GE2025 Bwege atoa wito kwa Serikali kutafuta maridhiano ya Kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu 2025

GE2025 Bwege atoa wito kwa Serikali kutafuta maridhiano ya Kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilwa Kusini mkoani Lindi, Suleiman Bungala maarufu kwa jina la "Bwege", ametoa wito kwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuketi na vyama vingine vya siasa ili kujenga maridhiano ya kitaifa kuhusu masuala muhimu ya uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025 ili kuwe na matumaini ya uchaguzi huru na wa haki

Akizungumza nyumbani kwake siku ya Jumatatu Kilwa Kivinje, Bungala amesema chama chake cha ACT Wazalendo kimejizatiti kushiriki uchaguzi huo huku kikiendelea kuwahamasisha wananchi kulinda kura.

Bwege amesema kuwa chama hicho kina nafasi ya kushinda si chini ya majimbo saba katika mikoa ya kusini endapo kitaweka mkakati madhubuti kuelekea Uchaguzi huo.

Amesema kuwa ukanda wa Kusini bado unakabiliwa na changamoto kubwa za kijamii na kiuchumi, ambazo zinahitaji uongozi wa kisera na usimamizi wa karibu kwa maslahi ya wananchi.

Akizungumzia hali ya wananchi wa ukanda wa Kusini, Bungala ametaja changamoto kubwa zinazowakumba wavuvi wa eneo hilo akisema nyavu zao zimekuwa zikichomwa moto ‘kiholela’, huku ukosefu wa elimu bora, huduma za afya na umaskini vikitajwa kuwa changamoto zinazozidi kukwamisha maendeleo.

Amesema sasa ni wakati wa wananchi wa Kusini, hususan wa Kilwa, kuungana na ACT Wazalendo ili kuleta mabadiliko ya kweli kwenye uongozi na ustawi wa maeneo yao




​
Chanzo: Jambo Tv
 
 
Back
Top Bottom