Ni sawa na jirani anayekuja kula kwako kila siku ila akiona juice anaogopa, anasema utakuwa umemwekea sumu.
Yaani watu hawaulizi dawa zote zilizovumbuliwa na kutengenezwa na kampuni za nchi za kigeni kama ni salama. Ila chanjo tu ya COVID-19. Tunakula ARV, dawa za malaria, tunapigwa chanjo za Hepatitis, Polio n.k huko kote hakuna shida ila Chanjo ya COVID-19.
Wengine wanasema wangeanza na chanjo ya UKIMWI, Off course ingependeza pia, lakini UKIMWI umesababisha KCMC watumie ya mitungi ya Oxygen 400 kwa siku? Halafu wewe wategemea kula kwa jirani, kwanini umpangie cha kupika?