Bw.Tundu Lissu siyo Intelligent!

Bw.Tundu Lissu siyo Intelligent!

Ikiwa Tundu Lissu haoni na Chadema nzima hawaoni? Hawana mshauri ambaye anawaongoza? Hawatambui Yatakayowaharibia sura? Maana nilimtambua mwaka moja uliopita alipotamka jambo lililokuwa kero masikioni kuhusu Zanzibar. Nilidhani aliponyokwa na maneno yale na kwamba angeomba radhi lakini wapi! Utasema ana TAPE kichwani iliyorekodiwa inachezeshwa. Bila hiyo huwezi kusikia sauti yake. Ajue anajimaliza kabisa na wenzake pia.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kusema UKWELI huitaji kuwa intelligent. Lissu ana guts za kusema ukweli hata kama ni mchungu.
 
sasa toa hoja yako upate pepo.
Hoja yangu ipi unayotaka? Lissu alichosema ni sahihi kuhusu Nyerere, wala hakukosea ni ukweli mtupu, kabla ya Lissu, kusema sisi wengine tulishasema muda mrefu tabia za Nyerere...upoo!
 
He will regret it big time.
He knows, his supporters knows,his party knows.
Lakini kwa sababu ALIVUTA BANGI KABLA HAJAINGIA BUNGENI!!! haitoshi kupata msamaha
 
@Kijakazi wa II,

..nadhani hujafuatilia mikutano na makongamano ya uamsho na kamati ya maridhiano kule Zanzibar.

..yaani likitajwa jina la Mwalimu Nyerere, basi umati unajibu kwa sauti "laanatul". wakimaanisha "aliyelaaniwa."

..hata huku Tanganyika kuna segment kubwa tu ya wananchi ambao wanaamini kwamba Mwalimu Nyerere aliwadhulumu haki zao kutokana na kutofautiana naye kiimani.

..ukiacha hao ambao wanamsema vibaya Mwalimu Nyerere, wapo wale ambao wanamtukana kwa matendo yao kwa jinsi wanavyokiuka maadili na miiko aliyoiacha Mwalimu Nyerere.

..Je, UFISADI unaofanywa na CCM siyo matusi kwa Mwalimu Nyerere?

..UBINAFSI unaoendekezwa na CCM siyo kumdhalilisha Mwalimu Nyerere?

..hao unaodai wako tayari kumhami Mwalimu Nyerere ni kina nani hao? Je, ni hawa waliokosa utu na kumumunyoa misingi yote aliyoiacha Mwalimu Nyerere?

..Hivi kweli kwa maoni yako unadhani Tundu Lissu amemdhalilisha Mwalimu, kuzidi hawa viongozi wa CCM walioua azimio la Arusha na kujilimbikizia mali kifisadi, huku wakiwaacha wananchi kwenye ujinga, umasikini, na maradhi?

cc Mkandara, Mchambuzi, gombesugu, Kasheshe, Mag3

Unajua hawa wanaona makosa ya Lisu wanaangalia positive ya matendo yao bila kuangalia negative side.
 
Hoja yangu ipi unayotaka? Lissu alichosema ni sahihi kuhusu Nyerere, wala hakukosea ni ukweli mtupu, kabla ya Lissu, kusema sisi wengine tulishasema muda mrefu tabia za Nyerere...upoo!

wewe kinachokusumbua sio tabia za Nyerere kinachokusumbua unaona ata aibu kukisema...uwezi ipata pepo kwa chuki kali za namna hii swahaba..
 
Hoja yangu ipi unayotaka? Lissu alichosema ni sahihi kuhusu Nyerere, wala hakukosea ni ukweli mtupu, kabla ya Lissu, kusema sisi wengine tulishasema muda mrefu tabia za Nyerere...upoo!

Labda ni untouchable huyu bwana.
 
Watu Intelligent na munaowapenda ni wale wanaowaambia Watanzania wale Nyasi lakini ufisadi lazima ufanyike,wale wanaotuambia kama hatuna hela ya kupanda kivuko tupige mbizi,wale wanaotuambia tunawivu wa kike tukihoji matumizi ya rasilimali zetu........acheni hizo wandugu, binafsi namheshimu Nyerere lakini kama binadamu lazima alikuwa na mapungufu yake,nitarudia kusikiliza hotuba ya Lisu nione wapi ametukana Nyerere, nikipaona na mimi nitamuandikia Lisu MSG ya matusi japo katusaidia hati feki imepelekwa bungeni.

Mkuu kuna watu wanamwona Nyerere ka mungumtu vile.. Yaani hawaamini kwamba angeweza kufanya makosa. Naona hata hotuba zake hawasikilizi kwa sababu yeye mwenyewe anakiri kwamba kuna makosa walifanya kwani hawakuwa malaika. Sasa mtu anapokuja na hoja kwamba huwezi kumsema akimlinganisha na Lincoln....yeye nani asisemwe, asikosolewe??!!. Kama Lisu ktukana hata mimi siafiki na wala sishabikii hilo... Lakini kumsema, kumkosoa hiyo sawa kabisa.
 
chama cha matapeli, wameshafilisika na kujikatia tamaa kwa siasa za Tz ndo safar yao imeshawadia
 
Sijasema kama Sio Intelligent kabisa bali SIYO intelligent kama ambavyo wengi wenu mnadhania.
K
uhusu kuhusu Hati ya Muungano ingeweza kuletwa bila ya yeye kuongea aliyoongea dhidi ya Mlm.Nyerere hata kama ni ya ukweli kiasi gani, Mtu Intelligent alipaswa kutambua kwamba kuwa dhidi ya Mlm.Nyerere nchi hii utashindwa tu na mwishowe watu watakuupuzia na haijalishi ulikuwa uko sahihi kwa kiasi gani!

Huyo Babu (Mlm.Nyerere) alishawahi na hakuna jinsi mtu anaweza kubadilisha hilo hata ajaribu vipi, hivyo mtu intelligent anapaswa kutambua hilo...Waswahili tunasema Ujanja kuwahi, na yeye basi alisha wahi wengine lazima tukubali tu...

anza kujifunza kufikiri. tl ni another level.tatizo lenu maccm hamtaki kuambiwa ukweli. mnapenda kusema uongo na kutaka kila MTU auamini. ukweli utabaki kuwa ukweli. kuna mengi nyerere alifanya lakini sio sababu kuwa asijadiliwe kwa machache ambayo watu wanaona yanahitaji marekebisho.
 
Nyerere mwenyewe wakati wa uhai wake alikwisha rahisisha kwa kusema' Yeye ni babu mwenye wajukuu. Wajukuu wanaweza kumtania babu yao kwa kumshikashika kichuwani na hata kidevuni. Babu huwa hawakasirikii wajukuu wake. Babu kwa kawaida ni mtani wa wajukuu' Tundu Lisu ni mjukuu wa Nyerere. Tundu Lisu ni mpenda misifa. Anadhani akimkosoa mtu maarufu kama Nyerere atapata sifa zaidi kuliko akimkosoa Mchungaji Mtikila au hata Ali Hassan Mwinyi. He is a risk lover. The higher the risk the more the return. Ni sawa na muuza dawa za kulevya. Ukifanikiwa kuzivusha unapata faida kubwa, lakini ukikamatwa wafwa nkamu gwangu. Tusubiri atavuka au atakamatwa? Time will tell.
 
Back
Top Bottom