Dialogist
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 1,167
- 1,872
Wanandugu Habarini...
Nimekaa na kutafakari kama mtu mzima, na nikiwa safarini kuelekea pale makao makuu ya nchi, na kwa kuzingatia mahusiano yangu ya mbali na huyu Bwana, nimeona ni heri nami niandike neno.
Bwana Mbowe, natambua kuna mijadala mingi sana inaendelea kwenye mitandao ya kijamii na hata mitaani ya wewe na Makamu wako juu ya mtifuano na mtafaruku kwenye ugombezi wa nafasi nyeti chamani kwenu.
Bwana Mbowe, nimefanya utafiti usio rasmi kuanzia kule kwetu Nyamisati mpaka maeneo yote ninayokuwepo kila siku ikiwemo mitandao ya kijamii, na kwa mawasiliano na watu mbalimbali, ni hivi BRO HUKUBALIKI TENA. Yaani HUUZIKI, HUNA MVUTO WALA USHAWISHI BRO.
Sina imani kwamba jamii yote inayokukataa inahongwa, No.. watu wanatoa hisia toka moyoni kaka. Zama zako zimeisha, ni wakati wa mageuzi.
Kila jambo na muda wake. Kila kanda inamuunga mkono Lissu, haijalishi ni wapiga kura au sio wapiga kura. Na hata kama sio wapiga kura bado ni hao hao ndio utalazimika kufanya nao kazi pale "utakaposhinda" hiyo siku.
Wajumbe 1300 sio kitu mbele ya Wanachadema mamilioni ndani ya nchi. Inawezekana ukawaamini hao wajumbe wachache lakini wafanya maamuzi ya uhai wa chama ni mamilioni. Na ndio maana kuna msemo unasema "never underestimate the power of stupid people in a large group" huu msemo kwako una faida sana kwa uhai wa chama.
Kwa minajili hiyo na kila linaloendelea, basi Bwana Mbowe huna budi kufanya maamuzi magumu. Nayo ni KUACHIA NGAZI NA KUJITOA KUGOMBEA KWA HESHIMA YAKO!!
Linda heshima yako ndani ya chama. Na hili haimaanishi kwamba Lissu anakuogopa, kwamba utashinda. No way! Dalili hazipo na hata ukishinda huo ndio utakua mwanzo wa KIFO CHA KIKATILI SANA CHA CHADEMA. Unless ukae na LISSU mapema myajenge na msitishe mitifuano kwenye media, mtangaze kwamba ninyi ni kitu kimoja kuanzia sasa. Na yoyote atakayeshinda basi atamsapoti mwenzake.
"A GOOD DANCER MUST KNOW THE RIGHT TIME TO LEAVE THE STAGE, BEFORE AUDIENCE GETS BORED"
Ni hayo tu!!