Hizi hasira ni za mpira pekee au umeunganisha na za ugumu wa maisha?
Labda nikufafanulie,
TFF hawezi kukwepa lawama maana yeye ndo msimamizi mkuu wa soka anayetambulika na FIFA na siyo Wizara chini ya Bashungwa. Kwa taarifa yako hakuna kinachoweza kufanywa na waziri dhidi ya soka kama kinakiuka kanuni na TFF wakasimama halafu wakaadhibiwa. Tatizo la TFF ni kushindwa kusimama kwenye taaluma inayowahusu na kuruhusu siasa ziingiliane na soka wakati wanajua moja kati ya kanuni FIFA isiyopepesa macho ni ile inayokataza serikali kuingilia utendaji wa vyama vya soka popote duniani. Wao kama wataalamu (na mwanasheria wa TFF yupo) walitakiwa kumahauri Waziri madhara ya ukiukaji wa sheria, na kama angekataa ilikuwa bora waifute mechi na kutoa sababu kuliko kusogeza muda wakijua wanavunja sheria.