Bwawa la Kidunda Kuleta Ahueni Wakati wa Kiangazi Kwa Wakazi wa Dar na Pwani

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
SERIKALI kupitia Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi Bwawa la Kidunda litakalojengwa mkoani Morogoro na kugharimu sh bilioni 335. Bwawa hilo litakua na uwezo wa kuhifadhi maji kwa miaka mitatu mfululizo.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Morogoro, Kaimu Afisa Mtendaji DAWASA, Kiula Kingu amesema lengo la utekelezaji mradi huo ni kuwezesha mitambo ya maji ya Ruvu juu na Ruvu chini kuwa na maji ya kutosha ili kuzalisha maji kipindi cha kiangazi.

Aidha, Kingu amebainisha kuwa bwawa hilo litakapokamilika litakuwa lina hifadhi maji kipindi cha masika ili maji hayo yaweze kutumika nyakati za kiangazi.

Mbali na upatikanaji wa maji kwa uhakika, Kiula ameeleza faida za mradi huo na namna utakavyotoa fursa mbalimbali kwa Taifa ikiwemo ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilomita 101, uzalishaji wa umeme megawatt 20, uvuvi na utalii ambavyo kwa pamoja vitawanufaisha wananchi kwa maeneo husika kwa kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi.​
 
Safi, Kazi iendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…