Buswita kafungiwa kwa matakwa ya nani?

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,804
Reaction score
10,715
Mwaka wa jana bodi ya ligi iliwatia kitanzini Kaseke na Chirwa kwa lengo la kusaidia klabu mojawapo lalamishi kutwaa ubingwa. Jaribio hill lilifeli. Msimu huu kijana machachari awapo uwanjani Buswita amefungiwa mwaka mmoja na TFF katika mazingira ya kutia shaka. Hebu soma makala hii kama ilivyo andikwa na Anjetile Osia. It is an eye opener.

BUSWITA ANA ADHABU YA KIPEKEE DUNIANI. INASHANGAZA!
 
Hiyo ndio kabumbu wakati Nchi nyingine zikicheza mpira sisi tz tunacheza kabumbu
 
Mtoa mada analengo la kupotosha kwa makusudi.

1.Hivi ni kweli hajui kuwa TMS na mkataba ni vitu viwili tofuati na vyote vina utaratibu wa kuvingoza tofautitofauti?
2.Hivi wakati Yanga inaadhibiwa kwa kumsajili Hassan Kessy huku akiwa ndani ya mkataba na klabu nyingine hajui kuwa Kessy alikuwa kwenye 'TMS' moja tu ya Yanga?

3. Ni kweli Angetile hajui maana ya mkataba, binding yake na impact ya ukiukwaji?
4. Ana tatizo na kanuni yenyewe? ukubwa wa kifungo, au tasfiri iliyolepelekea uamuzi wa kumfungia?
5. Alikuwa wapi mwaka jana wakati William Lucian na Saidi Mkopi wanafungiwa na kosa hilihili la Pius Buswita? Mbona hakuandika makala, mbona hakuchambua kanuni?
 
Ndo tatzo la ktokjua sheria sio kila ktu ukiona mpmbavu kaandka kwa ushabiki maandzi na ww uandke
 
Mkuu, nadhani kuna mahali hujaelewa kilichosemwa.

1. TMS ndiyo mfumo unaohakikisha mchezaji anasajiliwa pahala pamoja tu. Baada ya kusaini mikataba ya awali, majina huingizwa kwenye TMS kufuatia mkataba wa awali. Sasa Buswita ana mkataba na Yanga pekee pale TFF, Simba hawakupeleka jina lake kwenye kikosi chao.

2. Umesema vema, wakati Yanga inaadhibiwa. Tofauti hapa Buswita ndio anaadhibiwa. Pia Osiah anajaribu kuonesha kuwa kumfungia mchezaji mwaka ni kuua kipaji, na hii imepitwa na wakati.

3. Anjentile hata kama anajua mkataba, hoja hapa haukuwakilishwa TFF. Na kama ungewakilishwa kukawa na mikataba miwili, uliosainiwa mwanzo unngekuwa valid (kwa Jinsi nilivyomwelewa) na angetakiwa kulipa fidia kwa ule wa pili.

4. Hoja yake Ni tafsiri ya kanuni na aina ya adhabu, sio kubwa. Amegusia kuwa makosa haya anaadhibiwa kwa tozo sio kifungo.
 
Huyo mchezaji mpumbavu, full stop
 
Ndo tatzo la ktokjua sheria sio kila ktu ukiona mpmbavu kaandka kwa ushabiki maandzi na ww uandke
Sasa wewe unayejua sheria umesema nini hapa. Wewe ndio unaleta ushabiki wa kipumbavu. Soma hoja uelewe.
 
Mwanzisha mada siyo mwanamichezo bali msomaji wa magazeti mzuri.
 
Hakuna haja ya kumtetea mchezaji mjinga.
 
Basi tufanye hivi.

Buswita ni mchezaji halali wa Yanga fc.
Buswita katumia mbinu ovu kuiba pesa ya Simba sc.

Na kwakuwa Simba ni mwanachama wa TFF, Chama hiki cha Soka kimekasirishwa na tabia ya baadhi ya wachezaji wa mpira wa miguu kuwaibia wanachama wake.

Hivyo kikaamua kumfungia Buswita kucheza mpira kwa muda wa mwaka mmoja kama adhabu ya wizi wa fedha ya mwanachama wake Simba sc.

Buswita ni tapeli na mwizi wa fedha za Simba sc.

Anastahili kufungwa jera miaka saba kwa kitendo cha kukiri kuwa kaiba fedha za Simba sc. Kitendo cha kumfungia kucheza mpira huyo mwaka mmoja ni cha nafuu kwake.

Ikae hivyo.
 
Hahaha kwa matakwa ya sheria ya shirikisho la mpira wa miguu tanzania (TFF)
Kokote duniani mchezaji haruhusiwi kusajiliwa timu mbili au zaidi.
Pius busitwa kakosea!
 
Lakini pia mleta mada naona umekuja kwa utimu sio kujadili kwa ajili ya mafanikio ya mpira wetu nchini.
Je asingekua kasajili simba ingekua azamu vs Yanga ungetoa povu gani kwa upande wa pili???
Muache utimu kwe kujadili mambo ya msingi.
 

Issue ya Kessy ni tofauti na hii Kessy alikuwa ni mchezaji wa Simba na mkataba wake ulikuwa ukingoni sheria zilikuwa zinamruhusu kufanya mazungumzo na timu nyingine,kosa la Yanga ilikuwa ni kumsainisha mkataba kabla ya mkataba wake na Simba haujaisha bila kukubaliana na Simba na ile issue imesaidia msimu huu licha ya kujulikana kwamba Simba inawasajili Manula na Niyonzima lakini ilibidi Simba wasubiri mpaka tarehe ya mikataba yao kwisha ndio watangaze wamewasajili pia uliona ilibidi Yanga wakubaliane na Azam kwanza kabla ya kumsajili Gadiel Michael

Buswita alikuwa mchezaji wa Mbao FC na inasemekana kuwa amesajiliwa na Simba na Yanga lakini Yanga ndio walipeleka usajili wake TFF Simba hawakupeleka,kama Buswita alichukua fedha za Simba adhabu inapaswa yeye kurudisha fedha alizochukua ikiwezekana na riba lakini sio kumfungia kucheza soka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…