Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Burkina Faso iliyo chini ya utawala wa kijeshi wa Kapteni Ibrahim Traore imeanzisha utaratibu wa kurusha live kesi zote zinazohusu ubadhirifu wa fedha za umma.
Utaratibu huo umeanza mwezi Novemba 2024 na watuhumiwa walioanza nao ni maafisa wa wizara ya misaada ya kibinadamu wanaotuhumiwa kuiba fedha zilizotolewa kwa ajili ya kusaidia wananchi waliokimbia makazi yao kutokana na sababu za kiusalama.
Kesi hizo zinarushwa live kwenye vituo mbalimbali vya Televisheni, Chaneli za YouTube pamoja na kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ili kuwawezesha wananchi wote kujionea mwenendo wa kesi hizo.
Katika mwenendo wa kesi inayowahusu maafisa wa wizara ya misaada ya kibinadamu,leo tarehe 17 Disemba 2024 mmojawapo wa watuhumiwa aitwaye Amidou Tenya amekiri kuiba kiasi cha CFA Francs milioni 44 ambazo ni sawa na shilingi Milioni 12 za Tz katika nyakati mbalimbali kati ya mwaka 2023 na 2024.
Amidou amesema kwamba alitumia pesa hizo kwa ajili ya kununua shamba, jumba la kifahari pamoja na kumjengea nyumba baba yake aliyepo nchini Ivory Coast.
Amidou amekiri kuiba kiasi hicho cha fedha ingawa anatuhumiwa kuiba kiasi kikubwa zaidi ya alichotaja na kutumia kujenga hotel ya vyumba 20, mabwawa mawili ya kuogelea, kiwanda cha kuzalisha chakula cha mifugo, kuchimba visima virefu vinne ,kununua shamba na kuanza ufugaji wa wanyama mbalimbali kama ng'ombe, swala pamoja na ndege aina ya mbuni, kununua magari ya kifahari pamoja na kununua wanyama kama ng'ombe na ngamia waliotumika kwenye ibada ya "zindiko" ili kuzuia serikali kutambua wizi alioufanya.
Watuhumiwa wengine walikana mashtaka yao na kesi imeahirishwa hadi hapo itakapotajwa tena. Endapo watuhumiwa hao watakutwa na hatia, watakabiliwa na adhabu mbalimbali ikiwemo mali zao kuuzwa ili serikali iweze kurudisha kiasi kilichoibiwa.
Kwa upande mwingine mawakili wa upande wa utetezi wameomba utaratibu wa kurusha kesi mubashara ukomeshwe kwa madai kuwa unawadhalilisha watuhumiwa wao .
Chanzo: YouTube Channel ya Shirika la habari la Burkina Faso ( RTB)