Butiku na wenzake ni 'wahaini'

Siyo aliwekwa ndani. Alishtakiwa huyo yeye na marehemu mdogo wake akiitwa John ambaye alikuwa Trade Unionist. Hao wawili kwa sababu wana ujamaa na Oscar Kambona, Kambona recruited them. Huyu alipokamatwa alikuwa Captain Dan Lifa Chipaka. Kwa hiyo alishtakiwa na kesi ikasikilizwa na akafungwa kama sikosei. Walimtuhumu Nyerere na walikuwa wakimwita "Mchonga meno". Wakati wa kesi he was quite outspoken. Walitaka kumpindua Nyerere kwa sababu nchi wakati huo ilikuwa chini ya utawala wa udikteta wa chama kimoja.Mahakama iliwapata na makosa na akafungwa. Kwa hiyo anamposema Butiku inaeleweka kuwa kapata sababu ya kumcharaza. Kwani Butiku 2005 si alikuwa anamuunga mkono Salim. Sasa na yeye kapata sababu ya kumcharaza JK. Hiyo ndiyo si hasa (Siasa).
 

Sikutegemea Chipaka atumie neno "uhaini" kirahisi rahisi namna hii! Katika watu wote yeye alitakiwa kujua athari zake.

Amandla........
 

Sidhani kwamba Muungwana anajali sana kwa kuwa anao watu wa kumsemea!

Jana nilimsikiliza Agustino Lyatonga Mrema Mwenyekiti wa Chama cha Upinzani cha TLP akihojiwa na Mlimani TV. Akiulizwa kuhusu nia yake ya kutaka kugombe ubunge na akakiri kwamba ameamua kufanya hivyo ili awatumikie wana'nji'. Hilo sikuliona bizzare sana lakini sikuamini masikio yangu nilipomsikia anamfagilia Rais Kikwete na kuwashutumu wale walioongea kwenye Kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuelezea mapungufu wanayoyaona katika utendaji wa Rais, serikali na Chama tawala. Hvi hapo atakapokwenda jukwaani kujinadi kwa wananchi bila shaka ataendelea kufagia-fagia tu!

Jamani njaa haina heshima wala utu!

Nilipochoka kusikiliza ya Mrema nikahamia ITV nione kulikoni? Nikakuta mjadala wa jopo la watu wanne - Prof Mushi wa REDET, Mzee Mbawala (sikumbuki wa wapi) Mbunge Beatrice Shelukindo na Mbunge Ole Sendeka. Huko nako hakukuwa na jipya ni kwamba wanaodai/wanaotaka Rais achukue maamuzi magumu tayari alifanya hivyo kwa kukubali kustaafu kwa Lowassa na kuwafikisha watu mahakamani wakiwemo mawaziri - mambo magumu ambayo hayajawahi kufanywa na Rais yeyote. Vijembe vikapigwa kwamba waliokuwa kwenye (controversial) Kongamano wao nao walikuwa kwenye nafasi za uongozi mbona hawakuwahi kufanya hayo?! Prof. Mushi akasema hivi sasa demokrasia imepanuka sana kuliko huko nyuma, hayo ni mafanikio makubwa.... etc etc.

Conclusion ni kwamba Muungwana is just doing fine!
 
Maneno yako yamejaa hekima tupu. Haya mambo ya mtandao haya yanaharibu tu Taifa. Yamejaza watu kibao ndani ya nafasi za uongozi wasiojua wanachofanya.
Kweli JK hana mdomo wa kusema mpaka hawa jamaa waliojichokea waanze kumsemea? Sometimes I wonder who is the man/woman behind all these failing strategies? No doubt, these kind of strategies will fail whether its me implementing them or any other person because they don't hold any political truth,maturity or seriousness.
 
Guess what? Yangekwa madheebu mengine hususan Wakatoliki kelele zingekuwa nyingi wakina Makwaia wangeitisha midaalo ari mradi. Poor catholics!
 


Mkuu hapo naona limeeleweka ,waliosema ni wengi,ndio maana kwenye utaratibu wake wa kuongea na wananchi siku moja mh.Rais alisema kwamba wakubwa wajifunze kuongea mbele za wananchi maana kauli zao hazifanani na mtu wa kawaida.wazuie nguvu zao kuongea ikibidi wazielekeze kwenye mambo yenye tija.
 
JK wanataka kumsafisha, na huku Lowassa nae anahitaji kusafishwa....kaazi kweli, kweli. Wanajiachiaje mpaka wanachafuka hivo, kiasi cha kwamba iwe ni kazi ya watu wengine kuwasafisha?
Rais wetu sasa inabidi asuguliwe na JIKI ili awe squeaky clean
 
Inasikitisha kuona kumbe CCM ina nyama mjomba vya upinzani. Pamoja na hayo maandamano, jana on ITV, mama Shelukindo, Ole Sendeka na wengine walikua wanatetea JK. I just turned off the TV baada ya kusikia kwamba tusimulaumu, afanya maamuzi peke yake, ana washauri... Pumba. Kwani tulipigia kura washauri wake? Kwanza tunawajua?
Ninachofurahia ni mwamko tulionao. Leo hatudanganyiki
 
Wana JF, kabla ya kwenda mbali sana ni vyema tukawaangalia hawa watoa hoja. Kwanza ni wenyeviti wa vyama ambavyo havina wanachama.Pili wamechoka. Ingekuwa hoja huu imetolewa na vyama makini (Chadema, NCCR, TLP, n.k) ningeona sababu ya kuijadili.
 
Mpita Njia wa gazeti la Mtanzania la tarehe 4/12/2009 naye akasema yake kwenye kichwa cha habari "Mwalimu Nyerere Foundation!"


HUKU KUPANUKA KWA WIGO WA DEMOKRASIA NAONA KUNALETA MATATIZO KIDOGO. LUGHA ILIYOTUMIWA HAPA NA MPITA NJIA NI LUGHA YA KEJELI. BILA SHAKA MWANDISHI WA MAKALA HII YA MPITA NJIA ANAWEZA AKAWA NA UMRI MDOGO KULIKO HUYU MZEE ANAYEMBEZA KWA KEJELI. HUU NI MFANO DHAHIRI WA MMOMONYOKO WA MAADILI.


MIMI NI MSTAAFU NA NAIELEWA HISTORIA YA TAASISI YA MWALIMU NYERERE. NAELEWA HAYA YALIYOSEMWA HAPA NI UZUSHI WA WAZI KABISA.

TANGU MWALIMU NYERERE AKIWA BADO YU HAI, TAASISI YA MWALIMU NYERERE ILIKUWA NA ZOEZI LA KUTAFUTA MICHANGO KWA AJILI YA KUPATA FEDHA ZA KUENDESHA TAASISI. HAKUNA ASIYEELEWA KWAMBA MWALIMU ALIPOKUWA MADARAKANI HAKUTUMIA NAFASI YAKE YA UONGOZI KUJINUFAISHA WALA KUJILIMBIKIZIA MALI. KWA HIYO NI WAZI ALIPOTOKA MADARAKANI ALIKUWA HANA FEDHA ZOZOTE ZA KUWEZA KUANZISHA NA KUENDESHEA TAASISI. LAKINI, ALIAMINI KWA DHATI KABISA KWAMBA WANANCHI NA WATU WENGINE WENYE NIA NJEMA WANGELIWEZA KUICHANGIA TAASISI.

BAADA YA MWALIMU KUFARIKI DUNIA BADO TAASISI ILIKUWA BADO HAINA FEDHA ZA KUTOSHA KUWEZA KUJIENDESHA YENYEWE, KWA HIYO KAZI YA KUTAFUTA MICHANGO ILIENDELEA HADI MWAKA HUO WA 2005 BUTIKU ALIKUWA ANAENDELEA NA ZOEZI LA KUTAFUTA MICHANGO KUTOKA KWA WANANCHI. KADI ZA MAOMBI YA MICHANGO KWA AJILI YA TAASISI ZILIPELEKWA HADI KWENYE KATA KWA AJILI HIYO.

HATA HIVYO ZOEZI HILO LILISITISHWA NAAMINI KWA NIA NJEMA BAADA YA KUONEKANA LINAWEZA KUINGILIA MCHAKATO WA KUTAFUTA MGOMBEA URAIS.

INAVYOELEKEA WAZUSHI TAYARI WALIKUWA WAMEISHACHUKULIA ZOEZI HILO KAMA NI KAZI YA TAASISI KUMPIGIA DEBE ‘MGOMBEA' WAKE!

NINAWEZA KUSEMA KWA UHAKIKA KABISA NA BILA KUUMA MANENO KWAMBA KAMPENI ZA SALIM ZA KUTAFUTA KUCHAGULIWA KUWA MGOMBEA WA URAIS HAZIKUHUSIANA HATA KIDOGO AMA KWA NJIA YOYOTE ILE NA TAASISI YA MWALIMU NYERERE AMA UONGOZI WA TAASISI HIYO.

PENGINE KUTOKANA NA KUPOROMOKA KWA MAADILI WATU WANASHINDWA KABISA KUPAMBANUA NA KUELEWA UADILIFU WALIONAO BAADHI YA VIONGOZI WA SASA NA WALE WALIOKUWA VIONGOZI WA NCHI HII HUKO NYUMA. DK. SALIM KWA UADILIFU WAKE ASINGELIWEZA AKACHEZA MCHEZO MCHAFU WA KUITUMIA TAASISI KATIKA KAMPENI ZAKE. NA NAAMINI HATA NDUGU BUTIKU MWENYEWE ASINGELIKUBALI TAASISI ITUMIKE KWA AJILI HIYO.

KUTOKANA NA NILIYOYAELEZA HAPO JUU SI KWELI KWAMBA BUTIKU ALIKUWA NA MTANDAO KWA AJILI YA DK. SALIM. KWA HIYO SUALA LA YEYE KUUVUNJA MTANDAO HUO HALIPO! NI UZUSHI USIO NA MAANA YOYOTE.


Ila kubwa lililomsukuma MN kumgusa mzee huyu, ni tabia yake iliyoibuka. Tabia hii inakuwa na isipokemewa ataipeleka nchi pabaya. Mzee huyu ameamua kufumba macho ingawa hana upofu. Haelekei kusifia hata neno alilolitenda Rais Jakaya Kikwete.

KWA MIAKA YANGU NA KUPENDA KUSOMA HABARI NIMEKUWA MSOMAJI MZURI WA GAZETI LA MTANZANIA ENZI ZA JENERALI ULIMWENGU NA AKINA BWIRE WAKIWA PALE HABARI CORPORATION. KIBONZO CHA MPITA NJIA KILIKUWA KINAHABARISHA KINAELIMISHA NA KINAKOSOA KWA LUGHA YA KISTAARABU SANA NA KUWAHESHIMU WASOMAJI. INASIKITISHA SANA KUONA JINSI AMBAVYO MPITA NJIA HUYU WA SASA ANAVYOWEZA KUTUMIA LUGHA ISIYOHESHIMU WASOMAJI WAKE!


KUSEMA KWAMBA KILA KUKICHA BUTIKU ANALALAMIKA NA KUTAKA KUWAAMINISHA WANANCHI KUWA UONGOZI WA RAIS KIKWETE UMESHINDWA KAZI, NI UCHOCHEZI NA UCHONGANISHI USIO NA TIJA. HIVI HUYU BUTIKU YEYE HANA KAZI, KILA KUKICHA KAZI YAKE NI KULALAMIKIA UONGOZI WA RAIS KIKWETE? HAPA ANAYESTAHILI KUCHUKULIWA HATUA NA KUBUGHUDHIWA NI MWANDISHI WA MPITA NJIA KWA KUJARIBU KULETA UCHONGANISHI KATI YA WANANCHI NA RAIS/WANANCHI WENGINE.


HAYA PIA NI MANENO YA KEJELI NA DHARAU KWA WANANCHI KWAMBA WAO NI MAMBUMBUMBU HAWAJUI TOFAUTI KATI YA MTANDAO UNAOZUNGUMZIWA NA MTANDAO WA KICHAMA!


HEY! UMEZALIWA LINI ‘MPITA NJIA' WA SIKU HIZI?! ENZI ZA UJIMA BABA, MAMA, MTOTO, MJOMBA, SHANGAZI, NDUGU WA KARIBU NA WA MBALI NA HATA JIRANI WALIJUANA VYEMA NA KILA MMOJA ALIJUA MWENZIWE KALA NINI NA KALALA WAPI. WENZETU WA KABILA LA WANYATURU NA WAGOGO TANGU ENZI ZA UJIMA WANA SALAMU YAO YA KILA ASUBUHI YA KUULIZANA 'UMEKULA NINI?! TOFAUTI NA ILIVYO SASA AMBAPO ‘MWENYE SHIBE HAMJUI MWENYE NJAA'!


HIVI KWELI MPITA NJIA YUKO SERIOUS ANAONA ANAO UBAVU WA KUMWELIMISHA MZEE BUTIKU MAANA YA VYAMA NI NINI? MATUNDA YA UTANUZI WA WIGO WA DEMOKRASIA NI MATAMU KWELI.

WATANZANIA TUMSHUKURU RAIS KIKWETE KWA KUPANUA WIGO WA DEMOKRASIA LAKINI ASLANI TUSIUTUMIE VIBAYA NA KUHATARISHA KILE TUNACHOKIFAIDI. TUPINGANE KWA HOJA LAKINI TUENDELEE KUISHI KWA UPENDO KAMA WATANZANIA, TUHESHIMIANE NA KUJENGA/KUENDELEZA MAADILI MEMA YA TAIFA LETU ILI TUWEZE KUENDELEA KUISHI KWA AMANI NA UTULIVU KWA MANUFAA YETU SASA NA MANUFAA YA VIZAZI VIJAVYO.

Bibi Ntilie/Mama Ntilie Mstaafu!
 
Bibie Ntilie,
Sishangai Mpita Njia anaandikia gazeti la Rostum. Kuganga njaa kubaya sana mama yangu!
 

- Hizi mkuu ni dalili za kutudharau sisi wananchi wa taifa hili, kwamba this is all we deserve ili yeye kujisafisha, inasikitisha sana hata kusikia watu wa maana kama Mpita Njia nao wamo kwenye pay roll ya mtandao ni aibu sana!

Respect.


FMEs!
 
Chipaka ni mhaini aliyejaa mawazo ya kihaini na anafikiri kila mtu ni mhaini kama yeye! kwani uhaini wake ulifutika lini? baada ya kutoka gerezani?
 
Clever post!
 

Nafikiri hapo ndio vyama vikubwa vya upinzani kama CHADEMA, CUF na NCCR wanatakiwa kuonyesha creativity and responsibility yao kwa wananchi, waorganize pia maandamano ya kuunga mkono yaliyosemwa na kupendekezwa kwenye hilo kongamano la Nyerere....kumbuka wana mass kubwa tu behind them.
 
Watakaoandamana wote siku hiyo wasife kabla ya kuonja maumivu ya ufisadi wa nchi hii!

This's just a wish, we need to do something, we need to act now! Hao unaowataka waonje maumivu walishaonja tayari for sure, it's time to make changes, and changes is all down to our own decision! If you read my signature you'll understand what I mean.
 
Mmmh! Sound like a puppet!
 
TADEA na UPDP wamechanganyikiwa. Kukosoa Serikali kwa mapungufu yake, hasa yaliyo dhahiri ni kupenda nchi yako, sio uhaini. Ni uzalendo. Hata Rais Kikwete mwenyewe amekubali kuwa hakutegemea hawa viongozi wamsifu.

Labda Chipaka wa TADEA na mwenzake Dovutwa wa UPDP wanadhani Kikwete anaweza kufikiria vyama vyao na kuvisaidia vikue, badala ya kudumaa. Hivi ni vyama vya Dar es Salaam tu, na havionekani mikoani. Waende mikoani, badala ya kukaa Dar kuita mikutano na waandishi wa habari na kushiriki ktk maandamano yasiyokuwa na tija.

Ni dhahiri kwamba CCM kama Mwalimu Julius Nyerere alivyoiasisi mwaka wa 1977 ni tofauti sana na hii inayoongozwa na Kikwete na Makamba. Kukumbatia mafisadi au kutowachukulia hatua za haraka za kisheria hakuwezi kufumbiwa macho na wazalendo kama Butiku na Mawaziri wastaafu kama wale waliohudhuria Kongamano la MNF.

Kinachotakiwa kufanywa na hawa viongozi wazalendo na jasiri ni kujitoa katika chama kinachoonyesha kinakumbatia mafisadi, na kuungana na chama chenye mwelekeo wa kushughulikia janga hili linalolikumba taifa letu la Tanzania sasa. Hata Mwalimu Nyerere mwenyewe alitamka kwamba CCM sio mama yake, na kwamba angeweza kuiacha kama haitekelezi matakwa ya Watanzania kama alivyoyajua.

Sasa kuna vyama vingi vya siasa na ni vizuri viimarishwe na vitoe changamoto kwa CCM ili ijirekebishe, la sivyo iondolewe madarakani kwa kunyimwa kura wakati wa Uchaguzi Mkuu mwakani. Huo ndio ujumbe kutoka Kongamano la MNF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…