Burundi: Kwanini Viongozi wetu wakuu wameelekeza nguvu zao huko?

Soko kubwa la nini?
vitenge vya wax😀
mama kaenda kuchukua mishono mipya. SIku akija kukutana na wazee au vijana wa dar awe ametokelezea. Huku anakwambieni kwa sauti ya upole muendelee kuvumilia tozo maana anajenga uchumi.
 
Ni kukuza mahusiano kati yetu, Rwanda anaogopwa yule jamaa naona katuzidi ujanja tumeona bora tumkimbie tu.
Hahah Kuna video 1 niliona rais wa Burundi Gen. Neva anamwambia rais M7 'you're like a father of our nation(Burundi)' jamaa mmoja akaandika aisee kale kajamaa kembamba karefu ka Ile nchi nyingine ya jirani mtakaua tu lkn maneno hayo hakawezi kumwambia mtu kamwe,Hahah.
 
Wengi mmesahau kuwa Burundi ina Wakimbizi wengi pale Kigoma, na Serikali ilishatia nia ya kutaka kuwarudisha. Hope kutakuwa na mazungumzo ya jambo hili la Wakimbizi manake yenyewe Burundi kama haiko tayari kuwapokea kwa sasa inataka waendelee kusalia Tanzania.

Suala la mahusiano ya Kikanda litateka pia mazungumzo yao ukizingatia pia Viongozi wote ni Wageni, yule wa Burundi na Tanzania baada ya Viongozi wao wa awali Kupatwa na Umauti.
 
Burundi ni Soko kubwa la Nini? Maana usiandike kama unawasimulia watu wa kijiweni. BURUNDI NI SOKO KUBWA LA NINI?
Unajua maana ya soko ngoja nikupe maana ambayo sio common sana kwa walio wengi.

A geographical area where a certain commercial demand exists. Sasa kama unaona wanaagiza bidhaa fulani kutoka nchi zingine na wana pitishia nchini mwako bidhaa hizo kupitia bandari yako huoni huko kuna soko ila ni akili mgando tu zimegoma namna ya kupeleka bidhaa zinazo hitajika huko?
 
Walisaidia sana wakati wa uchaguzi. We hujui tu.
 
Unataka twende kwenu Rwanda
 
Ni ujinga tu wa viongozi waliopita kushindwa kuufungua mkoa wa kigoma. Vinginevyo burundi ni soko kubwa sana na nirahisi kuingia kule tofauti na nchi kama rwanda na uganda.
Kwenye hoja hii nimekuelewa
 
Labda wanaenda kununua mafuta, maana Burundi 🇧🇮 yako chini kidogo
 
Burundi kuna kauhusiano ka asili na Mwenda zake na makamu wa raising mjue!
 
Diplomasia ya kiuchumi Ni vizuri mama atembelee jirani zake
 
Hivi ni nani huyu anayemtuma sana rais wetu safari nyingi nyingi za ndani na za nje? Frequently, Dom to Dar, Uganda, then Burundi, ni kweli ni utashi wa rais wetu kusafiri kiasi hiki, au kuna mtu anamwagiza!
 
Njoo na takwimu Burundi anapitisha Tani ngapi za mizigo Bandari ya Dar kwa mwaka ukilinganisha na nchi majirani Kama RWANDA, ZAMBIA, MALAWI NA CONGO.

nakuomba uje na takwimu samahani.
 
Hivi ni nani huyu anayemtuma sana rais wetu safari nyingi nyingi za ndani na za nje? Frequently, Dom to Dar, Uganda, then Burundi, ni kweli ni utashi wa rais wetu kusafiri kiasi hiki, au kuna mtu anamwagiza!
Mshauri wake ni yule wa awamu ya nne unakumbuka naye alikuwa mbobezi wa kuwa hewani kila wakati
 
BURUNDI KUNA SOKO LA NINI? KWA NINI USIJIBU UNAZUNGUSHA ZUNGUSHA TU MKIA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…