Bwalya atimka Simba S. C

Bwalya atimka Simba S. C

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Taarifa za ndani zinasema kuwa kiungo wa Simba, Rally Bwalya ameshamwaga wino wa kujiunga na klabu ya Amazulu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, lakini uongozi wa Wekundu wa Msimbazi umesema umepokea ofa ya mchezaji huyo na utakaa na klabu hiyo ya Sauzi kuona kama dili ni zuri imuuze kwa sababu bado ana mkataba wa mwaka mmoja.

“Kwenye barua yao, Amazulu wameeleza wako tayari kumpa ofa nono Bwalya na wapo tayari kutoa pesa ndefu ili kumsajili, itabidi tukae nao chini ili kuona namna gani kama tunaweza kukubaliana ili kuwapa mchezaji au kama itashindikana watamuacha mchezaji wetu,” kilisema chanzo chetu cha ndani.

Mwaka 2020 Simba ilimsajili Bwalya kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Power Dynamos ya Ligi Kuu Zambia ametumikia mkataba huo kwa miaka miwili na mwisho wa msimu ujao ndio unamalizika.

Alipotafutwa Bwalya alisema mara zote mchezaji mzuri lazima atazivutia timu nyingi mbalimbali na hilo alikuwa anakutana nalo tangu akiwa Zambia kabla ya kujiunga na Simba.

“Bado nina mkataba Simba hao Amazulu wanatakiwa kuzungumza na viongozi wangu kwa sasa sina ruhusa ya kuongea ila kama watamalizana wao huko ndio litakuja kwangu nitaona uamuzi wangu ni upi,” alisema Bwalya.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alithibitisha kupokea ofa ya Bwalya kutoka Amazulu ila bado hawajafanya uamuzi wowote kuhusu suala hilo.

Credit,
MwanaSpoti
 
Bwalya atoke tyuuh, mie kwangu full burudaan.
 
Bwalya na Kocha Pablo wote wanaenda Amazulu.

Taarifa za ndani zinasema karibu asilimia 90 ya wachezaji wa Simba wote wana ofa za kununuliwa. Msimu ujao Simba itakuwa na maingizo mapya mengi
90% ya Wachezaji wote wa Simba ni zaidi ya 20 hawa, hakuna timu itaondoa wachezaji wengi hivi sababu hata kusajili wengine Kuna limitations zake.
 
Simba kila mchezaji ana offer. Wengi wanecheza kwa mafanikio na uwezo kwenye challenge mpya upo mkubwa tu.
 
Title: Bwalya atimka Simba
Content: Bwalya akanana kutimka Simba na uongozi umekiri tu kupokea offer
 
Kwani kibudenga yeye si tumeskia anatafutwa na bayern Munich?
 
Bwalya na Kocha Pablo wote wanaenda Amazulu.

Taarifa za ndani zinasema karibu asilimia 90 ya wachezaji wa Simba wote wana ofa za kununuliwa. Msimu ujao Simba itakuwa na maingizo mapya mengi
km ni kweli,ni habari njema
 
Back
Top Bottom