@Kijakazi wa II,
..nadhani hujafuatilia mikutano na makongamano ya uamsho na kamati ya maridhiano kule Zanzibar.
..yaani likitajwa jina la Mwalimu Nyerere, basi umati unajibu kwa sauti "laanatul". wakimaanisha "aliyelaaniwa."
..hata huku Tanganyika kuna segment kubwa tu ya wananchi ambao wanaamini kwamba Mwalimu Nyerere aliwadhulumu haki zao kutokana na kutofautiana naye kiimani.
..ukiacha hao ambao wanamsema vibaya Mwalimu Nyerere, wapo wale ambao wanamtukana kwa matendo yao kwa jinsi wanavyokiuka maadili na miiko aliyoiacha Mwalimu Nyerere.
..Je, UFISADI unaofanywa na CCM siyo matusi kwa Mwalimu Nyerere?
..UBINAFSI unaoendekezwa na CCM siyo kumdhalilisha Mwalimu Nyerere?
..hao unaodai wako tayari kumhami Mwalimu Nyerere ni kina nani hao? Je, ni hawa waliokosa utu na kumumunyoa misingi yote aliyoiacha Mwalimu Nyerere?
..Hivi kweli kwa maoni yako unadhani Tundu Lissu amemdhalilisha Mwalimu, kuzidi hawa viongozi wa CCM walioua azimio la Arusha na kujilimbikizia mali kifisadi, huku wakiwaacha wananchi kwenye ujinga, umasikini, na maradhi?
cc Mkandara, Mchambuzi, gombesugu, Kasheshe, Mag3
Mkuu JokaKuu,
Nimekusoma japo nipa fursa kiduchu ya kutafautiana nawe kwa baadhi ya uliyoyaandika!?
Hiyo segment kubwa ya hao Watanganyika unaodai yakua wanamtuhumu/wanamshutumu Nyerere kwa utofauti wa imani ya kidini naye...nakhis hapo unaamaanisha ni Waislam,sio!?
Hapo nafikiri umetizama hayo majambo kwa wepesi mno!? Matatizo au shutuma za Waislam hapo Tanganyika na hata Zanzibar,si kwasabu ya tafauti za imani ya kidini na Nyerere!?...hili si kweli asilan! japo inasikitisha yakua hii ndo myth ilotawala ndani ya takriban jamaa zetu wengi mno wa khasa madhahabi ya Kikristo hapo nchini!? Daah!
lakini sitawalaumu wao...maana hii ndo indoctrination ambayo hata Nyerere aliitaka ibaki hivi...yaani kuwaaminisha Watanzania woote yakua ati Waislam soote tunamjadili legacy yake au hata alipokua hai...basi ionekane ni kwasababu tu ya ati ule Ukristo/Ukatoliki wake!? Daah!
Awali ya yoote...Waislam wa hapo Tanganyika au Zanzibar,wao nao kama Wana-Adam wangine kwenye society nyanginezo takriban zoote ndani ya dunia hii...basi hawana ati mtazamo mmoja amma fikra moja!
Na hii ni pia hata kwa Hindus,Catholics/Christians,Jews,madhahabi mangineyo mbalimbali na hata wasio na imani za kidini!
Sasa kuweka sweeping statement/s kama hizo zako dhidi ya Waislam takriban woote hapo Tanganyika na Zanzibar...huoni yakua unafanza makosa ya kitaaluma, ndugu yangu!? Daah!
Pia kama kweli hayo usemayo kuhusu tafauti/matatizo ya Waislam kwa yule Nyerere ni tu sababu ya dini/imani yake ya Kikristo....sasa embu jiulize kwani yule Nyerere alipofika pale Mzizima...waliompokea,kumuhifadhi,kumuenzi na kushughulika nae bega kwa bega si walikua Waislam haohao,au!?
Sasa hao Waislam kama itikadi na dasturi yao kwa Nyerere ni sababu ya imani yake ya Kikristo tu...kama unavyotaka kutuaminisha ndugu yangu...je wakti huo Nyerere anafadhiliwa na kuthaminiwa na Waislam haohao kwani alikua ni dini gani!? Au wale Wazee Wetu/Masheikh hawakujua yakua yule Nyerere alikua ni Mkristo tena alobobea kwa imani yake!?
Hivi unafahamu yakua wakti wa zile harakati za uhuru hapo Mzizima...yule Nyerere alikua akisindikwa/akipelekwa Kanisani kwa motokari ya haohao Waislam...na pia wale Wazee Wetu/Masheikh pia wakiamrisha baadhi ya vijana wa Kiislam wampe ulinzi yule Nyerere...kwa kumusubiria nje ya Kanisa mpaka amalize sala yake na hatimae wamrejeshe nyumbani kwa salama!?
Kumbuka yakua hishma na kuthaminika kama huko,tena kwa nyakati kama zile ilikua ni kitu adimu mno...khasa ukichukulia ile background ya yule Nyerere na tafauti kubwa ya kiimani baina yake na wale Masheikh/Wazee Wetu...lakini utaona yakua kwa kiasi kikubwa mno waliishi vyema na walimthamini mno kama Mtanganyika mwenzao na pia Bin-Adam mwenzao,au!?
Kwa upande wa ndugu zetu Wazanzibary nao halikadhalika...si kweli asilan yakua ati pale Visiwani watu wanamchukia sababu ya Ukristo wake hasha,abadan asilan!
Wazanzibary takriban wengi mno na wa generations tafauti wanachukia yale matendo tu machafu alowafanzia na kuwanakamisha kimaendeleo ya kiuchumi na ksiasa na myaka mingi mno!
Pia soote tunafahamu ile complicity ya yule Nyerere kwenye takriban unyama woote uliofanzika visiwani mle dhidi ya Wazanzibary wenyewe na hata kwa Viongozi/Wanasiasa wao...au hili pia ndugu yangu unataka nikuwekee mifano lukuki hapa jamvini!? Daah! Mie najua yakua weye pia wayafahamu mangi mno na machafu yayo,au!?
Kwa kifupi,hoja zako kuhusu ati chuki za Waislam kwa Nyerere ni sababu tu ya Ukristo wake si kweli asilan!
Pana mangi mno na kwa undani mwingi pasi kiasi...tena yenye ushahidi lukuki kukhusu lawama za Waislam dhidi ya yule Nyerere...na hata baadhi ya Wakristo wengi waadilifu,wasomi na pia walioko kwenye ngazi za juu Serikalini...basi wanayakubali na kutambua ukweli huo,na pia wana-sympathise na Watanzania wenzao Waislam mpaka kesho!?
Sina hakika kama una access ya kuzungumza kiundani na Mzee Prime Minister John Malecela,Rais Benjamin Mkapa,Maokola Majogo...na wengineo wengi tu!? Sasa jaribu kuwauliza na kama wataamua kufunguka,basi nina hakika yakua hiyo taswira yako yoote na hishma umpayo yule Nyerere itayeyuka mithili ya theluji!? Daah!
Pia ikumbukwe...kama ni kweli ati Waislam wengi mno wana chuki na Nyerere sababu tu ya imani yake!?...sasa tujiulize pia,kwani yule Nyerere ndo Kiongozi pekee alokua Mkristo au mwenye tafauti na hao Waislamu!? Hapa lazim jibu ni hapana,au!?
Sasa mbona wale Viongozi/Wanasiasa Wakristo wangine wengi mno,pamoja na wale wasiokua na dini...mbona walikua wakiishi vyema tu na Waislam haohao na mpaka kesho kwa wale walio hai bado pia wanahishimika!?
Tena hapa nazungumzia Viongozi/Wanasiasa Wakristo au wasio na imani/itikadi za kidini ambao walikua na nyadhifa kubwa na nyeti mno tangia hiyo nchi inapata uhuru na wangine mpaka kesho!?
Tatizo la Nyerere inajulikana yakua yeye binafsi ndo alokua instigator wa udini,ukabila na kufumbia macho ubadhilifu na ufisadi katika takriban utawala wake woote!
Mkuu JokaKuu,bila ya kukuchosha,lakini napenda tu kukukumbusha yakua haya yoote nikwambiayo....nina ushaidi lukuki na ulo wazi kwa sisi soote kufahamu! Au utanidai niweke picha hapa jamvini,ndugu yangu!? Daah! Teeh! Teeh! Teeh!
Haya yoote nilosema,lakini pia ni uchache mno kwa nitamaniyo kunena,japo fursa nayo ndo yanikinza!
Kwa mfano bado asilan sijagusia historically,ni vipi situation ya Waislam yeye Nyerere binafsi kama Rais aliirithi/aliachiwa toka kwa wale Wakoloni!? Pia vipi yule Nyerere nae kwa sera na fikra zake alijaribu kufanza marekebisho kiduchu!? Vipi hayo "mabadiliko hayakuweza kuwa-effectively implemented kutoka na zile unsustainable mechanism/structures alizojaribu kuweka yule Nyerere bila ya kufuata ushauri wa kitaaluma au hata kuthamini hali khalis ya wakti ule,na mangineyo mangi mno!? Daah!
Ndo maana mie wakti mwangine hunilazim kucheka kiduchu...ninapoona abusive cooments za hawa baadhi ya vilaza wa history ya Taifa hilo....ati wanapowabeza wenzao Waislam,yakua ati wanatakiwa kumshukuru yule Nyerere kwa kutaifisha Shule/Skuli za Makanisa na kuwapa access ya Ilm wasome!? Duuh! Amma kweli,usilolijua ni usiku wa kiza!
Mkuu JokaKuu,binafsi kama wakumbuka uzuri naliwahi kusema katika week yangu ya awali tu wakti najiunga humu-JF...katika ule manakasha wa Maalim Mohamed Said na yule Yericko Nyerere!?...yakua Nyerere pana mangi mno na machafu alofanza sikubalinai nae asilan!
Hata hivyo,hii haimaanishi yakua ati labda hakuna baadhi ya majambo/siasa kiduchu mno nilokua nakubaliana nazo za yule Nyerere! Mara nyingi nimehudhuria Makongamano yenye kumsifu na kumjadili Rais Nyerere objectively!
Takriban sera,siasa na fikra zake nyingi mno zilikua mbovu na za uchovu wa kifikra....yaani hata kwa wakti ule! Japo pana ndugu zetu wengi mno wafia Unyerere,ambao tunaposema hivi,wao hutujia na zile cheap excuses,yakua ati Baba Wa Taifa alifanza makosa mengi au baadhi ya maamuzi yale dhaifu na ya kinyama sababu tu...ati zile pai zilikua ni nyakati tafauti na hali pia ilikua ni tafauti na sasa!? Daah!
Watu kama hao ni hatari na janga kubwa kwa hilo Taifa letu...inamaanisha hata wale Neo-Nazis nao pia waeza wakaja na cheap excuses kama hizo kukhus yule Adolph Hitler...na sisi tukubali,sio!? Maana hata zile pia zalikua ni zama?nyakati tafauti na labda hata ile geopolitic ya wakti ule yaezakuwa iliruhusu unyama ule,au!? Duuh!
Kwa kumalizia kwa leo...naona pia umegusia baadhi ya ati Viongozi/wanasiasa kwenda kinyume na "maadili" ya Baba wa Taifa...na yakua pia ati wamekiuka miiko ya uongozi na wamejikita kwenye ubadhilifu,ufisadi na kulitafuna/kulimaliza Taifa,sio!?
Ni kweli usemayo,yakua hali kama hiyo ni yakuhuzunisha mno na yatia simanzi ziso mipaka! Daah!
Lakini hiyo ndo legacy alotwachia yule Nyerere...ukweli ni kwamba hayo mazingira machafu yaliyopo hivi sasa hapo nchini, yalijengwa na kurutubiwa na yule Nyerere mwenyewe!
Japo scale/degree ya hiyo rushwa,ubadhilifu na ufisadi wakti wa zile tawala zake/"enzi za Mwalimu" ilikua labda tafauti na huo unyama uliopo hivi sasa!? Japo hii nayo ni Topic nyangine kabisa na pia ni ndefu mno!
Kwa mfano kiduchu,nafikiri soote tunakumbuka ni jinsi gani yule Nyerere alivyotumia influence,contacts na mabavu yake...ili kuhakikisha kwa hila,njama na ghilba zoote yule Ben Mkapa/chaguo lake anafanikiwa kuwa Rais!? Daah!
Nyerere aliamrisha wafuasi/misukule yake kama akina Joesph Butiku kupita nchi nzima,tena kwa kufuja senti za Wanachi ili kumnadi yule mbadhilifu,mwizi na fisadi wa kutupwa Ben Mkapa ili atwae madaraka!?
Na takriban Watanzania woote walifanza kama walivyoamrishwa/kuaminishwa kwa hishma tu ya yule Baba wa Taifa...matokeo yake Ben Mkapa akaukwaa Urais!? Duuh!
Ule unyama,ubadhilifu,ufisadi,wizi,vitisho na hata mauaji alofanza yule Ben Mkapa kwa Watanzania hao...nakhis labda hata yule Nyerere alijikhis vibaya mno!? Daah!
Sasa,lazim tujifunze namna ya kujadili baadhi ya ukweli kama Taifa!...si kutishana tu na pia baadhi ya watu kujiona wao pekee ndo labda wana haki ya kumjadili Rais Nyerere...na sisi wangine ati tunapojaribu kumjadili Rais wetu wa awali,basi tunatupiwa kashfa za udini au kuonekana tuna chuki binafsi dhidi ya Baba wa Taifa!? Daah!
Ndugu yangu JokaKuu...kama dasturi yangu,yaani nimefurahika mno kuzungumza nawe na ninakuhishimu mno kwa michango/hoja zako mbalimbali humu-JF...ambazo mingi ninakubaliana nayo!
Nakutakia jioni njema, na nitarejea pindi patapo fursa japo kiduchu!
Ahsanta.