Mpita Njia wa gazeti la Mtanzania la tarehe 4/12/2009 naye akasema yake kwenye kichwa cha habari "
Mwalimu Nyerere Foundation!"
Kwa muda sasa Mpita Njia (MN) amekuwa akifuatilia kauli zinazotoka ndani ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere Foundation). Katibu Mtendaji wa MNF, Joseph Butiku amekuwa akishutumu uwapo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mtu akimwangalia Butiku kwenye luninga wakati anapinga mitandao ndani ya vyama anaweza akasema Mungu weee, mtu si huyu! Kama ana ng'ombe au mwanambuzi anaweza kuuza ampelekee zawadi. Atamwona mzee huyu aliyepata fursa ya kufanyakazi karibu na Mwalimu Nyerere ni mkombozi wa kweli.
HUKU KUPANUKA KWA WIGO WA DEMOKRASIA NAONA KUNALETA MATATIZO KIDOGO. LUGHA ILIYOTUMIWA HAPA NA MPITA NJIA NI LUGHA YA KEJELI. BILA SHAKA MWANDISHI WA MAKALA HII YA MPITA NJIA ANAWEZA AKAWA NA UMRI MDOGO KULIKO HUYU MZEE ANAYEMBEZA KWA KEJELI. HUU NI MFANO DHAHIRI WA MMOMONYOKO WA MAADILI.
Lakini sikia. Kumbe mzee huyu ni chui aliyevaa ngozi ya kondoo. Inawezekana kama si hivyo, basi hajui maana halisi ya neno mtandao. MN anajiuliza hivi huyu mzee mwaka 2005 wakati anazunguka nchi nzima kumwombea kura Dk. Salim Ahmed Salim alikuwa anafanya nini?
Tena wapo wanaosema alizunguka kwa kutumia kasma ya Taasisi ya Mwalimu Nyeree. Hakuna asiyejua juhudi kubwa alizofanya kumwingiza madarakani Dk. Salim. Tena MN alikuwa akipita mahala akakuta Butiku akijadiliana na wakubwa wenzie nani anafaa kuwa Rais
Butiku alikuwa akizungumzia uzoefu, si ujuzi wala weledi, bali akisema anayefaa kuwa Rais wa nchi hii ni Dk. Salim, Hapa tunapoelekea ni uchaguzi wa mwakani. Butiku yeye alikuwa na matandao wake mwaka 2005, sasa hajatueleza kama aliuvunja au ulikufa wenyewe baada ya mtu wake kushindwa akaweweseka au vipi?
MIMI NI MSTAAFU NA NAIELEWA HISTORIA YA TAASISI YA MWALIMU NYERERE. NAELEWA HAYA YALIYOSEMWA HAPA NI UZUSHI WA WAZI KABISA.
TANGU MWALIMU NYERERE AKIWA BADO YU HAI, TAASISI YA MWALIMU NYERERE ILIKUWA NA ZOEZI LA KUTAFUTA MICHANGO KWA AJILI YA KUPATA FEDHA ZA KUENDESHA TAASISI. HAKUNA ASIYEELEWA KWAMBA MWALIMU ALIPOKUWA MADARAKANI HAKUTUMIA NAFASI YAKE YA UONGOZI KUJINUFAISHA WALA KUJILIMBIKIZIA MALI. KWA HIYO NI WAZI ALIPOTOKA MADARAKANI ALIKUWA HANA FEDHA ZOZOTE ZA KUWEZA KUANZISHA NA KUENDESHEA TAASISI. LAKINI, ALIAMINI KWA DHATI KABISA KWAMBA WANANCHI NA WATU WENGINE WENYE NIA NJEMA WANGELIWEZA KUICHANGIA TAASISI.
BAADA YA MWALIMU KUFARIKI DUNIA BADO TAASISI ILIKUWA BADO HAINA FEDHA ZA KUTOSHA KUWEZA KUJIENDESHA YENYEWE, KWA HIYO KAZI YA KUTAFUTA MICHANGO ILIENDELEA HADI MWAKA HUO WA 2005 BUTIKU ALIKUWA ANAENDELEA NA ZOEZI LA KUTAFUTA MICHANGO KUTOKA KWA WANANCHI. KADI ZA MAOMBI YA MICHANGO KWA AJILI YA TAASISI ZILIPELEKWA HADI KWENYE KATA KWA AJILI HIYO.
HATA HIVYO ZOEZI HILO LILISITISHWA NAAMINI KWA NIA NJEMA BAADA YA KUONEKANA LINAWEZA KUINGILIA MCHAKATO WA KUTAFUTA MGOMBEA URAIS.
INAVYOELEKEA WAZUSHI TAYARI WALIKUWA WAMEISHACHUKULIA ZOEZI HILO KAMA NI KAZI YA TAASISI KUMPIGIA DEBE ‘MGOMBEA' WAKE!
NINAWEZA KUSEMA KWA UHAKIKA KABISA NA BILA KUUMA MANENO KWAMBA KAMPENI ZA SALIM ZA KUTAFUTA KUCHAGULIWA KUWA MGOMBEA WA URAIS HAZIKUHUSIANA HATA KIDOGO AMA KWA NJIA YOYOTE ILE NA TAASISI YA MWALIMU NYERERE AMA UONGOZI WA TAASISI HIYO.
PENGINE KUTOKANA NA KUPOROMOKA KWA MAADILI WATU WANASHINDWA KABISA KUPAMBANUA NA KUELEWA UADILIFU WALIONAO BAADHI YA VIONGOZI WA SASA NA WALE WALIOKUWA VIONGOZI WA NCHI HII HUKO NYUMA. DK. SALIM KWA UADILIFU WAKE ASINGELIWEZA AKACHEZA MCHEZO MCHAFU WA KUITUMIA TAASISI KATIKA KAMPENI ZAKE. NA NAAMINI HATA NDUGU BUTIKU MWENYEWE ASINGELIKUBALI TAASISI ITUMIKE KWA AJILI HIYO.
KUTOKANA NA NILIYOYAELEZA HAPO JUU SI KWELI KWAMBA BUTIKU ALIKUWA NA MTANDAO KWA AJILI YA DK. SALIM. KWA HIYO SUALA LA YEYE KUUVUNJA MTANDAO HUO HALIPO! NI UZUSHI USIO NA MAANA YOYOTE.
Ila kubwa lililomsukuma MN kumgusa mzee huyu, ni tabia yake iliyoibuka. Tabia hii inakuwa na isipokemewa ataipeleka nchi pabaya. Mzee huyu ameamua kufumba macho ingawa hana upofu. Haelekei kusifia hata neno alilolitenda Rais Jakaya Kikwete.
KWA MIAKA YANGU NA KUPENDA KUSOMA HABARI NIMEKUWA MSOMAJI MZURI WA GAZETI LA MTANZANIA ENZI ZA JENERALI ULIMWENGU NA AKINA BWIRE WAKIWA PALE HABARI CORPORATION. KIBONZO CHA MPITA NJIA KILIKUWA KINAHABARISHA KINAELIMISHA NA KINAKOSOA KWA LUGHA YA KISTAARABU SANA NA KUWAHESHIMU WASOMAJI. INASIKITISHA SANA KUONA JINSI AMBAVYO MPITA NJIA HUYU WA SASA ANAVYOWEZA KUTUMIA LUGHA ISIYOHESHIMU WASOMAJI WAKE!
Anataka kuwaaminisha wananchi kuwa uongozi wa Rais Kikwete umeshindwa kazi. Kila kukicha anakaririwa akilalamika tu. Hawezi kumsifia Rais hata kwa hatua alizochukua kupanua wigo wa demokrasia nchini. Hata malalamiko anayotoa akaendelea kuishi uraiani bila kubughudhiwa anapaswa kufahamu kuwa ni kazi ya Rais Kikwete.
KUSEMA KWAMBA KILA KUKICHA BUTIKU ANALALAMIKA NA KUTAKA KUWAAMINISHA WANANCHI KUWA UONGOZI WA RAIS KIKWETE UMESHINDWA KAZI, NI UCHOCHEZI NA UCHONGANISHI USIO NA TIJA. HIVI HUYU BUTIKU YEYE HANA KAZI, KILA KUKICHA KAZI YAKE NI KULALAMIKIA UONGOZI WA RAIS KIKWETE? HAPA ANAYESTAHILI KUCHUKULIWA HATUA NA KUBUGHUDHIWA NI MWANDISHI WA MPITA NJIA KWA KUJARIBU KULETA UCHONGANISHI KATI YA WANANCHI NA RAIS/WANANCHI WENGINE.
Sasa Mzee huyu MN anampa ushauri wa bure. MN anamwambia kuwa haiwezekani hata siku moja wapiga kura wakaamka na kwenda kwenye vituo vya kura bila kushawihiwa wampigie nani kura. Si hilo tu, hata chama alichomo yeye kitendo cha yeye kukata kadi ya uanachama tayari ni mtandao.
HAYA PIA NI MANENO YA KEJELI NA DHARAU KWA WANANCHI KWAMBA WAO NI MAMBUMBUMBU HAWAJUI TOFAUTI KATI YA MTANDAO UNAOZUNGUMZIWA NA MTANDAO WA KICHAMA!
Ifahamike kuwa kama taifa hatuwezi kurejea kwenye enzi za ujima. Enzi ambazo si baba, mama wala au mtoto aliyejua ndugu kala nini, kalala wapi, hakukuwapo uchaguzi wala kugombea uongozi. Enzi hizo zilifutika. Ndiyo maana tuna vyama vya siasa. Vyama hivi ni mitandao.
HEY! UMEZALIWA LINI ‘MPITA NJIA' WA SIKU HIZI?! ENZI ZA UJIMA BABA, MAMA, MTOTO, MJOMBA, SHANGAZI, NDUGU WA KARIBU NA WA MBALI NA HATA JIRANI WALIJUANA VYEMA NA KILA MMOJA ALIJUA MWENZIWE KALA NINI NA KALALA WAPI. WENZETU WA KABILA LA WANYATURU NA WAGOGO TANGU ENZI ZA UJIMA WANA SALAMU YAO YA KILA ASUBUHI YA KUULIZANA 'UMEKULA NINI?! TOFAUTI NA ILIVYO SASA AMBAPO ‘MWENYE SHIBE HAMJUI MWENYE NJAA'!
MN anatakiwa kumwelimisha mzee huyu kuwa maana ya vyama ni kikundi cha watu waliokubaliana kiamwazo, kiitikadi na wana ajend ainayofanana kwa nia ya kuliletea taifa lake maendeleo. Kinachotokea sasa, wapo wenye kujiona kama si wana-mtandao, na hivyo u-CCM wao haukamiliki vizuri, hivyo lazima wasisemee hili. Si kweli!
HIVI KWELI MPITA NJIA YUKO SERIOUS ANAONA ANAO UBAVU WA KUMWELIMISHA MZEE BUTIKU MAANA YA VYAMA NI NINI? MATUNDA YA UTANUZI WA WIGO WA DEMOKRASIA NI MATAMU KWELI.
WATANZANIA TUMSHUKURU RAIS KIKWETE KWA KUPANUA WIGO WA DEMOKRASIA LAKINI ASLANI TUSIUTUMIE VIBAYA NA KUHATARISHA KILE TUNACHOKIFAIDI. TUPINGANE KWA HOJA LAKINI TUENDELEE KUISHI KWA UPENDO KAMA WATANZANIA, TUHESHIMIANE NA KUJENGA/KUENDELEZA MAADILI MEMA YA TAIFA LETU ILI TUWEZE KUENDELEA KUISHI KWA AMANI NA UTULIVU KWA MANUFAA YETU SASA NA MANUFAA YA VIZAZI VIJAVYO.
Bibi Ntilie/Mama Ntilie Mstaafu!