Business Advice

Wadau hawajamaa ni matapeli. Kama ukibahatika kukutana nao online achana nao kabisa. Kuwa makini utaliwa
 
jaribu tu mkuu..huwezi jua ndo utatokea hapo kaka...
 
Maoni yangu:
hiyo hela ni ndefu-- kama kuna mizengwe au hakuna huwezi jua, cha maana fuata procedure, tafuta na lawyer wako awepo soma mikataba mnayowekeana, mwombe uthibitisho wa fedha halali, kwasababu wajanja wako wengi, unaweza ukahusishwa na money laundering wakati wewe nia yako ilikuwa kutafuta pesa kihalali kwa jasho la project yako!

Ujanja janja wote weka pembeni-- usiiangalie kwa jicho la pesa ya haraka haraka-- ukaacha procedure za muhimu baadae ukaja kujuta!
kila la kheri
 
imekuaje tena mkuuuu...eeeehhhhh?

jamaa bana nimewaomba udhibitisho wa uwepo wa kampuni (makampuni) yao ila wameshindwa kufanya hivo. Wameishia kunitumia mikataba yao na kunitaka niingize kiasi cha $2,500 kwenye akaunt waliyo nitumia huku wakidai kua ni ya insurence company. Kwakufanya vile wata nitumia huo mkopo kwa muda wa masaa 48.
 

Thanks bro, dili yenyewe ishayeyeka maana wameshindwa kunidhibitishia uwepo wa kampuni zao.
 

Mhh... Kuna kitu kipo katikati ya mlima wa volcano kinaendelea!
Chunga jamaa, usitume pesa yako kama haujathibitisha uwepo wao na wa uhakika! Usicheze kamali ya kutuma $2,500!
GET RICH OR DIE TRYING
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…