Burkina Faso yafuta leseni za mashirika manne ya kigeni

Burkina Faso yafuta leseni za mashirika manne ya kigeni

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Burkina Faso imefuta leseni za mashirika manne ya misaada ya kiutu ya kigeni kuendesha shughuli zao nchini humo, na kusimamisha mashirika mengine mawili.Kwa mujibu wa amri ya serikali, iliyotiwa saini katikati ya mwezi Juni, inamnukuu waziri mmoja wa serikali akisema kuwa hatua dhidi ya mashirika hayo imetokana na ukiukaji wa taratibu rasmi.

Mashirika mengine mawili ya kigeni yaliyotajwa katika amri hiyo yamesimamishwa kwa muda wa miezi mitatu, moja likituhumiwa kwa uvunjaji wa sheria za usalama wa taarifa.

Utawala wa kijeshi wa Burkina Faso, mara kwa mara umekuwa ukishutumiwa kwa kuukandamiza upinzani, hasa kutoka kwa mashirika ya kiraia na vyombo vya habari kwa madai kuwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugaidi.

Wanadiplomasia waliotuhumiwa kwa shughuli za "uchochezi” wamefukuzwa, na vyombo kadhaa vya habari vya kigeni vimefungwa.
 
Safi sana. Ni wakati wa Africa kukataa ujinga ujinga usiokuwa na maana.
 
Back
Top Bottom