Business ideas (Bure)

Sijaona wazo zuri wala la mtaji mdogo yote kawaida tu ila asante ni pm nikuongezee mpya ambazo hukuziwaza wa kuzizania But Asante kwa somo mwenye kuchukua na achukue. Mtanganyika
 
Mtanganyika aksante sana kwa sensitive information of Entrepreneurship ideas!!

Na mimi pia ningependa niwashilikishe Wadau pamoja na wewe mtanganyika;

Mimi nina ndoto ya kusindika kahawa ila changamoto ninazokutana nazo ni hizi hapa

1. Mashine ya kuchomea kahawa na bei yake

2. Utalamu unaowezatumika kusindika na kuweza kuiacha flavour ya kahawa bila kubadilika.

3. Utalatibu unaoweza kutumika kupata mkopo kutoko financial institutions (Banks) ukiwa na shamba la msitu lenye hati miliki.

4. Soko kwangu sio changamoto kubwa sana japo mawazo ni ya mhimu kwa biadhaa hiyo.....

Wadau naombeni msaada wenu kwa mambo hayo!!!
 
Asante
Asante sana mkuu kwa utayari wa ku-share ulichonacho.
 
Ni kipindi ambapo vijana wengi wanatafuta mawazo ya biashara na jinsi ya kuondokana na umasikini na hali ya ufukara, leo nitatoa wazo ambalo linawahusu zaidi vijana wanaopenda matumizi ya mtandao ( Internet). Dunia ya sasa inahamia katika mitandao na vitu vingi vinahamishiwa katika mitandao kama kijana unatakiwa utambue fursa mapema kulingana na mwitikio wa nchi yako.

Biashara nyingi bado haziendani na kasi ya teknolojia hivyo kuna kila sababu ya biashara na bidhaa zinazotaka kuendelea kuhitaji msaada wa utumiaji ama matumizi ya wataalam ama wazoefu wa mtandao kama wewe ni mtaalam ama mzoefu wa mtandao basi usikae ukabweteka kila kitu ni biashara ukikiangalia kwa nje ya box.

Kazi ambayo unaweza kuipata kwa kupitia uzoefu ama uwezo wako wa matumizi ya mtandao ni pamoja na.Kufanya update za Mitandao ya kijamii,tovuti ama blogu, hii ni kazi ambayo inahitaji uelewa ama uzoefu wa coding kwa upande wa website, lakini kwa mitandao ya kijamii na blog ni uwezo wako tu wa ubunifu.

Jinsi ya kuifanya pitia tovuti nyingi uwezavyo kisha orodhesha mapungufu ya hizo tovuti kulingana na muonekano wa nyingine ndani ya soko moja kisha tengeneza ripoti ya kitu unachoweza kufanya na uwezo ulionao pia matokeo ama faida ya kufanya hicho kitu kisha nenda peleka kwa mmiliki wa website kwa barua pepe ama kwa kuonana. Kama ukiwa umeona marekebisho yenye tija atakupa kazi.

Hivyo hii ni kazi ambayo unatakiwa kutumia akili nyingi kuliko nguvu kutambua nia,uwezo,wateja na kadhalika.Vitu vya kuzingatia ni kwamba hakuna muamko mkubwa wa matumizi ya mtandao kwa biashara za kati na chini japo matokeo yanaonekana hivyo unahitaji kuwa makini kupata kile ambacho ni wazo chanya la kazi yako. Pia usiwe na bei ya juu anza chini ila mara nyingi ili mtu aone anakulipa kidogo ila kwa kazi husika,Hii sio kazi ya kufanya kwa sababu umekosa cha kufanya ni kazi ya kufanya sababu moyo wako unapenda mtandao na ni mtumiaji mzuri.

Kama kawaida usilichukue wazo na kukimbia nalo kwa sababu tu nimelitoa na umehisi litakufaa lipime kwanza kama liko sawa na wewe na kisha ndio ulifanyie kazi.Asante.

Pia unaweza kunipata katika mitandao ya kijamii kama

Elisha Chuma ( Facebook,Instagram,Jamii forums)
 
Thanks very much
 
Ndugu zangu Mimi nikijana mwenye umri Wa miaka 30 ,nipo kwenye ajira lakini nataka kujiajili mwenyewe sitaki kuajiriwa kabisa,,sasa Nina kamtaji ka mil 20 ,je wadau naweza fanya biashara gani kwa huo mtaji?, Nina familia inanitegemea sasa sitaki kukosea badae nikaja juta,,,,so please wadau nipeni mawazo yabiashara kwa huo mtaji.
 
kukosea kwenye biashara hakunaga mjanja..

hata bill gate, mengi, dangote huwa wanakoseaga,

biashara haifundishiki ndugu utaliwa hela tu...

fanya kitu unachokipenda na unachokijua kiundani ili hata hasara ikitokea usiumie sana sababu unakipenda.

ukiona huwezi jengea nyumba tu hiyo ndio ina risk ndogo...
 
Biashara za Hustles huziwezi, Nakushauri fanya uwekezaji, Jilipue tu kwa sasa kwa kununua hisa za voda kama you are still too young to handle the risks

N.B Usiache kazi

Watu wanaoweza kuacha kazi na kukaa normal ni wachache
Thanks sana kwa ushauri mkuu
 
Nashukuuru sana kwa ushauri mkuu
 
Thanks sana kwa ushauri mkuu
Au kama hutojali, Partner na mimi, nina wazo bora sana la kipindi cha TV na ninaamini halitakosa wadhamini kama makampuni ya simu na mabenk. uwekeze kwenye wazo langu then, mapato ni 50- 50 ,Win-Win situation

N.B Mimi ndo kwanza nimetoka chuo, sina hata mia
 
Endelea na kazi Kwani kuajiriwa sio dhambi.


Kwa tafsiri lahisi biashara/ujasiriamali ni sawa na mbio za "Nyika". Kadri unavyofanya mazoezi ndivyo unavyozidi kuwa na pumzi. Nakushauri ufungue biashara yako iwe ni sehemu ya kukuongezea kipato kwa kazi unayofanya.

Huu sio muda muafaka wa kuacha kazi na kufanya biashara sababu.
1. Uwezo wa watu kufanya manunuzi umepungua
2. Uhaba wa chakula umesababisha mfumko wa bei (Labda uanze na biashara ya nafasi).
3. Serikali haitabiriki. Serikali imekuwa ni ya matamko badala ya sheria, kanuni na taratibu kutamalaki. Mfano wazi ni wafanyabiashara wa "viroba" jinsi walivyotendewa.
 
Kuna wakati unaweza kufanya kitu kikakupa adhabu badala ya faida unayo tegemea kuipata

1.usiache kazi kwa kutegemea biashara ya kwenda kujifunza kuifanya
2. Angalia kitu unacho weza kukifanya kama uwekezaji katika mtaji mdogo na utapaswa kuajiri mtu wa kusimamia hii itakuongezea kupata uzoefu wa biashara au uwekezaji utakao kuwa umewekeza
3. Kupata hasara ni sehemu ya fundisho linalo patikana ndani ya biashara na ndo hukupa mwelekeo halisi wa kujua wapi umekosea wapi ulipatia upaongezee mkazo

Ukisha pata uzoefu ndo utapata mwelekeo wa kujua uache kazi au laa
 
Nashukuru sana mkuu
 
Nashukuru sana
 
OK. Hebu nipm tujuzane zaid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…