Bw.Tundu Lissu siyo Intelligent!

Bw.Tundu Lissu siyo Intelligent!

@Kijakazi wa II,

..nadhani hujafuatilia mikutano na makongamano ya uamsho na kamati ya maridhiano kule Zanzibar.

..yaani likitajwa jina la Mwalimu Nyerere, basi umati unajibu kwa sauti "laanatul". wakimaanisha "aliyelaaniwa."

..hata huku Tanganyika kuna segment kubwa tu ya wananchi ambao wanaamini kwamba Mwalimu Nyerere aliwadhulumu haki zao kutokana na kutofautiana naye kiimani.

..ukiacha hao ambao wanamsema vibaya Mwalimu Nyerere, wapo wale ambao wanamtukana kwa matendo yao kwa jinsi wanavyokiuka maadili na miiko aliyoiacha Mwalimu Nyerere.

..Je, UFISADI unaofanywa na CCM siyo matusi kwa Mwalimu Nyerere?

..UBINAFSI unaoendekezwa na CCM siyo kumdhalilisha Mwalimu Nyerere?

..hao unaodai wako tayari kumhami Mwalimu Nyerere ni kina nani hao? Je, ni hawa waliokosa utu na kumumunyoa misingi yote aliyoiacha Mwalimu Nyerere?

..Hivi kweli kwa maoni yako unadhani Tundu Lissu amemdhalilisha Mwalimu, kuzidi hawa viongozi wa CCM walioua azimio la Arusha na kujilimbikizia mali kifisadi, huku wakiwaacha wananchi kwenye ujinga, umasikini, na maradhi?

cc Mkandara, Mchambuzi, gombesugu, Kasheshe, Mag3

Mkuu JokaKuu,

Nimekusoma japo nipa fursa kiduchu ya kutafautiana nawe kwa baadhi ya uliyoyaandika!?

Hiyo segment kubwa ya hao Watanganyika unaodai yakua wanamtuhumu/wanamshutumu Nyerere kwa utofauti wa imani ya kidini naye...nakhis hapo unaamaanisha ni Waislam,sio!?

Hapo nafikiri umetizama hayo majambo kwa wepesi mno!? Matatizo au shutuma za Waislam hapo Tanganyika na hata Zanzibar,si kwasabu ya tafauti za imani ya kidini na Nyerere!?...hili si kweli asilan! japo inasikitisha yakua hii ndo myth ilotawala ndani ya takriban jamaa zetu wengi mno wa khasa madhahabi ya Kikristo hapo nchini!? Daah!

lakini sitawalaumu wao...maana hii ndo indoctrination ambayo hata Nyerere aliitaka ibaki hivi...yaani kuwaaminisha Watanzania woote yakua ati Waislam soote tunamjadili legacy yake au hata alipokua hai...basi ionekane ni kwasababu tu ya ati ule Ukristo/Ukatoliki wake!? Daah!

Awali ya yoote...Waislam wa hapo Tanganyika au Zanzibar,wao nao kama Wana-Adam wangine kwenye society nyanginezo takriban zoote ndani ya dunia hii...basi hawana ati mtazamo mmoja amma fikra moja!

Na hii ni pia hata kwa Hindus,Catholics/Christians,Jews,madhahabi mangineyo mbalimbali na hata wasio na imani za kidini!

Sasa kuweka sweeping statement/s kama hizo zako dhidi ya Waislam takriban woote hapo Tanganyika na Zanzibar...huoni yakua unafanza makosa ya kitaaluma, ndugu yangu!? Daah!

Pia kama kweli hayo usemayo kuhusu tafauti/matatizo ya Waislam kwa yule Nyerere ni tu sababu ya dini/imani yake ya Kikristo....sasa embu jiulize kwani yule Nyerere alipofika pale Mzizima...waliompokea,kumuhifadhi,kumuenzi na kushughulika nae bega kwa bega si walikua Waislam haohao,au!?

Sasa hao Waislam kama itikadi na dasturi yao kwa Nyerere ni sababu ya imani yake ya Kikristo tu...kama unavyotaka kutuaminisha ndugu yangu...je wakti huo Nyerere anafadhiliwa na kuthaminiwa na Waislam haohao kwani alikua ni dini gani!? Au wale Wazee Wetu/Masheikh hawakujua yakua yule Nyerere alikua ni Mkristo tena alobobea kwa imani yake!?

Hivi unafahamu yakua wakti wa zile harakati za uhuru hapo Mzizima...yule Nyerere alikua akisindikwa/akipelekwa Kanisani kwa motokari ya haohao Waislam...na pia wale Wazee Wetu/Masheikh pia wakiamrisha baadhi ya vijana wa Kiislam wampe ulinzi yule Nyerere...kwa kumusubiria nje ya Kanisa mpaka amalize sala yake na hatimae wamrejeshe nyumbani kwa salama!?

Kumbuka yakua hishma na kuthaminika kama huko,tena kwa nyakati kama zile ilikua ni kitu adimu mno...khasa ukichukulia ile background ya yule Nyerere na tafauti kubwa ya kiimani baina yake na wale Masheikh/Wazee Wetu...lakini utaona yakua kwa kiasi kikubwa mno waliishi vyema na walimthamini mno kama Mtanganyika mwenzao na pia Bin-Adam mwenzao,au!?

Kwa upande wa ndugu zetu Wazanzibary nao halikadhalika...si kweli asilan yakua ati pale Visiwani watu wanamchukia sababu ya Ukristo wake hasha,abadan asilan!

Wazanzibary takriban wengi mno na wa generations tafauti wanachukia yale matendo tu machafu alowafanzia na kuwanakamisha kimaendeleo ya kiuchumi na ksiasa na myaka mingi mno!

Pia soote tunafahamu ile complicity ya yule Nyerere kwenye takriban unyama woote uliofanzika visiwani mle dhidi ya Wazanzibary wenyewe na hata kwa Viongozi/Wanasiasa wao...au hili pia ndugu yangu unataka nikuwekee mifano lukuki hapa jamvini!? Daah! Mie najua yakua weye pia wayafahamu mangi mno na machafu yayo,au!?

Kwa kifupi,hoja zako kuhusu ati chuki za Waislam kwa Nyerere ni sababu tu ya Ukristo wake si kweli asilan!

Pana mangi mno na kwa undani mwingi pasi kiasi...tena yenye ushahidi lukuki kukhusu lawama za Waislam dhidi ya yule Nyerere...na hata baadhi ya Wakristo wengi waadilifu,wasomi na pia walioko kwenye ngazi za juu Serikalini...basi wanayakubali na kutambua ukweli huo,na pia wana-sympathise na Watanzania wenzao Waislam mpaka kesho!?

Sina hakika kama una access ya kuzungumza kiundani na Mzee Prime Minister John Malecela,Rais Benjamin Mkapa,Maokola Majogo...na wengineo wengi tu!? Sasa jaribu kuwauliza na kama wataamua kufunguka,basi nina hakika yakua hiyo taswira yako yoote na hishma umpayo yule Nyerere itayeyuka mithili ya theluji!? Daah!

Pia ikumbukwe...kama ni kweli ati Waislam wengi mno wana chuki na Nyerere sababu tu ya imani yake!?...sasa tujiulize pia,kwani yule Nyerere ndo Kiongozi pekee alokua Mkristo au mwenye tafauti na hao Waislamu!? Hapa lazim jibu ni hapana,au!?

Sasa mbona wale Viongozi/Wanasiasa Wakristo wangine wengi mno,pamoja na wale wasiokua na dini...mbona walikua wakiishi vyema tu na Waislam haohao na mpaka kesho kwa wale walio hai bado pia wanahishimika!?

Tena hapa nazungumzia Viongozi/Wanasiasa Wakristo au wasio na imani/itikadi za kidini ambao walikua na nyadhifa kubwa na nyeti mno tangia hiyo nchi inapata uhuru na wangine mpaka kesho!?

Tatizo la Nyerere inajulikana yakua yeye binafsi ndo alokua instigator wa udini,ukabila na kufumbia macho ubadhilifu na ufisadi katika takriban utawala wake woote!

Mkuu JokaKuu,bila ya kukuchosha,lakini napenda tu kukukumbusha yakua haya yoote nikwambiayo....nina ushaidi lukuki na ulo wazi kwa sisi soote kufahamu! Au utanidai niweke picha hapa jamvini,ndugu yangu!? Daah! Teeh! Teeh! Teeh!


Haya yoote nilosema,lakini pia ni uchache mno kwa nitamaniyo kunena,japo fursa nayo ndo yanikinza!

Kwa mfano bado asilan sijagusia historically,ni vipi situation ya Waislam yeye Nyerere binafsi kama Rais aliirithi/aliachiwa toka kwa wale Wakoloni!? Pia vipi yule Nyerere nae kwa sera na fikra zake alijaribu kufanza marekebisho kiduchu!? Vipi hayo "mabadiliko hayakuweza kuwa-effectively implemented kutoka na zile unsustainable mechanism/structures alizojaribu kuweka yule Nyerere bila ya kufuata ushauri wa kitaaluma au hata kuthamini hali khalis ya wakti ule,na mangineyo mangi mno!? Daah!

Ndo maana mie wakti mwangine hunilazim kucheka kiduchu...ninapoona abusive cooments za hawa baadhi ya vilaza wa history ya Taifa hilo....ati wanapowabeza wenzao Waislam,yakua ati wanatakiwa kumshukuru yule Nyerere kwa kutaifisha Shule/Skuli za Makanisa na kuwapa access ya Ilm wasome!? Duuh! Amma kweli,usilolijua ni usiku wa kiza!

Mkuu JokaKuu,binafsi kama wakumbuka uzuri naliwahi kusema katika week yangu ya awali tu wakti najiunga humu-JF...katika ule manakasha wa Maalim Mohamed Said na yule Yericko Nyerere!?...yakua Nyerere pana mangi mno na machafu alofanza sikubalinai nae asilan!

Hata hivyo,hii haimaanishi yakua ati labda hakuna baadhi ya majambo/siasa kiduchu mno nilokua nakubaliana nazo za yule Nyerere! Mara nyingi nimehudhuria Makongamano yenye kumsifu na kumjadili Rais Nyerere objectively!

Takriban sera,siasa na fikra zake nyingi mno zilikua mbovu na za uchovu wa kifikra....yaani hata kwa wakti ule! Japo pana ndugu zetu wengi mno wafia Unyerere,ambao tunaposema hivi,wao hutujia na zile cheap excuses,yakua ati Baba Wa Taifa alifanza makosa mengi au baadhi ya maamuzi yale dhaifu na ya kinyama sababu tu...ati zile pai zilikua ni nyakati tafauti na hali pia ilikua ni tafauti na sasa!? Daah!

Watu kama hao ni hatari na janga kubwa kwa hilo Taifa letu...inamaanisha hata wale Neo-Nazis nao pia waeza wakaja na cheap excuses kama hizo kukhus yule Adolph Hitler...na sisi tukubali,sio!? Maana hata zile pia zalikua ni zama?nyakati tafauti na labda hata ile geopolitic ya wakti ule yaezakuwa iliruhusu unyama ule,au!? Duuh!

Kwa kumalizia kwa leo...naona pia umegusia baadhi ya ati Viongozi/wanasiasa kwenda kinyume na "maadili" ya Baba wa Taifa...na yakua pia ati wamekiuka miiko ya uongozi na wamejikita kwenye ubadhilifu,ufisadi na kulitafuna/kulimaliza Taifa,sio!?

Ni kweli usemayo,yakua hali kama hiyo ni yakuhuzunisha mno na yatia simanzi ziso mipaka! Daah!

Lakini hiyo ndo legacy alotwachia yule Nyerere...ukweli ni kwamba hayo mazingira machafu yaliyopo hivi sasa hapo nchini, yalijengwa na kurutubiwa na yule Nyerere mwenyewe!

Japo scale/degree ya hiyo rushwa,ubadhilifu na ufisadi wakti wa zile tawala zake/"enzi za Mwalimu" ilikua labda tafauti na huo unyama uliopo hivi sasa!? Japo hii nayo ni Topic nyangine kabisa na pia ni ndefu mno!

Kwa mfano kiduchu,nafikiri soote tunakumbuka ni jinsi gani yule Nyerere alivyotumia influence,contacts na mabavu yake...ili kuhakikisha kwa hila,njama na ghilba zoote yule Ben Mkapa/chaguo lake anafanikiwa kuwa Rais!? Daah!

Nyerere aliamrisha wafuasi/misukule yake kama akina Joesph Butiku kupita nchi nzima,tena kwa kufuja senti za Wanachi ili kumnadi yule mbadhilifu,mwizi na fisadi wa kutupwa Ben Mkapa ili atwae madaraka!?

Na takriban Watanzania woote walifanza kama walivyoamrishwa/kuaminishwa kwa hishma tu ya yule Baba wa Taifa...matokeo yake Ben Mkapa akaukwaa Urais!? Duuh!

Ule unyama,ubadhilifu,ufisadi,wizi,vitisho na hata mauaji alofanza yule Ben Mkapa kwa Watanzania hao...nakhis labda hata yule Nyerere alijikhis vibaya mno!? Daah!

Sasa,lazim tujifunze namna ya kujadili baadhi ya ukweli kama Taifa!...si kutishana tu na pia baadhi ya watu kujiona wao pekee ndo labda wana haki ya kumjadili Rais Nyerere...na sisi wangine ati tunapojaribu kumjadili Rais wetu wa awali,basi tunatupiwa kashfa za udini au kuonekana tuna chuki binafsi dhidi ya Baba wa Taifa!? Daah!

Ndugu yangu JokaKuu...kama dasturi yangu,yaani nimefurahika mno kuzungumza nawe na ninakuhishimu mno kwa michango/hoja zako mbalimbali humu-JF...ambazo mingi ninakubaliana nayo!

Nakutakia jioni njema, na nitarejea pindi patapo fursa japo kiduchu!

Ahsanta.
 
Bw.Tundu sio mtu intelligent kama watu wengi wanavyodhania, kwa maana mtu intelligent huwa ana uwezo wa kujua madhara ya kile anachokisema kabla hajakisema!

Mtu intelligent yoyote anapaswa kufahamu ktk Nchi kama TZ hauwezi kuanzisha Vita dhidi ya Mlm.Nyerere na ukashinda hata uwe nani, hata Raisi wa nchi leo hii akianzisha Vita dhidi ya Mlm.Nyerere hawezi kushinda mwishowe kuna mtu tu anaweza hata akajitoa mhanga kumlipua!

Ni sawa naleo hii Marekani mwanasiasa aanzishe Vita dhidi ya sijui Raisi Washington au Lincoln hawezi kushinda hata iweje hata kama huyo Mwanasiasa yuko sahihi kwa kiasi gani, vile vile kama ilivyo pia hakuna Mwanasiasa AK leo hii ambaye anaweza akaanzisha Vita dhidi ya Bw.Mandela na akashinda hata kama atakuwa sahihi kwa kiasi gani, na ndio maana utaona Wanasiasa wenye akili linapofika kwenye swala la hawa watu huwa wanakuwa waangalifu sana wawe ni Demokrats au Republikan hakuna anayethubutu kuwaongelea na kuwakashifu Lincoln hata kama walifanya makosa kiasi gani kwa maana wanafahamu kwamba hawa Watu nafasi yao imeshaandikwa kwenye Historia na huwezi kuifuta bila kukugharimu...

Bw.Tundu alipaswa aelewe kwamba hata kama Mlm.Nyerere amekosea kwa kiasi gani hakupaswa kumuongelea vile, alipaswa aelewe kwamba kuna watu wako tayari kufa kumtetea Mlm.Nyerere na hiyo ni Nchi nzima kuanzia jeshini mpaka Utingo wa daladala...

Sina uhakika kama upo deep au shallow kwenye siasa za Marekani ila kwa kifupi ni kwamba George Washington hakuwa na Chama wakati anaitawala Marekani mara baada ya kuikomboa kutoka kwa Waingereza hivyo hakuwa mhanga wa vita vya kiitikadi miongoni mwa Vyama viwili.Abraham Lincoln anaheshimiwa kwa kufanikisha kupigania haki za watu weusi pamoja na kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani.Lakini pia James Madson mmoja wa wahunzi wa Katiba bora kabisa duniani inayotumika mpaka leo kule Marekani.Ukiwaangalia watu hao walikuwa wanapigania LIBERTY ya Mwamerika ndiyo sababu leo hakuna ambacho Waamerika wanakithamini kama uhuru (LIBERTY),Uhuru wa kujieleza,Uhuru wa kuchagua chochote upendacho,Na ndiyo maana Wamerikani siku zote wamekuwa wakichukia serikali ambazo zinajaribu kufanya maamuzi kwa niaba yao kwa mfano sheria mpya ya bima ya afya (OBAMACARE) Waamerika wanachukulia kama vile serikali inawalazimisha kujiandikisha kwenye mfuko wa bima ya afya wasioutaka ila kwasababu serikali wametaka iwe hivyo.Kama unauonaga ule mnara wa LIBERTY kwa Wamatekani una maana kubwa sana,Kwa Waamerika mnara wa LIBERTY unaashiria msingi ambao taifa la Marekani limejengwa.Je waasisi wetu walilijenga Taifa letu katika misingi gani?Kama waliijenga Tanzania katika misingi ya haki kwa vyovyote vile haya yanayotokea sasa yasingeweza kutokea.Popote pale ambapo serikali ya kijamaa/kikomunisti ilikuwepo demokrasia/uhuru vilikosekana.
 
Na mamaako????!

Mento fresh maneno yako hayachagizi ww na huyo Mwanasheria wenu mmetoroka Mirembe. Ila nawashauri msiache kunywa dawa zenu mlizopewa Muhimbili kutuliza makali ya Ugonjwa wenu coz mnajua kichaa huwa haponi ila anatulia na anatakiwa asiache kunywa dawa zake mda ndio maana mnakurupuka na mineno ya ajabu ajabu.
 
Bw.Tundu sio mtu intelligent kama watu wengi wanavyodhania, kwa maana mtu intelligent huwa ana uwezo wa kujua madhara ya kile anachokisema kabla hajakisema!

Mtu intelligent yoyote anapaswa kufahamu ktk Nchi kama TZ hauwezi kuanzisha Vita dhidi ya Mlm.Nyerere na ukashinda hata uwe nani, hata Raisi wa nchi leo hii akianzisha Vita dhidi ya Mlm.Nyerere hawezi kushinda mwishowe kuna mtu tu anaweza hata akajitoa mhanga kumlipua!

Ni sawa naleo hii Marekani mwanasiasa aanzishe Vita dhidi ya sijui Raisi Washington au Lincoln hawezi kushinda hata iweje hata kama huyo Mwanasiasa yuko sahihi kwa kiasi gani, vile vile kama ilivyo pia hakuna Mwanasiasa AK leo hii ambaye anaweza akaanzisha Vita dhidi ya Bw.Mandela na akashinda hata kama atakuwa sahihi kwa kiasi gani, na ndio maana utaona Wanasiasa wenye akili linapofika kwenye swala la hawa watu huwa wanakuwa waangalifu sana wawe ni Demokrats au Republikan hakuna anayethubutu kuwaongelea na kuwakashifu Lincoln hata kama walifanya makosa kiasi gani kwa maana wanafahamu kwamba hawa Watu nafasi yao imeshaandikwa kwenye Historia na huwezi kuifuta bila kukugharimu...

Bw.Tundu alipaswa aelewe kwamba hata kama Mlm.Nyerere amekosea kwa kiasi gani hakupaswa kumuongelea vile, alipaswa aelewe kwamba kuna watu wako tayari kufa kumtetea Mlm.Nyerere na hiyo ni Nchi nzima kuanzia jeshini mpaka Utingo wa daladala...

Utabakia kuwa kijakazi namba mbili wa kijani hadi kura kwako. Nyerere ni mtu wa kawwida, kama alikuwa na mapungufu sio kuyaficha yakijulikana, ni kuyaweka wazi ili kupata katiba mpya na nzuri. Watu kuuliwa unaona ni sawa na ni jambo la kujivunia hivyo lifichwe. Kijakazi ukweli unauma na unachomachoma , vumilieni.
Hebu mtaje huyo intelligent wa kijani. Wote ni bendera fuata upepo. Maamuzi ya mwenyekiti wenu na familia yake mnaufuata kama bendera. Mnajua madhara yake? Na pia huwezi kulinganisha Tanzania na Marekani hata siku moja, historia za nchi hizi na viongozi wao ni tofauti. Katiba ya familia haitakiwi
 
Angekuwa sio intelligent msingeleta saini za hati za Muungano.......as ingekuwa intelligent msingi kuwa mna poteza muda wa kuhangaika naye kama ambavyo sihangaiki na Lyatonga kwani sio intelligent ,,,,,,, ficha upumbavu wako......

Kwahiyo saini mmeziona!, Sasa imedhihirika Ni kwa jinsi gani Tundu Lissu alivyo punguani WA akili
 
TL pale alichemsha na kiukweli itamgharimu sana
Enzi zile watu kama hawa ilikuwa baada ya wiki 1 au 2 mnakuta maiti yake ikielewa Mto Ruvu au Wami. Tumezidi kuchekeana na hayo ndiyo madhara yake.
 
Enzi zile watu kama hawa ilikuwa baada ya wiki 1 au 2 mnakuta maiti yake ikielewa Mto Ruvu au Wami. Tumezidi kuchekeana na hayo ndiyo madhara yake.

Hahahah mkuu TL angepangua hoja za nyerere sawa lakini kumtusi kuwa aliishi kijanja janja ni kuamsha hasira na malumbano yasiyo na msingi.....

TL anaiua kambi yake bila kujua
 
He will regret it big time.
He knows, his supporters knows,his party knows.
Lakini kwa sababu ALIVUTA BANGI KABLA HAJAINGIA BUNGENI!!! haitoshi kupata msamaha

Nyinyi mnaoongea hivi hamzijui siasa za leo zilivyo.Mngejua namna gani Lissu alivyokuwa mwanasiasa makini wala msingejisumbua kumtabiria mabaya,yashapitwa na wakati hayo.Hoja za Lissu zipo mahususi kwaajili ya watanzania wa kutoka kundi flani ambalo kwa muda mrefu wamekosa msemaji,kundi hili ndilo linalolielewa hoja za Lissu,Na ndilo kundi muhimu litakaloamua Rais ajaye mwaka 2015,Nyie kaeni na hayo mawazo yenu mgando na maisha yenu ya kukariri.
 
Bw.Tundu sio mtu intelligent kama watu wengi wanavyodhania, kwa maana mtu intelligent huwa ana uwezo wa kujua madhara ya kile anachokisema kabla hajakisema!

Mtu intelligent yoyote anapaswa kufahamu ktk Nchi kama TZ hauwezi kuanzisha Vita dhidi ya Mlm.Nyerere na ukashinda hata uwe nani, hata Raisi wa nchi leo hii akianzisha Vita dhidi ya Mlm.Nyerere hawezi kushinda mwishowe kuna mtu tu anaweza hata akajitoa mhanga kumlipua!

Ni sawa naleo hii Marekani mwanasiasa aanzishe Vita dhidi ya sijui Raisi Washington au Lincoln hawezi kushinda hata iweje hata kama huyo Mwanasiasa yuko sahihi kwa kiasi gani, vile vile kama ilivyo pia hakuna Mwanasiasa AK leo hii ambaye anaweza akaanzisha Vita dhidi ya Bw.Mandela na akashinda hata kama atakuwa sahihi kwa kiasi gani, na ndio maana utaona Wanasiasa wenye akili linapofika kwenye swala la hawa watu huwa wanakuwa waangalifu sana wawe ni Demokrats au Republikan hakuna anayethubutu kuwaongelea na kuwakashifu Lincoln hata kama walifanya makosa kiasi gani kwa maana wanafahamu kwamba hawa Watu nafasi yao imeshaandikwa kwenye Historia na huwezi kuifuta bila kukugharimu...

Bw.Tundu alipaswa aelewe kwamba hata kama Mlm.Nyerere amekosea kwa kiasi gani hakupaswa kumuongelea vile, alipaswa aelewe kwamba kuna watu wako tayari kufa kumtetea Mlm.Nyerere na hiyo ni Nchi nzima kuanzia jeshini mpaka Utingo wa daladala...

Here we go again, politics of conviction vs politics of convenience.

Personality cults vs principled stance.

Sasa ulitaka Tundu Lissu awe mnafiki? Apande jukwani na kumsifia Nyerere wakati moyoni anaona Nyerere alituburuza?

Mimi naona Tundu Lissu kafanya vizuri, katuambia alichofikiri moyoni tumejua kwamba si kila mtu anamfagilia Nyerere. Kama yuko sawa au la ni suala jingine, kitu muhimu kasema ukweli wake bila uoga.

Nyerere alikuwa anajinadi kama mtu asiyependa makuu, anayependa kujadili dhana zaidi ya kujadili watu.

Kwa kumkuza Nyerere kama a sacred golden cow, unakuwa hufanyi kile Nyerere alichojinadi kukifuata.

Kwa Tundu Lissu kuwa critical kwa maswali magumu kuhusu uhalali wa Nyerere na uongozi wake kutuburuza kama inavyosemekana alivyotuburuza, anafuata mstari wa kuuliza maswali magumu bila kujali yanamgusa nani.

Kama tutaendelea kuwafanya baadhi ya watu kuwa miungu wasiogusika, hatuwezi kuendelea.

Mtu anaweza hata kubaka halafu akatuaminisha kwamba amebaka katika jina la Nyerere, kwamba Nyerere alihalalisha.

Mkishampaisha Nyerere na kumfanya mungu mtu hamuwezi kumfanya kitu huyu mtu.

Nyerere alikuwa na mengi mazuri na mengi mabaya.

Nyerere kafanikisha kupangua matokeao ya uchaguzi Zanzibar, huwezi kusema huyu mtu hana mawaa, however good he was.

After all yeye mwenyewe alishakiri kuwa na mapungufu.

Wewe nani utuambie Nyerere yuko off limit?
 
Lissu kautumia vizuri utaalamu wake wa uanasheria; kwa kushambulia ili kweli ipatikane. Bila Lissu hiyo hati isingetolewa abadani. Hati haijaanza juzi kuombwa na kumekuwa na majibu tofauti tofauti kutoka huko huko serkalini, vipi leo itoke ni sababu ya mashambulizi ya Lissu. Uhalisia yawezekana ni viongozi wengi wa serikali waliostaafu na wale angali kazini wanamshukru Lissu kwa kuwapatia furusa ya wao kuiona hiyo hati kwa mara ya kwanza. Hivyo kumpuuza au kumshambulia Lissu ni kujikana mwenyewe, kwasababu usingeiona hiyo hati ya muungano hadi unakwenda kaburini.
 
Lakini kwa statement yake ya juzi na jinsi alivyomkashifu Mwalimu kwa kutumia lugha ya kihunihuni nimegundua ni wa ovyo.
Angekuwa makini angeomba radhi kwa lugha aliyoitumia ambayo kwa hakika imetukera

Ukweli ni lugha ya kihuni?

Mbona hajapelekwa Kamati ya Bunge ya Maadili na Uongozi?

Ama wewe unajua lugha kuliko wote waliopo pale mjengoni?

Kwa nini unalaumu kwa kumfunua Nyerere pekee na sio Shivji au Mwakyembe? Au kuna binadamu bora zaidi ya mwingine kwako?
 
He will regret it big time.
He knows, his supporters knows,his party knows.
Lakini kwa sababu ALIVUTA BANGI KABLA HAJAINGIA BUNGENI!!! haitoshi kupata msamaha

Kama bangi ndiyo inawatoa nishai wabunge na kuwafanya waseme ukweli wa mioyoni mwao bungeni, then I am all for legalizing it.

Huyo Nyerere mwenyewe alivyokuwa anakutana na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha DSM ikulu, na kuona hawachangamki, wamemkalia kimya katika sehemu waliyotakiwa kuwa na mazungumzo makali, aliwafungulia chupa za bia wakapunguza nishai na kufunguka.

Walatini walisema "In Vino Veritas".

Kwa hiyo kama kilevi kinahusika kuondoa nishai basi ni poa tu,

Cc : King'asti
 
Sijasema kama Sio Intelligent kabisa bali SIYO intelligent kama ambavyo wengi wenu mnadhania.
K
uhusu kuhusu Hati ya Muungano ingeweza kuletwa bila ya yeye kuongea aliyoongea dhidi ya Mlm.Nyerere hata kama ni ya ukweli kiasi gani, Mtu Intelligent alipaswa kutambua kwamba kuwa dhidi ya Mlm.Nyerere nchi hii utashindwa tu na mwishowe watu watakuupuzia na haijalishi ulikuwa uko sahihi kwa kiasi gani!

Huyo Babu (Mlm.Nyerere) alishawahi na hakuna jinsi mtu anaweza kubadilisha hilo hata ajaribu vipi, hivyo mtu intelligent anapaswa kutambua hilo...Waswahili tunasema Ujanja kuwahi, na yeye basi alisha wahi wengine lazima tukubali tu...


mkuu nikuulize swali la Msingi utanijbu?
 
Fuatilia mihadhara ya dini uone babu anavyosemwa mbaya,we we kwakujitoa ufahamu umemuona Lissu, vua miwani ya mbao jomba uweze kuona.
 
Sijui aliumwa na chadema kusema vile au alijituma mwenyewe.
 
Tundu Lissu ni wale aina fulani ya watu wanajiona wanajua sana hata mkiwa kwenye discussion hataki kusikiliza mawazo ya wengine anataka siku zote kwenye group mumsikilize yeye. Sasa hii ni weaness kubwa sana.
 
Lissu hajaanzisha vita na nyerere bhana...yeye amechambua na kuweka wazi mambo yaliyokosewa kwa makusudi kwa loopholes za sheria ama ujinga wa raia..nyie msiopenda kujua madhaifu ya wakubwa ndo mtaanzisha bifu na Lissu..Nyerere nae alikua binadamu tu.
 
Lissu hajaanzisha vita na nyerere bhana...yeye amechambua na kuweka wazi mambo yaliyokosewa kwa makusudi kwa loopholes za sheria ama ujinga wa raia..nyie msiopenda kujua madhaifu ya wakubwa ndo mtaanzisha bifu na Lissu..Nyerere nae alikua binadamu tu.

Wabongo wengi ukiwaambia Nyerere alikuwa binadamu tu mwenye mapungufu yake kibao wanaweza hata kurusha ngumi.
 
Back
Top Bottom