Jambo zuri ni kwamba mashabiki wote wa pande zote mbili hawana ubaya na Yanga(hakuna shabiki anayeilalamikia Yanga)...wao wanalia na TFF na Wizara hii inamaanisha hatua waliyochukua Yanga inaweza leta faida ya hii kitu kutojirudia siku za usoni,ukweli ni kwamba mswahili ukimzoesha jambo atalirudia tu mara 2,3,4...kwa hiki kilichotokea walioboronga kama wapo sawa kiakili jambo hili halitakuja tokea tena abadan...ukubwa wa hizi timu si za kuwabadilishia ratiba masaa mawili kabla ya game tena bila kuomba radhi bila sababu za msingi(si TFF si Wizara mpaka sasa wametoa sababu ya kusogeza mbele ghafla huu mchezo)wao walikuwa kama wanatoa order(kama vile wanawaambia watoto wa under 12)wakati vitu vina taratibu zake...si Simba si Yanga timu yoyote inayocheza ligi lazima iheshimiwe,kwani hili lililotokea ni kuzikosea heshima klabu zote hizi mbili na vilabu vingine vya ligi kuu kiujumla...mashabiki wameumia lkn kuna jambo linaweza kuwa limetibiwa kupitia maamuzi haya ya Yanga hasa imezipa heshima timu zote mbili kwamba "we (Simba&Yanga) are not cheap to that extent"