Burundi: Mwandishi wa habari ahukumiwa miezi 19 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kuvuruga usalama wa nchi na kusambaza taarifa za ukabila

Burundi: Mwandishi wa habari ahukumiwa miezi 19 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kuvuruga usalama wa nchi na kusambaza taarifa za ukabila

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mahakama mjini Bujumbura imemuhukumu kifungo cha miezi 19 Gerezani Mwandishi wa habari Sandra Muhoza baada ya kukutwa na hatia ya kuvuruga usalama wa nchi na kusambaza taarifa za ukabila.

Mwandishi huyo wa habari mwanamke wa Burundi alikamatwa mkoani Ngozi tangu mwezi Aprili mwaka huu na kuibua wasiwasi kuhusu uhuru wa vyombo vya habari katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Sandra Muhoza (42) ni Mwandishi wa habari wa La Nova Burundi, chombo cha habari cha mtandaoni kinachojulikana kuwa karibu na Mamlaka.

Soma Pia: Mtangazaji wa Burundi aliyefungwa asamehewa na Rais

Baada ya kukamatwa,mumewe alipokea ujumbe kutoka kwa simu yake ukisema ‘mkeo anazuiliwa katika Makao Makuu ya idara ya kitaifa ya ujasusi.

Hii si mara ya kwanza kwa wanahabari kulengwa nchini Burundi. Mnamo Mei 2023, mwanahabari Floriane Irangabiye alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kudhoofisha usalama wa nchi.

Hata hivyo Floriane Irangabiye baadae aliachiliwa huru kwa msamaha wa Rais Evariste Ndayishimiye.
 
Back
Top Bottom