BURIANI Sultan Jamshid BIN Abdulla BIN Khalifa (1926 - 2024)

Pascal Mayalla
 
Mzee@Mohamed Said,niliwahi kuzungumza na Mzee mmoja Mzanzibari Chotara kuhusu Mapinduzi na utawala wa kisultan maana alikuwepo.
Alichoniambia,ni kwamba Waarabu waliishi kwa Amani na Wazawa ijapokuwa waliishi madaraja tofauti.
Waarabu walikuwa Raia wa Daraja la Juu na Wazawa wakiwa Raia wa Daraja la chini.
Na ubaguzi ulikuwepo.
Lakini alilalamikia Mapinduzi,kuwa Wazawa walimwaga Damu nyingi ya Waarabu mpaka kupelekea wengine kukimbia na manusura waliobakia ndio watu kama wao ambao Waarabu walizaa na wanawake wa kiswahili.
Kwa kifupi;
kwa mtazamo wangu Mapinduzi yalikuwa Muhimu ili kuondokana na Unyonyaji wa Waarabu na tabia zao za ukabaila za kukodisha ardhi kwa Wazawa wenye ardhi Yao na kuwatoza Kodi.
Pia kukomesha madaraja baina ya Waarabu na watu weusi.
Inasikitisha kiwango cha umwagaji damu uliotokea lakini lazima tukubaliane kwamba silaha zilitumika na pande zote Mbili,Wazawa wangezembea wao ndio wangekufa wengi.
Nayasifu MAPINDUZI maana sultan hakuwa na Haki ya kutawala na alikuwa mvamizi.
Ukiwavamia watu na ukawatawala kimabavu ni lazima siku Moja watakutoa tu,kama alivyotolewa sultan.
Labda Jemshid alikuwa mtu mzuri lakini historia ya watawala waliopita ilimponza,manyanyaso na ubaguzi vina tabia ya kuchosha watawaliwa.
Tabia hiyo ya Ubaguzi imeota mizizi mpaka Leo Zanzibar,Muunguja anambagua mpemba,Wazanzibar wanatubagua Wabara na kutuita majina ya kutweza,watu wengi wenye asili ya kiarabu na ngozi nyeupe nao huwaona watu weusi kama wewe kuwa si kitu.
Yote kwa yote,ni historia tu na inabidi tujifunze na tujirekebishe kwayo.
MAPINDUZI DAIMA.
Wasalaam.
 
Abdulatif...
Kwanza muhimu uelewe hakuna Mzanzibari Chotara wala Mzanzibari Mweusi.

Wazanzibari hawajapata kujinasibu kwa hivyo.

Hili la rangi na matabaka lilikuwapo enzi za Sultan kama lilivyo duniani kote na lipo hadi leo Tanzania.

Ukileta suala la uzawa Zanzibar utapata shida kubwa kupita kiasi kwani utawakuta Waafrika koo zao haziendi nyuma hata kizazi kimoja na utawakuta wengine wana damu ya Kiomani na Kimanyema wanakwenda nyuma vizazi hadi saba na pengine zaidi.

Sultani hakuvamia Zanzibar aliombwa na Wazanzibari wenyewe kuja Zanzibar kuwaondoa Wareno walioivamia Zanzibar wakaikalia kwa nguvu na kuupiga vita Uislam.
 
Kwa ufupi serikali ya Shamte na utawala wa Jamshid ulipinduliwa na mamluki kutoka Tanganyika na sio wazanzibari ?
 
Ahsante kwa kunielimisha zaidi,Sina ninalojua zaidi yako Mzee wangu.
Huu ni mtazamo wangu tu kutokana na uzoefu wangu wa Maisha ya visiwani pamoja na story za wazee huko kwenye maskani zao.
 
Kwan serikali ipi ilipinduliwa Zanzibar?
 
Nini maana ya uvamizi na nin maana ya mapinduzi?

Tuanzie hapa kwnz
 
Kwa ufupi serikali ya Shamte na utawala wa Jamshid ulipinduliwa na mamluki kutoka Tanganyika na sio wazanzibari ?
Proved,
Uongozi wa ASP ulishirikiana serikali ya Tanganyika kufanikisha Mapinduzi.

Halikadhalika Makomredi yaani Umma Party walitoa michango wao kuonyesha njia pale walipoingia kati kukomesha mauaji.
 
Mzee embu muogope Mungu wako,kwa hiyo unataka kutuambia kati yako wewe uliyehadithiwa kuhusu Mapinduzi na Wazanzibar wenyewe wakiongozwa na Abdulhaman Babu chini ya Umma party walioshiriki Mapinduzi nani ni mkweli katika Usahihi wa kufanya Mapinduzi hayo?
 
Huyu mzee amepata hitilafu kabisa kiakili!
Anamlilia mkoloni kwakuwa tu ni mwisilamu mwenzake na mwarabu!? Aibu gani hii kwa Mwafrika!!

Waafrika Imani hizi za kigeni zililetwa kutupiga pingu za ubongo.
 
Huyu Mzee kila siku anamdisi Mwalimu Nyerere aliyeongoza harakati za uhuru wetu, ila huyu hapa anamsifia Sultani aliyepinduliwa kwa kuwanyima haki za kisiasa n.k wazanzibar.
Kisa na mkasa; Dini.
Huyu mzee ni mhaini na mkosi mkubwa kwa taifa letu! Ni zaidi ya gaidi sijui kwanini serikali inamwangalia tu.

Sina lugha nyingine juu yake zaidi ya hiyo.
 
Proved,
Uongozi wa ASP ulishirikiana serikali ya Tanganyika kufanikisha Mapinduzi.

Halikadhalika Makomredi yaani Umma Party walitoa michango wao kuonyesha njia pale walipoingia kati kukomesha mauaji.
Hao ASP na umma party walikuwa watanganyika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…