GE2025 Bwege: Vyama vyote vya upinzani vilipaswa kuungana kususia uchaguzi kudai reforms

GE2025 Bwege: Vyama vyote vya upinzani vilipaswa kuungana kususia uchaguzi kudai reforms

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kada wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa zamani wa jimbo la Kilwa Kusini Selemani Saidi Bungara (Bwege) amesema anaamini kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiko sahihi kusimamia 'No Reforms, No Election' na kwamba vyama vyote vya upinzani nchini ikiwemo chama chake ilipaswa waungane pamoja 'kususia' uchaguzi wa mwaka huu badala yake wangepambana kudai 'reforms'

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Septemba 04.2025 mwanasiasa huyo mkongwe nchini amesema hafurahishwi kuona ndani ya vyama vya upinzani kuna kile alichokitaja uwepo wa 'madalali' ambao wamekuwa wakitumika kwa namna moja au nyingine kukandamiza vyama vyao kwa maslahi yao binafsi.


Tofautisha vyama na projects za wenye nazo:

GzyBB2MXsAA_nEH.jpeg

GfF9ragacAAWv7q.jpeg
 
ACT shida ni Zitto ambaye siyo mpinzani wa kweli. Anawatumia wenzake kwa maslahi yake.
 
Njaa na tamaa za watanzania,ukiondo chadema vyama vingine vya upinzani haviwezi kuwasimamia wananchi ,wanajali matumbo tu
 
Njaa na tamaa za watanzania,ukiondo chadema vyama vingine vya upinzani haviwezi kuwasimamia wananchi ,wanajali matumbo tu

Wasaliti wapo kila mahali hata Yesu aliyekuwa akifufua watu alifufuliwa. Sembuse wahunin waliopenyezwa kote? Pa kuanzia ilikuwa kuwakataa wahuni wote bila kujali walipo!

Angalizo la Polepole la Wahuni kuwa kila mahali linaonekana kutoeleweka bado. Hata upinzani, Sauti ya Tanzania, TLS, nk, ni dhahiri kuwa nako wapo!

Zingatia hata chadema wahuni wangalipo na hawatakaa waishe.

Kataa wahuni, si watu wazuri!
 
Back
Top Bottom