Burna Boy ana record kubwa balaa

Burna Boy ana record kubwa balaa

Storm shadow

Senior Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
167
Reaction score
132
Damini Ebunoluwa Ogulu maarufu kama 'Burna Boy' wengi wamemjua hivi karibuni lakini jamaa anatisha tokea mda kidogo, 2012 aliaachia single yake ya Like to Party kutoka katika album yake ya L.I.F.E iliyoachiwa 2013 na kuuza copies 40,000 Siku hiyohiyo ilipoachiwa.

2014 album take hiyo ilishinda tuzo za Nigeria entertainment award na kikubwa zaidi lishika no 7 billboard reggae album charts. 2017 jamaa alisainiwa Atlantic Record Label ya USA na Warner group kimataifa. January 2018 alishirikishwa na fall out boys kwenye hit song sunchine ambayo ilikuwa nominated kwenye tuzo za Grammy.

Pia, album yake ya Outside ilishinda tuzo za Nigeria Entertainment Award kipengele cha best Nigeria Album, October 7 aliperfom O2 academy brixto ambapo aliuza ticket zote (sold out). October 9alitangazwa na Spotify kuwa new afro hub take over

January 2019 alishinda tuzo 4 za Sound City MVP march 21 aliachia ngoma 3 na kundi la djds la Los Angeles. Mwezi June alishinda tuzo za BET award. Mwezi July aliachia album ya African giant aliyowashirikisha Future, YG, Jeremih na wengine.

Pia, aliperfom kipindi kinachoongoza kutazamwa na watu wengi cha Jimmy Kimmel. Ameshiriki katika album ya lion king the gift ya Beyonce. Na katika album ya DJ Snake carte Blanche akiwa msanii pekee kutoka Africa album almbayo imeshakuwa streamed 1billion on Spotify
 
Attachments

  • FB_IMG_15649868005432750.jpg
    FB_IMG_15649868005432750.jpg
    25.2 KB · Views: 34
  • FB_IMG_15649868005432750.jpg
    FB_IMG_15649868005432750.jpg
    25.2 KB · Views: 35
  • FB_IMG_15649867095826132.jpg
    FB_IMG_15649867095826132.jpg
    64.4 KB · Views: 39
  • FB_IMG_15649867095826132.jpg
    FB_IMG_15649867095826132.jpg
    64.4 KB · Views: 36
Tatizo nyie wasanii wa naija mmewajua kipindi iki..mimi ninewajua toka enzi hizo bado kabisa na sidhani kuna mtu humu jf anawajua wasanii wa naija zaidi yangu...

Nimemjua Burnaboy toka hajatoa wimbo wa Wombolombolo, like to party,Run my race, Yawa Dey, Don gordon, Etc etc.. Jamaa ni moja kati ya vocalist wakubwa afrika na chorus killer.. nimeacha kua shabiki kindaki ndaki 2016 baada ya kuishi na watu wanaosikiliza muziki wa bongo zaidi.

Home kwetu enzi hizo mdogo wangu wa miaka 5 anataja wasanii wa naija wote wanaotrend na nyimbo zao. Toka wizkid anatamba na kibao chake cha Holla at your boy bado hajatoa Kibao Na Femi kuti 2013 kilichomsogeza far kidogo
 
@Da'Vinci nimemsikili za Burma toka kitambo coz nawafuatilia Nigerian music toka mda and nawajua artist wao more than u think
 
@Da'Vinci

Tatizo gereration ya sasa inayopenda mziki inaongozwa na kina ADAM MCHOMVU and the likes ambao wengi wao ni watupu sana katika mambo ya mziki sema kelele nyingiii
 
Huyu mchiz nilikiwa simfaham before mapaka aliporekod na WBC ,ndipo nilipoanza kumfatilia ,wimbo wake wa Angelina ni bor a kwangu
 
miaka kama minne iliyopita nilikua nawafuatilia sana wasanii wa Nigeria ila sikuwahi kumjua Burna Boy mpaka pale nilipoona matangazo yake ya yeye kuja Mtwara kuperfom akiwa na msanii mwingine wa Nigeria nimemsahau(hii ilikua kabla hata ya kufanya collabo na Kina Mondi) na ilikua mara yake ya kwanza kuja Tanzania ikabidi nianze kufuatilia vibao vyake..dah nikajikuta nae nampenda tu
 
Basi we ulikuwa hufatilii vizuri mbona burna boy ana. Ngoma nyingi kubwa alizo shirikishwa kama all eyes on me ya AkA ambayo ili trend adi bongo

sidhani kama muda aliokuja bongo ngoma hiyo na AKA ilikua tayari imeshatoka..na kingine hata ufuatilie vipi wasanii huwezi kuwajua wote utastukia tu siku unaambiwa "ah wewe humjui fulani mbina ni msanii mkubwa tu" na muda huo unafuatilia muziki nje ndani
 
Ndo ivyo maana wasaani ni wengi
sidhani kama muda aliokuja bongo ngoma hiyo na AKA ilikua tayari imeshatoka..na kingine hata ufuatilie vipi wasanii huwezi kuwajua wote utastukia tu siku unaambiwa "ah wewe humjui fulani mbina ni msanii mkubwa tu" na muda huo unafuatilia muziki nje ndani
 
Daah ana wimbo wake moja matata sana sema jina nimesahau, wengine tunatumia Dstv hivyo kuona hao watu kawaida tuu
 
They call me Buuuuurnnerr! ... the killer. Bonge moja la vocal. No papara.
 
Back
Top Bottom