Bw.Tundu Lissu siyo Intelligent!

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Bw.Tundu sio mtu intelligent kama watu wengi wanavyodhania, kwa maana mtu intelligent huwa ana uwezo wa kujua madhara ya kile anachokisema kabla hajakisema!

Mtu intelligent yoyote anapaswa kufahamu ktk Nchi kama TZ hauwezi kuanzisha Vita dhidi ya Mlm.Nyerere na ukashinda hata uwe nani, hata Raisi wa nchi leo hii akianzisha Vita dhidi ya Mlm.Nyerere hawezi kushinda mwishowe kuna mtu tu anaweza hata akajitoa mhanga kumlipua!

Ni sawa naleo hii Marekani mwanasiasa aanzishe Vita dhidi ya sijui Raisi Washington au Lincoln hawezi kushinda hata iweje hata kama huyo Mwanasiasa yuko sahihi kwa kiasi gani, vile vile kama ilivyo pia hakuna Mwanasiasa AK leo hii ambaye anaweza akaanzisha Vita dhidi ya Bw.Mandela na akashinda hata kama atakuwa sahihi kwa kiasi gani, na ndio maana utaona Wanasiasa wenye akili linapofika kwenye swala la hawa watu huwa wanakuwa waangalifu sana wawe ni Demokrats au Republikan hakuna anayethubutu kuwaongelea na kuwakashifu Lincoln hata kama walifanya makosa kiasi gani kwa maana wanafahamu kwamba hawa Watu nafasi yao imeshaandikwa kwenye Historia na huwezi kuifuta bila kukugharimu...

Bw.Tundu alipaswa aelewe kwamba hata kama Mlm.Nyerere amekosea kwa kiasi gani hakupaswa kumuongelea vile, alipaswa aelewe kwamba kuna watu wako tayari kufa kumtetea Mlm.Nyerere na hiyo ni Nchi nzima kuanzia jeshini mpaka Utingo wa daladala...
 
Usihangaike naye ni mgonjwa, ila watu wanamuamini sijui nao kama wazima
 
TL pale alichemsha na kiukweli itamgharimu sana
 
Unajua hawa vica ndo wanaharibu dunia. kusemwa kawaida coz Kambarage alifanya mazuri na mabaya mengi.
 
Kijakazi wa II nenda shule tena kama hujaenda kabisa tafuta mwalimu wa tuition
 
Angekuwa sio intelligent msingeleta saini za hati za Muungano.......as ingekuwa intelligent msingi kuwa mna poteza muda wa kuhangaika naye kama ambavyo sihangaiki na Lyatonga kwani sio intelligent ,,,,,,, ficha upumbavu wako......

Sijasema kama Sio Intelligent kabisa bali SIYO intelligent kama ambavyo wengi wenu mnadhania.
K
uhusu kuhusu Hati ya Muungano ingeweza kuletwa bila ya yeye kuongea aliyoongea dhidi ya Mlm.Nyerere hata kama ni ya ukweli kiasi gani, Mtu Intelligent alipaswa kutambua kwamba kuwa dhidi ya Mlm.Nyerere nchi hii utashindwa tu na mwishowe watu watakuupuzia na haijalishi ulikuwa uko sahihi kwa kiasi gani!

Huyo Babu (Mlm.Nyerere) alishawahi na hakuna jinsi mtu anaweza kubadilisha hilo hata ajaribu vipi, hivyo mtu intelligent anapaswa kutambua hilo...Waswahili tunasema Ujanja kuwahi, na yeye basi alisha wahi wengine lazima tukubali tu...

 
Kwa sababu ni mwanasheria nguli na intelligent alijua alitumia mwanya huo kuwagusa vibaya ili hati itoke. Ukiwa mwanasheria mzuri katika argument zako lazima umchokoze mpinzani wako ili akupe ushaidi zaidi. Sasa hiyo hati imeombwa miaka nenda rudi haikutoka lakini jana alipowagusa pabaya imechomoka uko speed kali
Sasa wewe unayesema siyo intelligent sijui huoni ilo? au wewe ndiye mbumbumbu
Angekuwa sio intelligent msingeleta saini za hati za Muungano.......as ingekuwa intelligent msingi kuwa mna poteza muda wa kuhangaika naye kama ambavyo sihangaiki na Lyatonga kwani sio intelligent ,,,,,,, ficha upumbavu wako......
 
Lissu amejipoteza kwenye siasa za Tanzania kwa kumtusi Nyerere na amezidi kuizamisha chadema kwenye ramani ya siasa za bongo...ni suala la muda tu..subirini upepo upite
 
@Kijakazi wa II,

..nadhani hujafuatilia mikutano na makongamano ya uamsho na kamati ya maridhiano kule Zanzibar.

..yaani likitajwa jina la Mwalimu Nyerere, basi umati unajibu kwa sauti "laanatul". wakimaanisha "aliyelaaniwa."

..hata huku Tanganyika kuna segment kubwa tu ya wananchi ambao wanaamini kwamba Mwalimu Nyerere aliwadhulumu haki zao kutokana na kutofautiana naye kiimani.

..ukiacha hao ambao wanamsema vibaya Mwalimu Nyerere, wapo wale ambao wanamtukana kwa matendo yao kwa jinsi wanavyokiuka maadili na miiko aliyoiacha Mwalimu Nyerere.

..Je, UFISADI unaofanywa na CCM siyo matusi kwa Mwalimu Nyerere?

..UBINAFSI unaoendekezwa na CCM siyo kumdhalilisha Mwalimu Nyerere?

..hao unaodai wako tayari kumhami Mwalimu Nyerere ni kina nani hao? Je, ni hawa waliokosa utu na kumumunyoa misingi yote aliyoiacha Mwalimu Nyerere?

..Hivi kweli kwa maoni yako unadhani Tundu Lissu amemdhalilisha Mwalimu, kuzidi hawa viongozi wa CCM walioua azimio la Arusha na kujilimbikizia mali kifisadi, huku wakiwaacha wananchi kwenye ujinga, umasikini, na maradhi?

cc Mkandara, Mchambuzi, gombesugu, Kasheshe, Mag3
 

nyerere hakuwa malaika ila alikuwa raia dikteta; vizuizi kwa raia
 
Watu Intelligent na munaowapenda ni wale wanaowaambia Watanzania wale Nyasi lakini ufisadi lazima ufanyike,wale wanaotuambia kama hatuna hela ya kupanda kivuko tupige mbizi,wale wanaotuambia tunawivu wa kike tukihoji matumizi ya rasilimali zetu........acheni hizo wandugu, binafsi namheshimu Nyerere lakini kama binadamu lazima alikuwa na mapungufu yake,nitarudia kusikiliza hotuba ya Lisu nione wapi ametukana Nyerere, nikipaona na mimi nitamuandikia Lisu MSG ya matusi japo katusaidia hati feki imepelekwa bungeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…