiga nyimbo hii wakati wa kumaliza kipindi.
Nimeweka clip fupi ya mwisho wa kipindi Salum Zahoro akiimba nyimbo hii.
Umri wa nyimbo hii ni sawasawa na umri wa miaka 59 kipindi cha uhuru wa Tanganyika.
Salum Zahoro aliimba nyimbo hiyo akiwa kijana labda wa miaka 20 akiwa kiongozi wa Kiko Kids Tabora.
Katika nyimbo hii utamsikia Salum Zahoro akiwataja viongozi wa Serikali ya Uhuru - Julius Nyerere, Abdallah Fundikira, Nsilo Swai, Tewa Said Tewa, Kawawa na wengineo.
Picha hii pamoja na nyimbo hiyo kaniletea Hamisi Delgado kutoka Ujerumani ambae ni mzaliwa wa Tabora na akimjua Salum Zahoro toka yeye bado kijana mdogo.
Nilimfahamisha Delgado maradhi ya Mzee Salum Zahoro alipokuja likizo na siku ya pili tu alikwenda kumjulia hali nyumbani kwake ambako alifahamishwa kuwa Mzee Salum Zahoro amelazwa Hospitali ya Amana.
Delgado alikwenda kumuona hospitali.
Inatia simanzi na kusikitisha kuwa wazalendo wetu waliojenga taifa hili hatuwathamini. Hapa sitasema mengi kwani tatizo hili kwa sasa ni maarufu hakuna asiyelijua.
Miezi michache iliyopita nilipokea simu usiku kutoka kwa Juma Mwapachu akaniambia kuwa yuko na Mzee Steven Hiza aliyetunga nyimbo, ''Tanzania Yetu ni Nchi ya Furaha,'' akiwa na Atomic Jazz Band ya Tanga.
Juma Mwapachu akanieleza masikitiko yake kwa hali ambayo amemkutanayo Mzee Hiza wakati nyimbo hii yake ndiyo imekuwa kama utambulisho wa taifa letu ukipigwa na steshini zote za radio na televisheni.
Aliniuliza nini tufanye ili Mzee Hiza na wanamuziki wetu walioitumikia nchi hii angalau waonje faida ya jasho lao lau kama tumechelewa.
Hii ndiyo hali ya mashujaa wetu waliohamasisha Watanzania katika kujenga taifa hili na kuleta maendeleo.
Picha ya Mzee Salum Zahoro akiwa amelazwa hospitali.
https://youtu.be/kb7etyo820c