BURIANI Sultan Jamshid BIN Abdulla BIN Khalifa (1926 - 2024)

BURIANI Sultan Jamshid BIN Abdulla BIN Khalifa (1926 - 2024)

Mzee embu muogope Mungu wako,kwa hiyo unataka kutuambia kati yako wewe uliyehadithiwa kuhusu Mapinduzi na Wazanzibar wenyewe wakiongozwa na Abdulhaman Babu chini ya Umma party walioshiriki Mapinduzi nani ni mkweli katika Usahihi wa kufanya Mapinduzi hayo?
Fainali...
Hapana haja ya maneno kama hayo ya kumtaja Mungu.

Niulize tu utakalo nami nitakujibu.

Mimi nimeshiriki katika utafiti wa historia ya mapinduzi nikiwa Mtafiti Msaidizi wa Dr. Harith Ghassany aliyeandika kitabu, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," (2010).

Kazi hii nimeifanya kwa miaka 7 kuanzia 2003 hadi 2010.
Ukikisoma kitabu hiki utajifunza mengi sana katika historia ya mapinduzi.

Softcopy ya kitabu ipo Google.

1735654020701.jpeg

Kipumbwi Tanga 2003​
Katika kijiji hiki cha Kipumbwi, Tanga ndipo mamluki wa Kimakonde walikuwa wakivushwa kwa siri kuingia Zanzibar na kiongozi wao alikuwa Mohamed Omari Mkwawa.

1735654339117.png

Picha ndani ya kitabu
 
1735655022773.png

Inachanganya mbona wanasema ana 95 na hapa inaonekana ana 98
 
Huyu mzee ni mhaini na mkosi mkubwa kwa taifa letu! Ni zaidi ya gaidi sijui kwanini serikali inamwangalia tu.

Sina lugha nyingine juu yake zaidi ya hiyo.
Mzizi...
KITABU KATIKA KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR SEHEMU YA KWANZA
PITIO LA KITABU: ''MIMI, UMMA PARTY NA MAPINDUZI YA ZANZIBAR'' MWANDISHI: HASHIL SEIF HASHIL

Kuandika historia ya ukombozi katika nchi za Kiafrika kunahitaji ujasiri mkubwa sana na sababu yake ni kuwa Afrika ina historia rasmi.

Historia hii rasmi ni ile ambayo imepitishwa na kukubalika na watawala.
Historia hii ikishaandikwa ndiyo mwisho kwani haitoi nafasi ya kuwapo kwa historia nyingine itakayokwenda kinyume na hiyo.

Hii ni moja ya sifa ya siasa katika Afrika.
Historia rasmi ndiyo hiyo itakayokuwa katika mitaala kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu.

Hatari yake ni kuwa inasababisha na pengine kwa miaka mingi sana kusomeshwa historia yenye upungufu hadi pale atakapotokea mtu jasiri akaandika ukweli.

Wako watu bado wa hai na pengine wapo hapa ukumbini wanaijua historia ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuyaona mapinduzi yenyewe na kwa kushiriki lakini hawajanyanyua kalamu kuandika wala kufungua mdomo kuihadithia na watakwenda kaburini na watazikwa na historia zao ambazo laiti wangeliziandika nchi ingenufaika pakubwa.

Hashil Seif Hashil anastahili pongezi kwa ujasiri huu wa kutuandikia kitabu na kutueleza historia ya Zanzibar ambayo si wengi wanaijua khasa vijana waliozaliwa baada ya mapinduzi mwaka wa 1964 ambao kwa sasa ni watu wazima.

Kuiandika historia ya mapinduzi ya Zanzibar ni kazi inayohitaji, ushujaa kwani si rahisi kuieleza na ukakosa kuwaudhi baadhi ya watu na wengine watu wako wa karibu sana.

Afrika tuna utamaduni wa kuzifanya historia zetu kuwa kitu nyeti kwa hiyo iogopwe na isiguswe kwa kuigeuzageuza kutaka kujua undani wake.

Hashil Seif ni mwandishi jasiri na mtu huwezi kustaajabu kwa huu ujasiri wake utakapoijua historia yake binafsi.

Hashil Seif mwaka wa 1962 akiwa kijna mdogo kabisa wa umri wa miaka 26 alitoroka Zanzibar pamoja na wenzake wapatao 20 kwenda Cuba kupata mafunzo ya vita kwa nia ya kurejea Zanzibar na kupindua serikali na kuweka utawala wa Ki-Marxist.

Hili la kwanza na kaeleza katika kumbukumbu hizi.
Pili, Hashil Seif hajasita hata mara moja katika kitabu hiki kueleza kuwa yeye alikuwa mwanachama wa ZNP, maarufu kwa jina la ‘’Hizbu.’’

Katika historia ya Zanzibar baada ya mapinduzi neno, ‘’Hizbu,’’ lilikuwa linatisha na kuna watu na si wadogo hadi leo bado wana hofu kubwa ya kunasibishwa na historia yao katika Hizbu.

Katika kumbukumbu hizi Hashil Seif anaeleza historia yake ndani ya chama hiki na mchango wake kama kijana katika Youth Own Union (YOU) bila hofu wala wasiwasi wowote na hadi leo katika umri mkubwa wa miaka 80 bado ni komredi na hajabadili fikra zake za siasa za mrengo wa kushoto.

Katika kitabu hiki Hashil Seif anaeleza fikra zake kama bado yuko katika Zanzibar ya miaka ya 1960 bila ya kuongeza wala kupunguza nukta.

Hii ni moja ya mambo yanayokifanya kitabu hiki kiwe kiongozi katika kuijua historia ya mapinduzi na wanasiasa wake wa nyakati zile.

Ili kitabu kiwe kitabu ni lazima kiwe kina elimu mpya ambayo kabla haikuwa inajulikana.

Wazanzibari wengi, ukimtoa Dr. Harith Ghassany: ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,’’ (2010), walioandika historia ya mapinduzi wote wamepita mle mle katika historia rasmi.

Msomaji hapati jipya isipokuwa tofauti ya jalada, jina la kitabu na la mwandishi.

Unapoanza kumsoma Hashil Seif mwanzoni tu unakuwa mfano wa mtu aliyekuwa kalala usingizi fofofo na ghafla anatokea mtu akammwagia maji baridi usoni na kwa maji yale akashtuka kutoka usingizini na pengine kwenye ndoto akawa karejea katika dunia ya kweli.

Hashil Seif anakifungua kitabu kwa majina ambayo hutayakuta katika historia tuliyoizoea ya mapinduzi ya Zanzibar.

Hashil Seif katika kitabu hiki kataja majina ambayo yalifutika katika historia ya Zanzibar na kama utayakuta basi yatakuwa yemetajwa, ‘’in passing,’’ kama Waingereza wasemavyo, yaani majina hayo yatakuwa yametajwa kijuujuu.

Nitatoa mfano kwa uchache.

Hashil anawataja mara kadhaa katika kitabu Abdulrahman Babu, Khamisi Abdallah Ameir, Ali Sultan Issa na Badawi Qullatein katika siasa za kupigania uhuru wa Zanzibar.

Ahmed Rajab mmoja wa makomredi, ambae kaupitia mswada wa kitabu hiki ameniandikia na kunifahamisha kuwa Khamis Abdallah Ameir kama ‘’Theoretician,’’ sifa hii hutaisoma katika kitabu lakini katika mawasiliano yangu na Ahmed Rajab hili kanieleza na akasema kuwa Khamis Abdallah Ameir hakuwa mwanachama wa kawaida katika harakati zile.

Hili lilidhihirika baada ya mapinduzi kwa Khamis Abdallah Ameir kuwa memba wa Baraza la Kwanza la Mapinduzi.

Khamis Abdallah Ameir sikupatapo kumsikia kabla mpaka nilipomuona hapa katika ukumbi huu katika muhadhara wa Abdallah Kassim Hanga na sasa kaletwa tena na Hashil Seif.

Babu, Ali Sultan na Badawi Qullatein hawahitaji maelezo.

Bahati mbaya sana kuwa kitabu hakikuwekwa faharasha yaani ‘’index,’’ lakini laiti ingekuwapo faharasha msomaji angeweza kuona umuhimu wa wazalendo hawa waliotajwa katika kitabu hiki kwa kuangalia ni mara ngapi majina yao yametajwa katika historia hii.

Huu ni mfano mmoja tu katika majina mengi ambayo hayajatajwa katika historia ya Zanzibar lakini Hashil Seif ameyarejesha na kueleza historia za watu hao katika kupigania uhuru wa Zanzibar.

Msomaji atamsoma Ali Sultan Issa aliyekuwa Mkomunisti ndani ya ZNP, Badawi Qulattein, Salim Rashid aliyekuwa katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.

Wazalendo hawa historia zao zina mvuto wa pekee kabla na baada ya mapinduzi.

Ali Sultan ndiye aliyetengezeza mpango mzima wa kuwapeleka vijana wa ZNP, Cuba kwa mafunzo ya kijeshi kujitayarisha kwa mapinduzi.

Haya ndiyo msomaji atakutananayo katika kitabu hiki na ikiwa ni hivi ndivyo hali ilivyokuwa wakati wa kupigani uhuru wa Zanzibar haiwi tabu kuelewa sifa za makomredi katika uongozi na mchango wao katika mapinduzi.

1735656483013.png
 
Basi jitahidi kufanya taafiti kabla ya kukimbilia keyboard
Much...
Hapana ndugu yangu niliona kosa na nikasasahisha kwenye text.
Na kukosea ni sifa ya binadamu.

Allah peke yake ndiye asiyekosea.
Niwie radhi kwa hilo.

Hapana sababu ya hayo maneno, ''kukimbilia keyboard.''
Heshima kitu cha bure.
 
Mnaitawala Zanzibar au nyie ndiyo mnatawaliwa!
Zanzibar ni sawa na mtaa mmoja tu wa huku bara ukipiga filimbi watu wote wanakusanyika, sasa we uliona wapi mtaa ukatawala nchi?
 
Unaweza ukaeleza huo msaada ni upi?
Much...
Wanachama wote wa TANU walikuwa wanaunga mkono ASP kuanzia mwaka wa 1957 chama kilipoasisiwa.

TANU walikuwa na mtu maalum aliyekuwa akipeleka fedha Zanzibar na ndiye alikuwa mwakilishi wa Mwalimu kwa Karume.

Karume alikuwa akija Dar es Salaam akifikia nyumbani kwa mtu huyu.

Mwalimu akaweka kambi ya Kipumbwi Tanga na akamteua Jumanne Abdallah kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Ali Mwinyi Tambwe Mkuu wa Wilaya.

Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mtu wa Mwalimu sana na wakati wa kupigania uhuru alikuwa mkono wake wa kulia.

Ali Mwinyi na Abdul Sykes ndiyo walimjadili Nyerere nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio vipi wamwingize kugombea nafasi ya President wa TAA 1953 na 1954 TANU iundwe na Mwalimu aongoze mapambano ya kudai uhuru.

Lakini kubwa ni kuwa Ali Mwinyi TANU alikuwa mtu wa Special Branch wakati wa ukoloni.
Kipumbwi ilikuwa chini yake na yeye ndiye aliyemwingiza Mohamed Omari Mkwawa katika harakati za Zanzibar kuelekea uchaguzi wa 1961, 1963 na mapinduzi 1964.

Halikadhalika kwa kazi hii ya Zanzibar Mwalimu alimteua Oscar Kambona kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na Kambona akafanya kazi hii kwa ufanisi na usiri mkuwa na Abdallah Kassim Hanga.
 
Kuungwa mkono kwa ASP na TANU ni jambo la kawaida maana vyama vyote vya ukombozi Africa vilikuwa vikishirikiana ni sawa na wa southAfrica walalamike kwanini tuliiunga mkono ANC kupambania uhuru wao
 
Much...
Wanachama wote wa TANU walikuwa wanaunga mkono ASP kuanzia mwaka wa 1957 chama kilipoasisiwa.

TANU walikuwa na mtu maalum aliyekuwa akipeleka fedha Zanzibar na ndiye alikuwa mwakilishi wa Mwalimu kwa Karume.

Karume alikuwa akija Dar es Salaam akifikia nyumbani kwa mtu huyu.

Mwalimu akaweka kambi ya Kipumbwi Tanga na akamteua Jumanne Abdallah kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Ali Mwinyi Tambwe Mkuu wa Wilaya.

Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mtu wa Mwalimu sana na wakati wa kupigania uhuru alikuwa mkono wake wa kulia.

Ali Mwinyi na Abdul Sykes ndiyo walimjadili Nyerere nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio vipi wamwingize kugombea nafasi ya President wa TAA 1953 na 1954 TANU iundwe na Mwalimu aongoze mapambano ya kudai uhuru.

Lakini kubwa ni kuwa Ali Mwinyi TANU alikuwa mtu wa Special Branch wakati wa ukoloni.
Kipumbwi ilikuwa chini yake na yeye ndiye aliyemwingiza Mohamed Omari Mkwawa katika harakati za Zanzibar kuelekea uchaguzi wa 1961, 1963 na mapinduzi 1964.

Halikadhalika kwa kazi hii ya Zanzibar Mwalimu alimteua Oscar Kambona kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na Kambona akafanya kazi hii kwa ufanisi na usiri mkuwa na Abdallah Kassim Hanga.
Malengo ya TANU kuisapoti ASP yalikuwa yapi?
 
Zanzibar wanayaita mapinduzi matukufu.

Oman wanayaita mauaji ya kimbari.
 
Kwa hiyo unataka kusema Kitabu cha Ghassanry ndio Ukweli pekee na Historia nyingine yoyote ni Uongo
Fainali...
Hapana haja ya maneno kama hayo ya kumtaja Mungu.

Niulize tu utakalo nami nitakujibu.

Mimi nimeshiriki katika utafiti wa historia ya mapinduzi nikiwa Mtafiti Msaidizi wa Dr. Harith Ghassany aliyeandika kitabu, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," (2010).

Kazi hii nimeifanya kwa miaka 7 kuanzia 2003 hadi 2010.
Ukikisoma kitabu hiki utajifunza mengi sana katika historia ya mapinduzi.

Softcopy ya kitabu ipo Google.

View attachment 3189459
Kipumbwi Tanga 2003​
Katika kijiji hiki cha Kipumbwi, Tanga ndipo mamluki wa Kimakonde walikuwa wakivushwa kwa siri kuingia Zanzibar na kiongozi wao alikuwa Mohamed Omari Mkwawa.

View attachment 3189462
Picha ndani ya kitabu
 
Mtu mwema au ufalme utokanao na watu kamwe hauwezi pata upinzani au mapinduzi kutoka kwa watu wake.

Ukiona ufalme umepinduliwa jua ni ufalme aliojipa madaraka wenyewe,umeua na kuumiza,umeleta madhira kwa watu hadi watu wakauchoka na kuamua kuleta mapinduzi.

Huyo sultan ni moja kati ya watawala walio umiza sana wazanzibar kwa kuwafanya watumwa katika nchi yao,wakati huo yeye sio mzawa halisi wa visiwa hivyo bali ni uzao wa watesi kutokea omani.

Daima mapinduzi matukufu ya enziwe kutoa utawala haramu wa sultani.
Huyu Mzee anachoamini na kutaka kutuaminisha ni kuwa Masultan wa Zanzibar walikuwa watu wazuri sana na waliwaletea Wazanzibari Dini,majengo makubwa mazuri,Ustaarabu n.k

Na huwa anaamini kuwa hakukuwa na haja ya Mapinduzi Zanzibar, na walioleta mapinduzi ya kumwaga damu ni Wakristo

Huyu Mzee hamjamjua bado?
 
Embu tuelezee ushiriki wa Kanali Ali Mahfuodh katika Mapinduzi hayo,kwanini alikwenda Cuba kupata mafunzo makali na kukubali kuumia tena kwa hiari yake mwenyewe wakati Zanzibar kulikuwa na Raha na hakukuwa na ubaguzi au udharimu wa hao masultani?
 
Back
Top Bottom