Bwawa la Nyerere likikamilika umeme utapanda bei ama utashuka bei?

Bwawa la Nyerere likikamilika umeme utapanda bei ama utashuka bei?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kutokana na uwekezaji kwenye Bwawa la Nyerere kuhusisha na mikopo pia, je, lile bwawa likikamilika, bei ya umeme itapanda ama itashuka?
 
Hautapanda wala kushuka. Bali utakuwa wa uhakika!!
Uhakika siyo bei. Uhakika ni hali ya kuaminika kwamba umeme utakuwa unapatikana muda wote bila ya kukatika katika. Jee bei yake itakuwa kubwa ama itashuka toka hapa ilipo!!??
 
Uhakika ni kutoshushwa umeme.

Kupanda hakuna uhakika
 
Uhakika ni kutoshushwa umeme.

Kupanda hakuna uhakika
Jee Bei itakuwa kubwa ama itashuka. Yaani kwa sasa kama Yunit moja ni shilingi mia saba (700) jee umeme ukianza kuzalishwa kwenye bwawa la Nyerere bei yake itashuka ama ndiyo itaongezeka!!??
 
Bado natafakari kauli ya Benson kigaila ,maji ya kulijaza yatatoka wapi? Mvua ikinyesha litajaa kwa miaka mitatu ,je kwa mvua hizi za nchecheme nchecheme litajaa kwa miaka mingapi?
 
Watasingizia gharama za uendeshaji kuwa juu. Hivyo uwezekano wa bei kupanda ni mkubwa zaidi, kuliko kushuka.
 
Kama umesikia Mapendekezo ya Bei ya Treni mpya!

Basi majibu yako hapo kwa Swali lako, Watasema kabisa tumetumia gharama kubwa kufanikisha huu mradi, hivyo gharama lazima zirudi!
 
Back
Top Bottom