Bw. Pompeo afanya ziara nchini Denmark bila kutaja suala la kununua eneo la Greenland

Bw. Pompeo afanya ziara nchini Denmark bila kutaja suala la kununua eneo la Greenland

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo amefanya ziara nchini Denmark ikiwa ni mwaka mmoja baada ya ziara yake kuahirishwa baada ya kauli ya Rais Donald Trump kuwa Marekani inataka kununua eneo la Greenland kutoka kwa Denmark kuzusha mvutano wa kidiplomasia.

Ziara hii inafanyika wakati Denmark haijasahau kauli ya Rais Trump iliyozua mvutano mwaka jana, na kukumbusha historia ya Marekani ya kupanua eneo lake kutokana na kununua ardhi kutoka kwa nchi nyingine. Katika baadhi ya maeneo ambayo Marekani imenunua ni pamoja na Florida iliyonunua kutoka kwa Hispania, Louisiana kutoka kwa Ufaransa na Alaska kutoka kwa Russia n.k

Pamoja na kuwa kununua maeneo ili kupanua ardhi yake si jambo geni kwa Marekani, na pamoja na kuwa safari hii kwenye ziara ya Bw. Pompeo suala la kununua eneo la Greenland halikuzungumzwa kwenye ziara ya hivi karibuni nchini Denmark, ndoto ya Marekani kutokana kununua eneo hilo haijaisha. Kinachofuatiliwa zaidi ni sababu ya msingi kwa Marekani kutokana kununua eneo hilo.

Greenland linajulikana kuwa ni eneo la kimkakati, na atakayedhibiti eneo hilo la ncha ya kaskazini anaweza kuwa na nafasi nzuri kwenye masuala ya usalama na kijeshi. Lakini pia umiliki wa Denmark kwa eneo hilo sio tatizo na sio hatari kwa nchi yoyote duniani. Na nchi za eneo hilo zimeonekana kutofurahia nia hiyo ya Marekani, ambayo ni kujaribu kudhibiti eneo hilo ili kudhibiti usafiri katika ncha ya kaskazini, na kuwa na nafasi ya juu kwenye mambo ya kimkakati..

Bw. Pompeo amefanya ziara hiyo wakati Marekani inaendelea kusumbuliwa na changamoto ya virusi vya Corona, na nchi za Ulaya Kaskazini zikiwa zimepata mafanikio kiasi kwenye mapambano dhidi ya virusi hvyo. Bw, Pompeo alitaka kumpa mkono waziri wa mambo ya nje Visiwa vya Faroe, lakini waziri huyo alikata kumpa mkono, alitaka kumpa mkono waziri wa mambo ya nje wa Denmark Bw. Jeppe Kofog naye alikata kumpa mkono, na matokeo yake, ni Bw. Pompeo alitishia kusalimiana nao kwa kiwiko.
 
Back
Top Bottom