Bush kusaidia mapambano dhidi ya saratani shingo ya kizazi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
bushii.jpg

Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush

KWA UFUPI
Bush aliyasema hayo jana wakati akizindua mkanda mwekundu na pinki kwa wanawake chini ya taasisi yake kwa kushirikiana na Mpango wa Umoja wa Mataifa wa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi.

Dar es Salaam. Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush, ameahidi kuisaidia Tanzania katika mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi ili kuokoa maisha ya mama.

Tanzania itakuwa nchi ya tatu kufaidika na mpango huo ikitanguliwa na Zambia na Botswana tangu kuzunduliwa kwake mwaka 2011.

Akizungumza kwenye Mkutano wa wake wa Marais wa Afrika, Bush alisema kuwa kuna kila sababu ya kumsaidia mwanamke kwa kuwa ndiyo nguzo ya uchumi.

Hata hivyo, katika mkutano huo, mjadala zaidi ulikuwa ni jinsi gani ya kutibu tatizo hilo hilo.

"Hakuna kingine zaidi ya kuokoa maisha na zaidi, hili ni janga kwa wanawake," alisema.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Bush, Doyin Oluwole, alisema Dola 3 milioni (Sh4.8 bilioni) zitatumika katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Alisema,mashine 16 za kuchunguza ugonjwa huo,zitapelekwa katika mikoa mbalimbali huku washiriki wakiahidi kutoa misaada mbalimbali ya hali na mali.

Bush kusaidia mapambano dhidi ya saratani shingo ya kizazi - Siasa - mwananchi.co.tz
 
Nampenda Bush, Mkweli sana, toka ndani ya moyo wake, mengine ni siasa za Marekani.
 
Namfagilia sana huyu rais shinda Obama.
 
Back
Top Bottom