SI KWELI Burkina Faso inajenga sanamu kwa ajili ya Rais wao Traore

SI KWELI Burkina Faso inajenga sanamu kwa ajili ya Rais wao Traore

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu nimeona huko mitandaoni hili jambo lina trend sana
Ibra Statue Sept 20,.jpg

​
 
Tunachokijua
Captain Ibrahim TRAORÉ ni Rais wa kijeshi chini Burkina Faso aliyefanya mapinduzi ya kumtoa Rais wa wa mpito wa wakati huo ambaye alikuwa ni mwanajeshi pia Paul-Henri Sandaogo Damiba September 2022. Aidha Captain Ibrahim anatajwa kuwa miongoni mwa marais wenye umri mdogo zaidi barani Afrika na duniani.

Madai

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook na TikTok kumekuwapo na taarifa inayoeleza kuwa wananchi wa Burkina Faso wanajenga sanamu la Rais wao, Ibrahim Traoré kama njia ya kumpongeza, taaifa hiyo imeambatana pia na picha inayoonesha sanamu hilo.

Uhalisia wa madai hayo

JamiiCheck imefuatilia kwa kina taarifa hiyo na kubaini kuwa haina ukweli wowote.

Ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo za kidigitali ikiwemo google reverse image search, JamiiCheck imebaini uwepo wa picha nyingine nyingi zinazofanana na hiyo zikiwahusisha watu mbalimbali ikiwemo viongozi zikiwa zimechapishwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii. Tazama hapa

Picha hiyo inayoonesha sanamu la Traoré na nyinginezo zimetengezwa kwa teknolojia ya Akili Unde kutoka google ambayo imekuwa mashuhuri hivi karibuni na kupelekea uwepo wa picha nyingi za aina hiyo.

Utafutaji zaidi umebaini kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo kumuhusu Rais huyo wa Burkina Faso. Taarifa za mwisho zinaeleza kuhusu sanamu la aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Thomas Sankara.

Taarifa hii imekuwa ni muendelezo wa Taarifa za uzushi zinazotengenezwa kumuhusu Rais huyo wa Burkina Faso. Mathalani tizama hapa, hapa na hapa kuona taarifa nyingine zilizohakikiwa na JamiiCheck kumuhusu Rais Traoré​
Back
Top Bottom