Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Bwana Bonge ni mmoja wa matajari wa nchi ya Kusadikika, alimuoa classmate wake ambae alijaliwa kupata nae watoto wanne. Wakike mmoja na wanaume watatu. Watoto wote walishakua na miji yao na wengine waliishi nchi za mbali.
Mrs Bonge aligundulika na saratani ya ziwa akiwa na miaka 40, wakati hata watoto walikua vyuoni bado. Alitibiwa Ujerumani na alipata majibu kuwa wamefanikiwa kuua chembe hai zote za saratani.
Utajiri wa wenye fedha unaonekana katika maisha wanauoishi. Nyumba ya bwana Bonge ilikua juu ya mlima inaonekana hata ukiwa mbali. Ni nyumba nadhifu ya ghorofa tatu, ina vyumba nane vya kulala, cinema room, gym, sitting room tatu dining na ball room.
Katika umri wa miaka 70 Mrs Bonge afya yake ilianza kuleta mgogoro ghafla, alikwenda India kwa matibabu alikoambiwa saratani imerudi na imeenea mwili mzima. Hakukua na dawa zaidi ya za kupunguza maumivu akisubiri mauti yamfikw.
Mama Bonge ndiye alikua rafiki mkubwa wa mume wake. Habari hIzi familia ilizipokea kwa masikitiko makubwa. Watoto walikusanyika lakini baada ya muda walirudi katika miji yao. Bwana Bonge aliajiri mama wa miaka 40 ili amsaidie mama Bonge katika maswala ya usafi. Kulikua na daktari na nesi wa kuhakikisha anapata tiba ya kupunguza maumivu.
Huyu mama wa miaka 40 aliikua mrembo kweli. Baada ya kufanyia huduma mgonjwa alipiga kimini na kumfuata mzee Bonge sebuleni alikokua anapiga brandy kupunguza maumivu na mawazo. Mzee Bonge akiwa kama binadamu uzalendo ulimshinda. Mwisho alimuacha mgonjwa na kujifungia na mama wa huduma.
Mama alikua carer wa Mzee na mama Bonge kwa huduma tofauti na wote walimhitaji. Minong’ono ilizidi kuwa Mzee Bonge amemjengea Mall carer. Watoto wake waliposikia walirudi haraka, walimteka yule mama carer na kumpeleka kusikojulikana walimwambia awaeleze ilipo hati ya mall, walimpa kibano mpaka waliipata. Walimfahamisha kuwa kwa usamala wa maisha yake wanampa $10,000 apoteewna asirudi tena pale nyumbani kwao.
Mzee Bonge amepata hamaki hajui atampata wapi carer na mama Bonge analalamika kuwa carer alimhudumia vizuri lakini iweje apotee ghafla. Katika tafrani ile mama Bonge aliaga dunia. Baada ya mazishi watoto wakiamua kuishi na baba yao wakidhibiti mpunga mwingine usiende kwa mashangingi.