Buriani Salum Zahoro

Buriani Salum Zahoro

Siyo swala la kiswahili cha bara wala cha Dar es salaamu au cha Mombasa au cha Tanga au cha Zanzibar, bali tunaongelea kiswahili kufuatana na isimu ya lugha yenyewe kama inavyotambulika na BAKITA. Kiswahili cha makabila mbalimbali kinaweza kuwa kinachanganya na lugha zao za asili lakini kiswahili cha BAKITA ni hicho tunachokuambia, inawezekana na wewe unaongea kiswahili cha kabila lako kwa hiyo hufuati isimu ya kiswahili bila kujielewa. Nimeishi na wamarekani wengi ambao hawana lugha nyingine bali ni kiingereza tu lakini wanaongea kiingereza broken sana, kwa mfano anaweza kupinga jambo kwa kusema "I don't know nothing!" Kwa hiyo na wewe inawezekana umeazaliwa na kukulia dar es Salaam na unajua kiswahili tu, lakini ni hicho kiswahi cha "I don't know nothing"

Kubali tu mzee mwenzangu kuwa inawezeka umekulia katika kiswahili kisichofuata isimu ya kiswahili na hilo lisiwe tatizo la kukufanya upinge kuwa wanonyoosha kiswahili chako ni watu wa bara tu wasiojua kiswahili ilihali hata wataalamu akina Sheikh Kilemile waliwahi kuliweka hilo bayana.
Kichuguu,
Sijui kwa nini unataabishwa na lugha yangu.

Hiyo BAKITA iangalie kama ina Waswahili wenyewe.

Mimi ni Mswahili na sijapata kuzungumza lugha nyingine toka nizaliwe ila Kiswahili.

Hiyo BAKITA ndiyo hawa wa "mapungufu" na "masaa."
 
Back
Top Bottom