Pre GE2025 BUSOKELO: Kanisa la TAG Latoa Tuzo kwa Mbunge Mwakibete Kutambua Kazi Inayofanyika Jimboni Busokelo

Pre GE2025 BUSOKELO: Kanisa la TAG Latoa Tuzo kwa Mbunge Mwakibete Kutambua Kazi Inayofanyika Jimboni Busokelo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

BUSOKELO: Kanisa la TAG Latoa Tuzo kwa Mbunge Mwakibete Kutambua Kazi Inayofanyika Jimboni Busokelo

KANISA LATAMBUA KAZI ZA MBUNGE MWAKIBETE, AKABIDHIWA TUZO IBADA YA MWAKA MPYA 2025

Katika Ibada ya Mwaka Mpya Iliyofanyika Katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God JCC Lwangwa imetambua kazi zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo la Busokelo Mheshimiwa Atupele Fredy Mwakibete na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Ibada hiyo iliyoongozwa na Mchungaji Kelvin Kwileka imefanya maombi maalum kwa viongozi akiwemo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dkt. Phillip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Busokelo Atupele Fredy Mwakibete, kisha kukabidhi tuzo kama ishara ya kutambua kazi iliyotukuka na inayoonekana jimboni inayofanywa na viongozi hao.

Aidha Katika Ibada Hiyo Mheshimiwa Mwakibete amelishukuru Kanisa kwa maombi hayo pamoja na tuzo ya kutambua kazi inayofanywa na serikali ya awamu ya sita, pia ameweza kuchangia ujenzi wa ofisi ya mchungaji unaondelea kwa pesa Taslimu Shilingi Milioni Moja na Tripu Tano za Mchanga.

Screenshot 2025-01-03 at 11-13-27 Instagram.png
Screenshot 2025-01-03 at 11-13-32 Instagram.png
 
Tundu alisema Maaskofu huwa wana 'pigwa' na mamilioni toka kwa Samia.
Mwakibete ana ukwasi wa kutumia hao wachungaji kuwa imanishe yeye kashushwa na Yesu 😡
 
Hilo kanisa la TAG tukisema limeanza kujiingiza kwenye abrakadabra za kisiasa msitokwe povu
 
We jamaa unayejiita jesus is comming again huwa unatokwa povu TAG ikisemwa kuachana na imani na kufuata matakwa yake ya kibinadamu tu. hapa utadai ushahidi gani? jionee mwenyewe
 
Haya makanisa sasa yanaanza kuvuka mipaka na kumdhihaki mwenyezi mungu.
Binafsi hii sikubaliani na hii tuzo.
 
Back
Top Bottom