Selemani Said Bungara 'Bwege' amesema alikuwa anashiriki katika uchaguzi na kukiuza chama chake cha ACT Wazalendo, lakini tokea Mgombea wa Urais kupitia Chama chake, Luhaga Mpina aenguliwe ameona ni kama wagombea wote wa udiwani na ubunge kupitia chama ACT Wazalendo wameenguliwa kwasababu nafasi ya Urais ndio nguzo kubwa.
Ameyasema haya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Manzese, jijini Dar es Salaam, Oktoba 18, 2025.
A
Nimemsikiliza Bwege leo. Sijamsikiliza pote, ila nimesikia kwa kiasi kikubwa.
Ameongea mambo mengi sana. Sijakubaliana naye kila kitu, ila kuna mambo machache nimemuelewa.
Mambo ambayo sijakubaliana na Bwege.
Bwege anampa sana nafasi Rais Samia. Kwamba Samia ana nia nzuri, ila anakwamishwa na wasaidizi wake tu.
Sijui kama hii ni euphemism tu, analinda mahusiano, au ni utamaduni wa kumuheshimu rais sana tu. Ila hili limepelekea mpaka vijana fulani kufikiri Bwege kalamba asali.
Nimesikitika sana kusikia vijana wakisikia mtu ana mawazo tofauti, hata kama mtu ni moderate tu kifalsafa, kitu cha kwanza wanacjosema ni kuwa huyu kalamba asali.
Pia, suala la Lihaga Mpina hata kama kazuiwa na CCM Luhaga Mpina mwenyewe alishaharibu kwa kuchakachua utaratibu wa kugombea ugombea urais kw akupitia ACT. Ali uchujua utamaduni wa uchakachuaji utaratibu kutoka CCM akaupeleka ACT. Mwanachama wa AcT Monalisa Mdala akam challenge Mpina, QCT na Mpina mpaka leo hawajajibu hoja za Monalisa.
Masuala ambayo nimekubaliana na Bwege.
Bwege ameasa watu kutofanya maandamano tarehe 29 October, akisema, kwa lugha yake ya kufikisha ujumbe kwa urahisi kabisa kwamba Maji hayajachemka hatutaweza kupika ugali.
Alieleza kuwa siku ya uchaguzi watu wasiandamane. Waandamane kabla au baada ya uchaguzi.
Hili jambo hata mimi nilishauri, lakini watu wengi hawakulipenda.
Pia, Bwege ameasa watu kuachana na habari za kutaka jeshi lichukue madaraka ya kuongiza nchi. Hili jambo watu wanalishabikia sana siku hizi, almost like in desperation. Kwangu mimi ni contradiction kubwa sana kutaka kurudisha demokrasia kwa mtutu wa binduki. Hatujui wanajeshi watatawala vipi, hatujui kama wataondoka, hatujui tutatengeneza precedent gani, ni kitu kibaya sana kuliko wengi wanafikiri.
Unatetea vipi jesho kuchukua nchi kuleta utawala wa kidemokrasia wakati jeshi liki hukua nchi lina suspend utawala wa kikatiba?
Hivi watu wanaotetea jeshi kuchukua nchi wanaelewa hili jambo maana yake nini?