#COVID19 Burundi imeridhia kupokea chanjo ya Covid 19 lakini Serikali haitawahamasisha watu kupata chanjo hiyo

#COVID19 Burundi imeridhia kupokea chanjo ya Covid 19 lakini Serikali haitawahamasisha watu kupata chanjo hiyo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
waziri wa afya nchini humo, Dkt Thaddée Ndikumana amewaambia waandishi wa habari kuwa chanjo hizo zimependekezwa na Benki ya Dunia na wakachukua uamuzi wa ''kuzikaribisha''.

Aliongeza, hatahivyo serikali haitahamasisha watu kuchoma chanjo, bali kila atakayehitaji ataifuata chanjo hiyo.

Mamlaka ya Burundi wamekuwa na wasiwasi kuhusu kupokea chanjo hizo, na hapo awali walisema watafuatilia ufanisi wa chanjo katika maeneo mengine, kabla ya kuzikubali nchini.

Katika mkutano na wanahabari, waziri alithibitisha ripoti kuwa maambukizi ya virusi vya corona yameongezeka katika wilaya za kaskazini zilizo maeneo ya mpakani na Rwanda, na mji wa kibiashara wa Bujumbura.

Kwasababu hiyo, amesema watafungua vituo vya tiba katika mikoa iliyoathirika.

Wizara ya afya ya Burundi hadi sasa imeripoti maambulizi karibu 6,000 vya Covid tangu janga hilo lilipoingia nchini humo mwezi Machi 2020.
 
Hiyo nimeipenda, sio wengine wanaleta chanjo na kusema wataalamu wamejiridhisha kuwa ni salama na kuanza kuzipigia debe halafu wakati huo huo chanjo zenyewe wamefanya kama operation hawana uhakika yani ukichaja litakalokupata wao wamejitoa hawahusiki.
 
Ila chanjo imekuwa na siasa nyingi sana.

Si kwa mataifa yaliyoendelea pekee sasa hadi huku kwetu ndio imekuwa tabu tupu.
 
Jamani wananchi wana haki ya kuelimishwa na kupewa uhuru wa kuchagua.
Bila shaka,ila nakuwekea vizuri zaidi sentensi yako...."wananchi wana haki ya kuelimishwa faida na HASARA za chanjo hii halafu wao wenyewe ndio wanachague"...

Pia haina haja ya kutumia watu maarufu kama wasanii nk kuhamasisha watu wachanje wakati tayari wameshapewa elimu kuhusu faida na hasara za chanjo,tuwaache wenyewe wachague,tusiwahamasishe.

Msitufanye sisi wajinga.
 
Waafrika wengine washachoka maisha haya ya dhiki wanatafuta kifo cha heshima tu wasemwe wamekufa kwa ugonjwa, mnawalazimisha nini jamani kuendelea kuishi?
Hata mimi nashangaa!

Tangu lini mzungu akapenda waafrika waishi?,tangu lini mzungu akahuzunishwa na vifo vya waafrika kiasi cha kufanya juhudi ya kutulazimisha kudungwa chanjo ili tusife?!!...tangu lini?

Ukitaka kujua kama asilimia kubwa ya wananchi hata walio "uswahilini" wameshtuka na hawataki kudungwa chanjo hii,fanya uchunguzi wako huko mitaani....

Mshike ndege tunduni,wajanja wamekimbia!
 
Mzungu ni nani?
 
Hiyo nimeipenda, sio wengine wanaleta chanjo na kusema wataalamu wamejiridhisha kuwa ni salama na kuanza kuzipigia debe halafu wakati huo huo chanjo zenyewe wamefanya kama operation hawana uhakika yani ukichaja litakalokupata wao wamejitoa hawahusiki.
Ni sawa na jirani anayekuja kula kwako kila siku ila akiona juice anaogopa, anasema utakuwa umemwekea sumu.

Yaani watu hawaulizi dawa zote zilizovumbuliwa na kutengenezwa na kampuni za nchi za kigeni kama ni salama. Ila chanjo tu ya COVID-19. Tunakula ARV, dawa za malaria, tunapigwa chanjo za Hepatitis, Polio n.k huko kote hakuna shida ila Chanjo ya COVID-19.

Wengine wanasema wangeanza na chanjo ya UKIMWI, Off course ingependeza pia, lakini UKIMWI umesababisha KCMC watumie ya mitungi ya Oxygen 400 kwa siku? Halafu wewe wategemea kula kwa jirani, kwanini umpangie cha kupika?
 
Hata mimi nashangaa!

Tangu lini mzungu akapenda waafrika waishi?,tangu lini mzungu akahuzunishwa na vifo vya waafrika kiasi cha kufanya juhudi ya kutulazimisha kudungwa chanjo ili tusife?!!...tangu lini?

Ukitaka kujua kama asilimia kubwa ya wananchi hata walio "uswahilini" wameshtuka na hawataki kudungwa chanjo hii,fanya uchunguzi wako huko mitaani....

Mshike ndege tunduni,wajanja wamekimbia!
Duuh.....

Kwa hiyo wazungu hawataki mwafrika aishi si ndio eee?!!!

Mbona wanatuletea ARV's bure tunabugia na kutoka vitambi?!!

Hizo njugu zinatengenezwa Mwalusembe?!!

Kwa hiyo mzungu hamuihitaji mwafrika kama cheap labour ,kama mnunuzi wa biashara zake ?
 
Misimamo hiyo 🤣🤣

Duuuh....

#TujiandaeKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
 
Mbona wanaoelimisha watu kukataa chanjo wanapigwa vita wakati ilipaswa wenye kuelimisha umuhimu wa chanjo na wenye kuelimisha madhara ya chanjo wapewe fursa sawa ili Raia wafanye uamuzi baada ya kupata elimu ya pande zote mbili
Ndio maana UFARANSA chanjo ni lazima.....

Katikati ya VITA mnatoa Uhuru wa kuchagua la kufanya?!!

Anyways ,tungoje tuone huko mbele kama hiyari hii itaendelea.....

#TujiandaeKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
 
Mwanzo tuliambiwa ukichanja hupati corona, baadae watu wakawa wanapata Maambukizi tukaambiwa Unaweza kupata Corona lakin hautakuwa Mahututi

Ntajie chanjo nyingine yenye sifa hii ya kuchanja na bado unapata hayo maradhi ila unaambiwa hutokuwa mahututi

52% ya Waliolazwa kwa maradhi ya Corona nchini Uingereza ni wale waliokwisha chanja kwa takwimu za hivi karibuni

Sasa hii ni chanjo dhidi ya corona au dhidi ya umahututi wa Corona?
Ndio maana UFARANSA chanjo ni lazima.....

Katikati ya VITA mnatoa Uhuru wa kuchagua la kufanya?!!

Anyways ,tungoje tuone huko mbele kama hiyari hii itaendelea.....

#TujiandaeKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
 
Duuh.....

Kwa hiyo wazungu hawataki mwafrika aishi si ndio eee?!!!

Mbona wanatuletea ARV's bure tunabugia na kutoka vitambi?!!

Hizo njugu zinatengenezwa Mwalusembe?!!

Kwa hiyo mzungu hamuihitaji mwafrika kama cheap labour ,kama mnunuzi wa biashara zake ?
1.ARVs=HIV/AIDS....yaani ARVs ndizo zinazoua na si HIV
2.ARVs unapewa bure wewe mwananchi na serikali yako,lakini serikali inanunua....unajua inanunua tshs ngapi dosage ya mwezi kwa mtumiaji mmoja?....unajua kwa mwezi mmoja serikali inatumia tshs ngapi kulipia dosage ya watumiaji wa nchi nzima?

Serikali ikinunua inatosha,si lazima anunue mwananchi,kina Rockefeller wanachotaka ni account isome,haijalishi pesa imetoka kwa nani....na isitoshe kina Rockfeller hawafanyi biashara na makapuku,wanafanya biashara na serikali za dunia.

Unahitaji kuwa very smart kunielewa.
 
Mbona wanaoelimisha watu kukataa chanjo wanapigwa vita wakati ilipaswa wenye kuelimisha umuhimu wa chanjo na wenye kuelimisha madhara ya chanjo wapewe fursa sawa ili Raia wafanye uamuzi baada ya kupata elimu ya pande zote mbili
Umejiuliza vyema sana....

Hivi serikali hiihii inayoruhusu biashara ya sigara kwa kuigonga chapa ya TBS ilihali watengenezaji wenyewe wa sigara hizo wameonya kwamba uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako unaweza kuiamini kwenye mambo mengine yahusuyo afya yako kweli?

Mchakato wa upatikanaji mpaka utumiaji wa hii chanjo unanikumbusha historia ya HIV kutangazwa kama "PROBABLE CAUSE" of AIDS halafu hata kabla ya utafiti na utaratibu wa kisayansi wa kuthibitisha hilo haujafanyika wakaanza kuruhusu ma AZT(ARVs) kutumika bila hata scientific paper moja kuandikwa kuthibitishwa hilo....

Na ndio maana watu wengi sana wamekufa na wanaendelea kufa kwa madhara ya ARVs huku HIV akisingiziwa kwamba ndio muuaji wakati iko wazi kabisa na hata hao wanaotuaminisha kuhusu HIV wanajua kwamba huyo HIV hawezi kusababisha cancer,kisukari,ugonjwa wa moyo,upungufu wa damu,figo na ini kushindwa kufanya kazi...sasa wale watumiaji wa ARVs wanapokufa huwa wanakufa kwa matatizo haya....haya ndio matokeo ya kushabikia vitu tusivyovijua na kukurupuka kufuata akili za wazungu bila hata kujiridhisha wenyewe....

Baadhi ya makampuni yameandika kabisa kwamba chanjo yao haikuidhinishwa na FDA,lakini bado hatujiulizi kwanini zinatumika...halafu pia wamesema ukipata madhara wewe mtumiaji ndio utakua responsible kwa afya yako lakini pia hatujiulizi.Halafu chanjo haina hata miaka 2 tangu itengenezwe sasa utajuaje madhara ya miaka 10 baadaye?,hatuoni kwamba sisi ndio experimental specimen(guinea pigs),hatuoni hili kweli?

Ili mtu aunge mkono chanjo hizi kwanza lazime ajitoe ufahamu wake kisha ndio aunge mkono,vinginevyo huyo atakua kilaza wa kutupa na kichwani mwake hamna kitu kabisa.
 
Ni sawa na jirani anayekuja kula kwako kila siku ila akiona juice anaogopa, anasema utakuwa umemwekea sumu.

Yaani watu hawaulizi dawa zote zilizovumbuliwa na kutengenezwa na kampuni za nchi za kigeni kama ni salama. Ila chanjo tu ya COVID-19. Tunakula ARV, dawa za malaria, tunapigwa chanjo za Hepatitis, Polio n.k huko kote hakuna shida ila Chanjo ya COVID-19.

Wengine wanasema wangeanza na chanjo ya UKIMWI, Off course ingependeza pia, lakini UKIMWI umesababisha KCMC watumie ya mitungi ya Oxygen 400 kwa siku? Halafu wewe wategemea kula kwa jirani, kwanini umpangie cha kupika?
Hata hizo dawa zengine zina madhara inajulikana mfano hizo ARV zishajadiliwa sana humu ila tatizo ni kuonekana unapotosha sijui unapingana na wataalamu, sasa nawashangaa mnapokuja na hizo hoja za sijui mbona dawa/chanjo zengine mnatumia wakati zikijadiliwa mnasema tunapotosha.

Halafu hilo suala la mitungi we unalielewa vp maana ubaya ni kwamba watu hata hawafuatilii mambo kwa kina kwenye issue zenye kuhusu corona.
 
Back
Top Bottom