Business partner anatafutwa (Project ya maji safi Ubungo)

Business partner anatafutwa (Project ya maji safi Ubungo)

shaurimbaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
1,915
Reaction score
2,329
Habari wadau.

Business partner anatafutwa (Project ya maji safi Ubungo)

Mi ni kijana (me) 28yrs, graduate, mjasiriamali na mwajiriwa pia.

Natafuta mtu, Taasisi au Kampuni ya kushirikiana nayo Project ya maji safi Ubungo external.

Nimepata hili wazo baada ya kufanya feasibility study na Swot analysis katika eneo linalonizunguka.

Project hii itafuata vibali vyote halali na taratibu zote zinazotambulika kisheria na kiafya.

Cost za project hii za uwekezaji nimezigawa katika pande kuu mbili.. CAPEX na OPEX ambazo tutashirikina kama partners na tutashare profit and loss of the project 50/50 kama partners.

Binafsi kwenye capital expenditure natoa eneo la mradi, water source ambayo ni kisima drilled 80m nilichokichimba june 2015,, chenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita elfu 10 kwa siku za maji chumvi, umeme wa mradi luku inayojitegemea na usimamizi wowote utakahitajika.

Partner upande wake yeye atatoa utaalamu wake wa kusimamia mradi, ku treat maji kuyaondoa chumvi kwa njia atakayoichagua yeye kama ni kufunga oxidizer filter, aeration, reverse osmosis,water softerner, soda ash injection system,,neutralizing filter, iron remover au njia yoyote ta halali inayotambulika kiafya na kiusalama.

Targeted customer wa hii project ni magari ya kuuza maji ( water bowser), wafanyabiashara mabibo hostel, wauza maji kwa mikokoteni, majirani, car washes na wengineo..

Nina imani project itakuwa successful sana kwa kuangalia shida ya maji na mahitaji yaliyopo hili eneo.

SWOT analysis niliyoifanya.

Strength yetu kubwa ipo kwenye location yenye mahitaji kubwa ya maji kuliko supply za uhakika na availability of water aquifer zenye maji mengi wenye hii water well especially wafanyabiashara wa mabibo hostel na magari ya kuuzia maji na majirani.

Weakness ipo kwenye poor technical knowledge on how to treat water kwa unafuu zaidi, Water project management experience, umeme wa tanesco sio wa uhakika..

Opportunities ya kufanikiwa ipo sana n asana maana ni eneo lenye watu wengi sana na sana wateja w haya maji tutakayozalisha daily bila kusahau hotelz na wafugaji wanaoteseka na maji chumvi tu,, maana eneo hili ni maji chumvi tu kwa wenye visima.

Threat kubwa ya huu mradi ni serikali ikifanikiwa kutatua tatizo la maji dar es salaam nzima. Ikitokea muujia serikali iwe inatoa maji 24/7 a day milele kiasi kwamba kila mtu anakuwa na bomba lake kila sehem ambalo halikatiki siku zote.. hapo ni threat kweli kwa biashara japokuwa huu ni muujiza mkubwa sana kwa serikali za Africa kufanya hivyo.

Mtu, Taasisi, Kampuni iliyo interested kushirikiana nami katika hii project inakaribishwa initafute.. nayo ifanye feasibility study yao kwa huu mradi ikiwezekana tushauriane na kushirikiana katika hii project. Namba yangu ni 0658 000106

Nilipanga niifanye mwenyewe yote peke yangu kilichonibana hela zote kwa mara moja peke yangu itanichukua muda mrefu sana kukamilisha peke yangu.

Ninakaribisha pia mawazo ya watu wengine ili ndoto yangu itimie kwa kutengeneza hela huku nikiisaidia jamii pia kupunguza changamoto ya maji kupatikana 24/7 eneo la ubungo na maeneo mengine jirani

The Boss, lara 1, Malila, Mtambuzi, Khantwe, misschaga, na wengine wote mnakaribishwa sana mawazo yenu na kushiriki mradi huu yoyote anaeweza
 
Last edited by a moderator:
Lita moja ya maji ni shilingi ngapi? (bei ya jumla). Unaweza kuuza lita ngapi kwa siku?
 
Lita moja ya maji ni shilingi ngapi? (bei ya jumla). Unaweza kuuza lita ngapi kwa siku?

kwa wastani ndoo ya maji safi lita 20 ipo around 300 hadi 500,,, mimi kwa wazo langu nina imani shilingi 200 itatulipa sana na sana as my goal ni kuzalisha n kuuza maji mengi sana per day.. kwa siku kwa wastani tutauza lita elfu 15 hadi elfu 20 kutegemea na mvua kunyesha au dawasco kutoa maji
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Okay.

Kwa hiyo ni kama sh 10 kwa lita. Kwa siku revenue sh 150,000 ambayo kama mtambo una operate at 90% kwa mwaka ni kama sh 50m. Gaharama za uendeshaji (opex) zinaweza kuwa kama sh 20m kwa mwaka (wastani wa kama sh 50,000 kwa siku). Gharama za uwekezaji inaweza kuwa another sh 5m kwa mwaka.

Kwa hivyo, kunaweza kuwa na faida ya sh 25m kwa mwaka ambayo ikitozwa kodi ya 30% (sh 8m kwa mwaka) itaacha faida inayoweza kugawanywa ya sh 17m (sawa na wastani wa kama sh 45,000 kwa siku na mkigawana kila partner atalamba sh 22,500 kwa siku karibia 675,000 kwa mwezi). Kama mahesabu haya yapo sawa, ni mradi mzuri tu ingawa mtatakiwa muwe na miradi ya ziada au vyanzo vingine vya mapato ili kuweza kukidhi changamoto za maisha ya hapa Dar. Ni mradi mzuri pia kwa sababu hauna changamoto nyingi ukilinganisha na miradi mingine (kama ya kuku, kilimo nk).
 
inshort nina vyanzo vingine vya kupata hela ya kula.. nina ndoto tele.. natafuta mpiganaji mwenzangu tuwekeze kwenye maji sfi na salama tufaidike huku jamii pia inafaidika...
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Wadau karibuni sana kwa mswali na ushauri pia jinsi ya kufanikisha hii project
 
Sory mkuu may be we ar interesting lkn unaweza kuchange jina lako(avater name) hilo ili tuweze kukuamini
 
Partner upande wake yeye atatoa utaalamu wake wa kusimamia mradi, ku treat maji kuyaondoa chumvi kwa njia atakayoichagua yeye kama ni kufunga oxidizer filter, aeration, reverse osmosis,water softerner, soda ash injection system,,neutralizing filter, iron remover au njia yoyote ta halali inayotambulika kiafya na kiusalama.

Hapo kwenye lugha ya kitaalamu ndipo ninapohisi utanipiga changa la macho iwapo nitaamua kuwekeza, mimi sipatani na Kiingereza kwa kweli, na hizi lugha ndizo wanazitumia wawekezaji wakija nchini na kutupiga za uso.......
 
Kwa makadirio partner aje na mtaji kama wa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom