digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 10,508
- 23,368
Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limefanikiwa kuwakamata watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya aliyekuwa Mhandisi wa Maji wa RUWASA Wilaya ya Busega, Safiel Peter Senzota (37). Tukio hilo lilitokea tarehe 25 Mei 2026 katika eneo la Mwanogi, Wilaya ya Busega.
Baada ya uchunguzi wa kina, mtuhumiwa wa kwanza alikamatwa tarehe 01 Juni 2026 jijini Dar es Salaam, na mtuhumiwa wa pili ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari Chegeni iliyopo wilaya ya Busega alikamatwa baadaye akiwa Bulima na sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Maswa.
Kupitia uchunguzi huo, Polisi wamefanikiwa kurejesha baadhi ya mali za marehemu ikiwemo kompyuta mpakato (laptop) na kadi ya ATM ya Benki ya CRDB.
Inasadikia kuwa Chanzo kikuu mauaji ni tamaa ya mali ambapo inadaiwa marehemu alimshirikisha mwalimu juu ya nia yake ya kununua Lori kwa ajiri ya karakana yake ya kufyatua tofari,hivyo baada ya kupewa taarifa wahusika waliingiwa tamaa na kumuua mhandisi sifael ili wachukue fedha .
My take: Walimu wenzangu punguzeni majigambo na kutaka maisha ya mtelezo mtaishia jera