NN: I am definetely not talking of causation here, I am only refering to correlation. That saidi, yes, of course, I am not saying that communication skills and language are the only predictors of intelligence; on the contrary, I am saying that they are one of the strong predictors. FYI I am in line with Gardner's theory of multiple intelligence-in this case I cannot claim that language and communication skills are the only attributes of intelligence, far from it!
JokaKuu: Unakosea sana unaposema kwamba tuhahitaji maendeleo ya uchumi tu, n.k lakini hapohapo unajichanganya unaposema unahitaji "ku-mobilise" forces za kiuchumi-sasa uta-mobilise vipi kama huwezi ku-communicate vision yako sawasawa? Halafu una-miss point muhimu sana, nayo ni kwamba kwa sasa TZ tunahitaji sana an inspiration leader ili kuwahamasisha watu waweze kutumia potential zao kwa kufanya kazi kwa bidii, wajue majukumu yao ni yapi na ya serikali ni yap, etc-yote haya yanahitaji mtu mwenye uwezo wa kuzungumza sawasawa sio uswahili, kuchekacheka, soga, n.k.
Haya sasa huyu jamaa yetu ana miaka mitatu madarakani unaweza kuniambia dira na faslafa yake ya uongozi hasa ni ipi? Inawezekana kabisa anayo lakini hatuijui kwa sababu ya udhaifu wa kujenga hoja na uduni wa uwezo wa kimawasiliano. Mafanikio mengi ya Nyerere yalitokana na uwezo wake wa kuzungumza, kujenga hoja, kushawishi. Vilevile Mkapa aliweza kuwashawishi wazungu kutufutia lundo la madeni na kupata ushirikiano wa ajabu wa kila nchi ya magharibi partly kwa sababu ya uwezo wake wa kimawasiliano.
Sasa swala la EPA,Meremeta, Kiwira, n.k. limewashinda hawa jamaa wa CCM partly kwa sababu hawawezi kuwasiliana wanachokijua na wanachotaka wananchi tujue. Hata kujitetea hawawezi, kila wakinyanyua mdomo ni kuchemsha, kuropoka, kuibua kashfa ingine, partly hii ni kwa sababu viongozi wetu wengi hawana kabisa uwezo wa kuwasiliana.
Ninakwambia hizi issue zote ingekuwa Mkapa ndio yupo madarakani zingeshaisha, angejenga hoja, whether positively or negatively, lakini angelimaliza. Lakini kwa sababu ya uduni wa kimawasiliano wa hawa jamaa zetu waliopo madarakani tumejikuta miaka mitatu ya JK tunaongelea jambo moja tu- ufisadi wa EPA, tumesimama, hatuendi, tumekwama kabisa-lakini ukichunguza kwa makini kwa nini-sio kwa sababu ya EPA, ni kwa sababu ya uwezo mdogo wa viongozi wetu ikiwemo uwezo hafifu wa kujieleza. Kujieleza ni silaha muhimu sana sana kwa uongozi wa kisiasa hasa katika ulimwengu wa demokrasia ambao haukwepeki kabisa kwa sasa.
Don't ever misunderestimate the power of communication skills and language.