Bw.Tundu Lissu siyo Intelligent!

Hawa ndio intelligent hawa
 

Attachments

  • 1397580334882.jpg
    56.2 KB · Views: 416
Lisu ni comedy tu mimi nambeza sana kitambo sana.
 
Mbona Ponda na Baadhi ya Masheikh Hujawaweka humo maana Bora Tundu Lissu kuliko mikutano ya Hawa jamaa

Lissu anataka apewe nchi...hio ndio tatizo tutampa nchi mtu anayetukana baba yetu wa taifa.
 
Hawa ndio intelligent hawa

Kampeni za CCM bhana.

1. Kuleta Show na Wasanii
2. Kuweka watu maarufu kwenye Kampeni ili wavutie wananchi
3. Hakuna Elimu yeyote inayotolewa ya kiraia
 

Tatizo ni Kwamba Dunia haiko hivyo unavyodhani wewe, ndio maana nikakupa Mfano wa Marekani hao Maraisi waanzilishi kama akina Lincoln na Washington wengine walikuwa wanamiliki Watumwa ingawaje ni JAMBO BAYA lkn ni MWIKO kuwaongelea vibaya hao jamaa waliopita hata iweje na kila Mwanasiasa kama anajitaka basi huwa anatafuta tu mazuri waliyoyafanya na mabaya kuyaacha, vivyo hivyo kwa Mlm.Nyerere hapa kwetu nafasi yake tayari ipo na ameshakufa hivyo kumuongelea vibaya kama Mwanasiasa hata kama uko sahihi kwa Kiasi gani (kumbuka Dunia haiko fair) hakutakufikisha mbali, hauwezi kugeuza Maoni ya Watz leo hii dhidi ya Mlm.Nyerere hata ufanye nini bila kukugharimu na haijalishi utakuwa uko sawa kwa kiasi gani yeye (Bw.Lisu) alipaswa kulifahamu hilo...

Kuna mambo mengine haupaswi kuyasema hata kama unafikiri uko sahihi, ni hivyo tu na kwa bahati mbaya Dunia ndivyo ilivyo aliyekutangulia, amekutangualia na Mlm.Nyerere tayari ameshaweka Mark yake TZ na kuiondoa ni kazi kubwa...Bw.Tundu alipaswa kufahamu hilo!
 
Lissu anataka apewe nchi...hio ndio tatizo tutampa nchi mtu anayetukana baba yetu wa taifa.

Mtu kama.huyu ni kumuepuka ila Si kumuangalia Yeye Tu pia kuna Wananchi huku mtaani na Viongozi wa Dini wanamtukana sanaa mwalimu.mpaka wanapata Chance ya Kutengeneza VCD na DVD na zinauzwa Mtaani kabisa
 
Semeni yote, muhimu hiyo hati mmeicholopoa, sasa tunacheza na authenticity yake tukimaliza tunaenda kwenye uhalali wake, tatu mpaka kieleweke
 
Watu waajabu sana mbona Yesu kristo alifanya maajabu na miujiza mingi lakni kuna watu wanampinga mpaka leo? Sio vibaya kuhoji uwezo wa nyerere yeye hakua mungu ndo mana wanasaikolojia wakizungu waliotuponda kwenye vitabu vyao sisi tumewapinga so nyerere hakufanya mazuri tu alifanya makosa either kutokana na hakukua na multiparty system wakajisahau au kwa utashi wake
 
Hivi mtu kueleza ukweli wa tabia za Nyerere, unakuwa siyo Intelligent.

Majanga.
Kumbe kuna wasaa unakuwa kamili tu.....tuko pamoja kwenye hili , ila la mbili na tatu mimi niko tatu ...siju. Wewe
 
Binafsi, sija amini tundu lisu anapatawapi ujasiri wa kumdhalilisha Nyerere. Nahisi amechoka na maisha ya kisiasa.
hao watu waliotupa nchi huwa hawaguswi....

kudai hati ya muungano lilikuwa ni mawazo finyu tu, kwani Leo hii tusipo oneshwa hati Kuwa tumepewa Uhuru na waingereza mwaka 61' tanganyika itakuwa sio huru?

Kwa mawazo yangu, nchi sio campuni, kuna document zingine muhimu huwezi kuonesha kila mtu Akitaka......
nimeamini kuwa kusoma sio Kuwa na maarifa.......na kama huyo ndiyo mwanasheria wetu mkuu wa choma.....tunaelekea papaya..........
 

Yote hayo yanajulikana lkn ukiwa intelligent unapima maneno yako kulingana na jamii uliyoko, leo hii huwezi kwenda Israel ukasema kwamba Waisrael wanawaua Wapelestina na wanawadhulumu halafu utegemee kushinda uchaguzi Israel hata kama ni kweli Waisrael wanawadhulumu Wapalestina lkn ukitaka ushinde Uchaguzi na kama wewe ni Intelligent basi utaongea vinginevyo ndivyo Dunia inavyokwenda...
 
kijakazi wa II;9261105]Yote hayo yanajulikana lkn ukiwa intelligent unapima maneno yako kulingana na jamii uliyoko, leo hii huwezi kwenda Israel ukasema kwamba Waisrael wanawaua Wapelestina na wanawadhulumu halafu utegemee kushinda uchaguzi Israel hata kama ni kweli Waisrael wanawadhulumu Wapalestina lkn ukitaka ushinde Uchaguzi na kama wewe ni Intelligent basi utaongea vinginevyo ndivyo Dunia inavyokwenda

wewe je ulishajipima,we mbona kilaza 2?
 
Kwaiyo Lissu kusema nyerere alikua na maamuzi mabaya basi ameonekana ni mdhambi? Hivi ni wazee wangapi ambao wengi ni baba zetu ambao kimya kimya wanalaumu nakumtusi nyerere ndo aliyewasababishia umaskini? Wazee wangapi walikimbia nchi kuogopa sera za nyerere? Kuongea ukweli isiwe sababu mana ni wengi wamemtusi huyu baba nyerere lakni Lissu ndo anaonekana kakosa heshima? Ccm acheni unafiki ukweli mnaujua
 
Kwahiyo unapanga kummaliza Lisu? Bila kuweka ukweli hadharani hakuna wa kuikokomboa nchi hii, heko Lisu.
 

..mimi nadhani kwa Mtanganyika kama wewe kujua kwamba Lincoln alimiliki watumwa maana yake ni kwamba wako Wamarekani wanaomsema vibaya Lincoln.

..hata kule Soviet Union kulikuwa kuna watu walikuwa hawawezi kumsema vibaya Lenin au Stalin. Lakini kiko wapi leo.

..Mwalimu Nyerere amekuwa akisemwa vibaya kwa muda mrefu sasa. nimekupa mfano wa kule Zanzibar kwenye mikutano ya uamsho.

..hata hao CCM ni suala la muda tu, lakini wakiona inalipa kumsema vibaya Mwalimu hawatasita kufanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…