Blueprint 9
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 798
- 1,381
Tahadhari mimi sio dogo sawawacha uboya dogo
tunaongelea majukumu makubwa ya kuiwakilisha nchi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tahadhari mimi sio dogo sawawacha uboya dogo
tunaongelea majukumu makubwa ya kuiwakilisha nchi
wewe ni dogo mimi bro wako, kuwa na nidhamu kwa wakubwaTahadhari mimi sio dogo sawa
Usikute upo kwenye sofa la mume wa dadako muda huu umetuna unasubir lunchwewe ni dogo mimi bro wako, kuwa na nidhamu kwa wakubwa
Hivyo unataka kusemaje mwaka huu mtafanya kipi? Nataka nihifadhi kauli yako. Enheee. 👂👂Japo mpira hauchezwi kwa historia lakini nikujuze tu kua hao National Al Ahly walishawahi kupakatwa na Simba mwaka 1984 pale CCM Kirumba Mwanza, shukran kwa mabao ya Zamoyoni Mogella na Mtemi Ramadhani. Wakati huo Ahly walikua ndio mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Afrika na wakiwa na wachezajai hatari kama Mahmoud El Khatib, Abdul Mustafa, beki Rabia Yassin na golikipa mahiri kabisa Shahat El Ikram, japo aliyetunguliwa Kirumba alikua Ahmed Showeib
As Vita walikuja Bongo mwaka 1979 kukipiga na Pan Africa kwenye Kombe la Washindi la Afrika (Cup Winners Cup) na walipakatwa kwa bao mbili kwa moja. Wakati huo baba yake Haji Manara yaani Sunday Manara na ndugu zake kina Kitwana na Kassim waliichezea Pan siku hiyo kwenye mtanange uliopigwa Sheikh Amri Abeid kule Arusha, japo kwenye mechi ya marudiano AS Vita walishinda 1-0 hivyo kusonga mbele kwa bao walilolipata ugenini
Vita walikua na wachezaji machachari sana kina Lobilo, Mayanga, Lufombo n.k lakini Pan nao walikua wamekamilika. Kikosi chao kilikua na kina Juma Pondamali, Leopord Tasso Mukebezi,Jaafar Abdurahman, Mohamed Mkweche, Leodger Chillah Tenga, Jellah Mtagwa, Mohamed Richard Adolf, Hussein Ngulungu, Ali Katolila, Peter Tino, Sunday Manara , Kitwana Manara, Kassim Manara, Gordian Mapango n.k
Huyu Kassim Manara alikua mtata sana kama alivyo Haji na katika mechi ya marudiano pale Kinshasa alitaka kupigana kavukavu na Lobilo
Ni katika mwaka huo mnyama Simba ndio aliishangaza Afrika kwa kuitoa Mufulira Wanderers ya Zambia kwa kuitandika bao tano sifuri kwenye uwanja wa Independence pale Lusaka mbele ya Rais Keneth Kaunda. Hii ni baada ya kua Simba walikubali kichapo cha bao nne sifuri kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Simba ilitolewa kwenye round iliyofuata na waliokua tena mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Afrika, Union Despotive Douala ya Cameroon
Nimekupa historia kidogo ili uone hili klabu la Simba lipo level moja na maklabu makubwa kama vile Klabu la Tu Poisant Englebert Mazembe ya kule Lubumbashi. Pale inapokua imetolewa hua ni kwa mbinde sana na inakua imetolewa na matimu makubwa ambayo hatimaye yananyakua ubingwa
Kama una swali uliza Shadeeya ,nataka leo nikupe hadi uridhike kabisaa
ngoja nikupuuze tuUsikute upo kwenye sofa la mume wa dadako muda huu umetuna unasubir lunch
Wewe mwenyewe unajua hamna binadamu yeyote yule asiyemuogopa simba, tutapita kwa uwezo wa Allah, pia hongera kwa ushindi wa leo pale Sokoine, mwenzio azam kapokea kipigo pale turiani, kwenye mechi yenu ya kumalizia mzunguko wa kwanza na azam itakuwa niya kufa na kupona, hope azam atatoboa tundu.Insha Allah na iwe hivyo Mtani japo najua utayakataa haya maneno.
Hahahaaa. Tusubiri tuone jirani.Wewe mwenyewe unajua hamna binadamu yeyote yule asiyemuogopa simba, tutapita kwa uwezo wa Allah, pia hongera kwa ushindi wa leo pale Sokoine, mwenzio azam kapokea kipigo pale turiani, kwenye mechi yenu ya kumalizia mzunguko wa kwanza na azam itakuwa niya kufa na kupona, hope azam atatoboa tundu.
Tumepewa kweli Al ahlymuda umekaribia hapa
Mungu baba tuepushie wydad, mazembe na esperence
Naomba utupe Al ahly, hawa tutawamudu vilivyo.
Sent using Jamii Forums mobile app