GE2025 Bussungu: Nitanunua ndege za doria kila mkoa kuimarisha usalama wa Taifa

GE2025 Bussungu: Nitanunua ndege za doria kila mkoa kuimarisha usalama wa Taifa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mgombea urais wa Chama cha ADA-TADEA, Georges Bussungu, ameahidi kuiimarisha Idara ya Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi kwa kununua ndege maalumu za doria katika kila mkoa endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.

Akizungumza leo na wananchi wa Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, katika mwendelezo wa kampeni zake, Bussungu alisema taifa linakabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama ikiwemo ujambazi, usafirishaji wa dawa za kulevya, ujangili, uhalifu wa mipakani na vitendo vya utekaji, hivyo kuna umuhimu wa kutumia teknolojia ya kisasa ya anga kudhibiti uhalifu.

“Kila mkoa utapewa ndege maalum ya doria — si ya abiria bali yenye teknolojia ya kisasa ya kufuatilia maeneo kwa haraka. Polisi wetu hawatatembea tena kwa miguu au pikipiki kuwafuata majambazi porini au kufuatilia uhalifu wa usiku,” alisema Bussungu.

Ameongeza kuwa nchi haiwezi kuwa salama iwapo itaendelea kutumia mbinu za zamani za ulinzi, wakati wahalifu wanatumia teknolojia ya kisasa kufanya uhalifu. Kwa sababu hiyo, amesema atafanya mageuzi makubwa ndani ya Jeshi la Polisi kwa kufuta kitengo cha Upelelezi (CID) na kuanzisha kikosi maalumu cha kitaalamu cha upelelezi, kama ilivyo katika baadhi ya nchi zilizoendelea.

Bussungu alisisitiza kuwa Tanzania ni nchi kubwa, hivyo haiwezi kusubiri wahalifu wachukue hatua ndipo vyombo vya ulinzi viitwe. Amesema ndege hizo zitawawezesha polisi kufuatilia harakati za kihalifu kwa wakati halisi, kudhibiti mipaka, miji na vijiji kwa ufanisi mkubwa.
1761216174747.png
 
Chama cha Wanyamapori ndege za kusaka majangili?
 
Huyo ndio anachuana vikali na Kwa ukaribu zaidi na chama tawala yaani ana ushawishi mkubwa sana ikitokea chama tawala kikashinda kitakua kimepambana sana
 
Naye Bwege kama mabwege wengine

Binadamu anapoomba dhamana kitu pekee kinanachomlinda ni moyo wake unaoruhusu wengine kuwa sehemu ya nafsi yake, kwakuwa wanamhisi

Ndipo wanapokuwa walinzi Pasi na ujira, wanapokuwa macho ya uso wake na vidole vya mikono yake wanapobeba dhamana ya udhaifu wake Pasi na ujira

Ni MPUMBAVU kwakuwa anadhani ana mfumo Wa kuongoza watu wenye akili
 
Back
Top Bottom