Mimi Niko mbeya na biashara zipo za aina nyingi na zinalipa Ila naomba mtambue biashara Kubwa mbeya na maeneo yanayozunguka ni kilimo. Kwa asilimia Kubwa wakazi wa mbeya Hata kama ana shughuli nyingine mfano ameajiriwa lazima atajishughulisha na kilimo pia. Sasa tukisema kilimo ni kipana, kuna Kulima kwa kupanda na kuvuna, kuuza pembejeo za aina mbalimbali, kuna shughuli za mashine za kilimo kama Kulima mashamba ya watu kwa kutumia trekta au kubota na wao kukulipa kwa ekari ulizowalimia, kuna kununua Mazao kipindi cha kuvuna bei akiwa chini na kuifadhi Mpaka kipindi bei Zimepanda unauza nk.
Biashara zingine zote zinategemea kilimo na misimu yake. Kwa wale wanaotaka kuja mbeya na kufanya biashara karibuni tubadilishane mawazo kutokana na uzoefu tulionao.